Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Mkuu huenda JokaKuu naye amehesabiwa na Lowassa? Uhuni wote wa Lowassa pale Amri Abeid bado Lowassa ni kielelezo l kulinganisha na wengine?

Hii kauli ya Lowasa ya simama uhesabiwe inanipa wasiwasi mkubwa sana! Tujadile kidogo nini maana ya kauli hii!

Nikianza mimi mwenyewe inamaanisha kwamba, asije mtu yeyote baada ya Lowasa kupitishwa na chama chake akajifanya naye alikuwa naye pamoja, huyo hana nafasi ya kuvuna mapesa baada ya kuwekeza pesa ndefu kwa jamii.
 
Last edited by a moderator:
Katika CCM mgombea pekee anayeweza ku_shake up the system ni Nchemba,sina uhakika na Makongoro,ngoja nimsikilize naye.
 
Hauwezi kuwa umemsikiliza mwigulu

Nimemsikiliza ndio mana nimesema hivyo. Mfano anasema ataifanya Nchi kuwa ni ya viwanda, atahakikisha watu wanaacha kufanya kazi kwa mazoea nk. Hajatwambia HOW ataifanya nchi ya viwanda? Tuwapime wagombea WOTE kwa "HOW" zao sio kwa ahadi tu, hata wewe unaweza kusema ntaifanya nchi iwe na flyovers kila kwenye junction ya barabara! Udipotuambia HOW, Then ni ngonjera tu kama za kwenye kanga
 
Mwigulu ni miongoni mwa wanachama wachache sana wa CCM ambao unaweza ukatafuta kashifa zao ukashindwa kupata kashifa hata moja inayo mgusa,kama ilivyokuwa kipindi kile cha Mkapa alipo pitishwa na CCM,wapinzani wake walishindwa kabisa kumzushia kashifa kwa kuwa alikuwa hana kashifa yoyote.

Mwigulu akijitahidi kujitenga na baadhi ya mambo ya chama chake ambacho kimejaa viongozi wenyekashifa,hasa hili la kutumika na chama chake kutaka kuua upinzani ambalo linamfanya awe muongo,ana weza akawa kiongozi mzuri sana.

Either humjui Mwigulu vizuri, au unamjua sana ndio maana unamfichia madhambi yake. Mwigulu hana kashfa? Unga urafiki na Ludovic yule aliewahi kuwaga rafiki wa Lwakatare wa CDM then muulize huyo Ludo issues za Mwigulu.

Au tafuta rafiki Vodacom kisha akufanyie udukuzi wa mawasiliano kati ya hawa watu wawili. Angalizo tu ni kua do this at your own risk
 
ni gaidi linalotapatapa kulipua bomu likafel lazima life lenyewe huyu ameacha unaibu ataacha uwaziri na ubunge ajajua rais atakuwa nani kama ni kutoka ukawa ajiandae kulima mtama kiomboi kisiriri
 
Kwa hiyo kila jema likiongelewa na CCM ni idea ya upinzani?

Mwigulu ni jembe na ni kiboko ya upinzani, lazima mpanick..

Katika watu wasiotufanya tuwaze ni huyo yani ingetokea bahati mbaya ccm wakampa hiyo nafasi wangetupunguzia gharama sana mana tungefanya kampeni za madiwani na wabunge tu na urais tungekuwa hatuna haja mana yy nisawa na jiwe
 
Tuache utani, na ushawishi Mwigulu hafai kwa lolote, hata uwaziri wenyewe unampwaya. Ni mtu hatari kwa umoja wa kitaifa: mtu ambaye yuko tayari hata kuua, ambaye hamuungi mkono. Kumbuka mauaji ya Arusha alipokuwa ameweka kambi, na kupoteza majimbo yote. Kwa ushauri wangu, Mwigulu apewe nafasi zaidi ya kuchunguzwa, atajifunua wazi jinsi alivyo.
Kwa maoni yangu anafaa kuwa jasusi, ajiuunge nao kama bado.
Watu tunaridhika tu akituimbiwa wimbo wake kuwa katoka familia maskini, kwani nani hakutoka huko?
Yupo ndani ya serikali iliyotufukarisha, na inaendelea kufukarisha anafanya nini cha msingi isipokuwa kutuhadaa na hadithi zake kuwa katoka familia maskini?
Tatizo tunasahau haraka.
unaleta hekaya za KIBAVICHA katika mambo ya msingi!!
kwa taarifa yako tu ni kwamba baada ya NCHEMBA kutangaza nia, hata LOWASA chupi inambana sembuse nyie wapumbavu??
 
ile kushindwa kudhbiti sarafu against dollar ni udhaifu mkubwa


Naamini akiwa na Mamlaka kamili anaweza kufanya hicho unachokisema,lakini kwa mamlaka aliyonayo,anaweza akashauri jinsi ya kuidhibiti hyo dollar na akapuuzwa tu na watawala
 
Hata mimi nilishuhudia jamaa akiiponda na kuikosoa serikali ya chama chake mwanzo mwisho.....in short aliongea kama anatoKa opposition. I la sio mbaya maana lengo lake ni kutaka kujaribu kuleta mabadiliko ndani ya chama chake ambayo wananchi wanayataka ambayo wakiyakosa huko watayafata UKAWA.
 
Hayo ni mawazo yako kijana, Ccm ndo baba na mama wa maendeleo yote uyaonayo hapa nchini wengine hao watasubiri sana, kaeleweka sana wewe tu umetumwa kwa mambo yenu binafsi, angalia njaa itakuua kijana.
Pia CCM ni baba na mama wa umaskini uliokithiri
 
Wanataka kufanya nchi hii ya
majaribio....kila mtu anataka uongozi tena uraisi.... Ivi uraisi umekua rahisi kiasi iki??

Uko nyuma bado kuna wenzake kibao wanafata. Eti nia... Uuuuuiiiii tutakoma safari hii

Tena tutakoma haswa, woooote wanaongea sera zilezile walizoshindwa kuzitekeleza, yaani hawa watu wametuona sie kama nyani wa porini kabisa, hatuoni nchi inavyokwenda kazi kweli.
 
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ametangaza nia yake ya kugombea urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba akieleza jinsi atakavyoivusha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati utakaopatikana kwa kutoa haki kwa watu wote.

Akitangaza nia hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Mipango Dodoma, Nchemba alisema: "Ahadi yangu kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha. Nitawavusha wanaCCM wenzangu pamoja na Watanzania kwa ujumla… wakati ni sasa tunataka Taifa letu lifike kuwa nchi yenye uchumi wa kati," alisema Nchemba na kuongeza:

"Ninachoomba kutoka kwenu, mniamini na mniunge mkono katika hili… nitawavusha. Lakini tukumbuke kwamba kila mmoja lazima atimize wajibu wake katika utendaji kazi ili tufikie huko tunapotaka kufikia."

Nchemba aliyekuwa ameongozana na mkewe, Neema na watoto wake watatu, Isaack, Grecious na Joshua pamoja na ndugu jamaa na marafiki, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo hayo, lazima nchi iwe na mfumo wa uwajibikaji utakaowezesha kulinda rasilimali za Taifa na kuongeza Pato la Taifa.

Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko ni Matendo, Wakati ni Sasa', ambayo ataitumia katika safari yake ya kuelekea Ikulu, Nchemba aliyetumia dakika 115, kuanzia saa 10.10 jioni hadi saa 11.25 jioni, alisema atapambana na tabia za watu kufanya kazi kwa mazoea, rushwa, ufisadi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano atakayoiongoza endapo atachaguliwa, itakuwa ya uadilifu na uaminifu.

Alisema iwapo atachaguliwa, ataifanya nchi kuwa ya kipato cha kati sambamba na watu wake, kujenga Taifa linalojitegemea kibajeti na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.

Huku akieleza jinsi atakavyomaliza kilio cha ukosefu wa ajira, wanafunzi, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara na watu wa kada mbalimbali nchini, Nchemba alianza hotuba yake kwa kuwashukia baadhi ya watu wenye dhana potofu juu ya mtu anayestahili kuwa rais wa nchi.

"Nimeamua kutangazia nia hapa Dodoma kwa sababu ndipo makao makuu ya nchi na kama nikiwa rais nitaapishiwa hapa. Pia sikutaka kutangazia nia nyumbani Iramba ili kuondokana na umimi," alisema na kushangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.

Awajibu wanaomponda
"Uzoefu ni mazoea ya starehe. Mtu aliyekaa katika uongozi ni mtu aliyesahau shida za Watanzania.
Jambo la kwanza na la msingi ni kuitambua ajenda ya Watanzania, Watanzania watamuunga mkono kiongozi kwa kuitambua ajenda yake," alisema.

Alisema wakati akijitathimini kutangaza nia ya kugombea alikuwa akifahamu ajenda ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa umaskini hakuusoma katika vitabu, bali amekulia katika maisha ya kimaskini.
"Ukizungumzia ukosefu wa ajira na dawa hospitali hilo sijalisoma vitabuni, ukizungumzia ajira kwa vijana na watu wote hilo jambo sijalisoma vitabuni."

Alisema katika pitapita zake, amesikia habari za mtu anayefaa kuwa rais zikihusishwa na umri na uzoefu, "Ujana na uzee haviwezi kuwa sifa ya kuiongoza nchi. Kukaa serikalini muda mrefu haiwezi kuwa sifa ya kutosha kuliongoza Taifa hili, unaweza ukakaa sana serikalini lakini ukasababisha hasara kubwa.

Hata kuishi ni hivyohivyo, kinachoangaliwa si kuishi miaka mingi, bali ni kipi ulichokifanya. Leo hii marehemu (Edward) Sokoine hakumbukwi kwa sababu alikaa sana serikalini, anakumbukwa kwa matendo yake kwa kipindi kifupi alichokaa serikalini."

Huku akishangiliwa alisema, "Kiongozi akipatikana kwa mazoea atafanya kazi kwa mazoea. Vita ya kwanza tunayotaka kuikomesha katika nchi yetu ni kufanya kazi wa mazoea. Tunahitaji mambo matatu; mabadiliko, mbinu za kufanya mabadiliko na utayari wa kufanya mabadiliko."

Kuhusu umri alisema: "Wengine wanaongelea umri wamesahau kuwa Katiba inasema umri wa kugombea ni miaka 40, hata vitabu vitukufu vimeandika kwamba umri wa miaka 40 ni sahihi mtu kupewa utume na unabii, Mussa alipofikisha miaka 40 aliaminiwa kwenda kuwakomboa ndugu zake."

Alisema hata Mwalimu Julius Nyerere alikuwa rais akiwa na miaka 40, tena akitoka kufundisha sekondari.
"Watu wanataka kuwatoa Watanzania katika ajenda kwa kuzungumzia vitu vyepesi. Eti wanasema ukimaliza kuwa rais wakati bado kijana utafanya nini. Nifanye nini tena wakati nitakuwa nimeshamaliza kazi. Najipambanua kwa ajenda yangu na wale watakaoniangalia wataangalia ajenda yangu," alisema.

Mipango yake
"Kwa miaka 50 tumekuwa tegemezi, sasa imetosha tunakwenda kujitegemea. Kujitegemea ni kila mmoja kulipa kodi anayostahili," alisema.

Alisema wakati wa watu wachache kubeba mzigo wa kodi umefikia mwisho na kwamba kila mtu anayestahili kulipa atailipa, awe mdogo au mkubwa.

"Tunakwenda kuachana na utaratibu wa kukimbizana na wauza vitumbua kuwadai kodi. Kujitegemea ni nidhamu ya matumizi na sasa tunakwenda kuziba mianya ya rushwa," alisema.

Alisema ili uchumi umilikiwe na Watanzania wenyewe, lazima njia za kuwapatia watu kipato ziboreshwe kwa sababu uchumi wa nchi unakua lakini wananchi bado wanalia umaskini.

"Njia ya kuwatoa hapo walipo ni kuongeza thamani ya mazao na kazi wanazozifanya kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania ni wakulima. Lazima wakulima watafutiwe pembejeo na masoko. Tunatakiwa kutumia sekta binafsi ili kuwa na viwanda vingi nchini," alisema na kutoa mfano:

"Pamba ya Tanzania inaweza kutumika kutengeneza sare za shule, za jeshi na viatu kutoka katika viwanda vilivyopo nchini. Tuna wanafunzi zaidi ya milioni nane na kila mwaka wanaandikishwa shule, kwa nini tulilie soko la nje halafu sare zao tunanunua nje."

Kuhusu mafuta, Nchemba alisema kilimo cha alizeti kikiboreshwa kitazalisha ajira nyingi na hilo linaweza kufanyika pia katika sukari, kahawa, chai na korosho.

"Awamu ya tano, nchi itaingia katika uchumi wa viwanda na vijana watafanya kazi kwa kupokezana," alisema.

Mwigulu aligusia suala la Watanzania kutozwa kodi zisizokuwa na kichwa wala miguu na zisizoendana na uzalishaji wa biashara husika, huku akitolea mfano mama ntilie na wamachinga.

"Wakubwa wakitaka kuwekeza wanapewa likizo ya miaka 10 ya kulipa kodi lakini anayefungua saluni anatozwa kodi wakati akiwa anapaka rangi jengo hata biashara hajaanza," alisema na kushangiliwa.
Rushwa.

Akizungumzia rushwa alisema: "Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na kurejesha nyuma maendeleo na hupindisha ukweli na kuwanyima haki maskini."

Alisema awamu zote nne za Serikali zimejitahidi kupambana na rushwa, ila awamu ya tano itakuja na njia tofauti kwamba atakayethibitika kupokea au kutoa rushwa atachukuliwa hatua haraka ili iwe fundisho.

"Sasa hivi mtu akikamatwa na rushwa kesi zimekuwa na mlolongo mrefu. Tutabadilisha Sheria namba 11 ya Kupambana na Rushwa ili kuipa meno Takukuru iweze kushughulika na suala hili na atakayebainika atafilisiwa, kufukuzwa kazi na kufungwa," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Tunaitaji mkanda wa mauwaji ya soweto ukitupa basi tunakupa urahisi sio urais.


swissme
 
Back
Top Bottom