Kutoka Bungeni: Sugu ajibu tuhuma za kupora mtoto kutoka kwa mzazi mwenzake

Status
Not open for further replies.

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
sugu-300x300.jpg

Baada ya jana Martha Mlata kumtuhumu Sugu kumpora mtoto toka kwa mama yake amemuomba Spika kutoa maelezo binafsi. Kwanza anakiri mtoto ni wake, na anasema watu wazima hawazungumzii mambo ya ndoa za wenzake na anasema ni mambo binafsi.

Anasema binti yake ameishi Dar tangu mwaka 2012 na amekuwa akilipa laki tano kila mwezi na milioni 3 kwa mwaka kama karo.

Anasema mzazi mwenzake amekuwa akivaa nusu uchi na kuacha sehemu za siri nje.

Anasema Mlata anayejiita mlokole hawezi kutetea maovu kama hayo, na yeye hasemi kwa nini ndoa yake ilivunjika .

Anasema kile kinachodaiwa kuwa kumpora mtoto ni hukumu ya mahakama na Mlata hakuwa shahidi wala hana uhakika kama hata mtoto mwenyewe anamjua.

Anasema kwa kuwa ni mambo ni ya faragha hata Mlata asingetaka mambo yake na mabwana zake wa sasa yajulikane.

Anasema hata mtoto hajamchukua na ameacha maswala ya kifamilia yachukue mkondo wake.

Ndugai anasema suala hili liachwe maana linaweza kumuathiri kisaikolojia hata shule.

Anawataka waandishi wa habari kuliacha suala hili.
Sugu anatokwa na machozi kwa uchungu.

Bonye HAPA Kumsikiliza Mh. Joseph Mbilinyi



Melezo ya Joseph Mbilinyi "SUGU"

"Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi jana tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo"


"Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang'anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia"

"Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika"

"Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito"

"Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge"

"Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niiwashilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee. Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge"

"Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi. Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa"

Mbunge Joseph Mbilinyi.
 

Attachments

  • sugu na sasha.mp3
    5.1 MB · Views: 8,024
Kaka si ungepiga kimya tu kaka. Kuongea yote hayo ya nini? Maswala ya mahusiano unayaweka bungeni ?Sugu sugu sugu!!!!!!!!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom