....Mkuu,hebu fafanua kidogo kwa hilo la AFYA....je unamaana akajiuzulu kwa sababu nyingine licha ya hiyo ya Afya Nchi haitamuelewa au??,najua hapa Nyumbani(TZ) Afya za watu/public figures huwa ni siri binafsi je Mkulu anahistoria yeyote ya matatizo ya Ki-afya??Mimi naisubiri sana siku atakapojiuzulu sababu ya afya ...ili aepuke aibu iliyo mbele yake...alidhania uraisi ni rahisi hivyo???apumzike sababu ziko nyingi sana kubwa iwe afya.....inatosha aichie nchi.........hana jipya wala hajawahi kuwa nalo
anaongea na wazee saa 11 jioniHio hutuba haijaanza? Please hebu tupeni mlenda nasi tushushie
hivi wakuu, huu utaratibu wa kuhutubia 'wazee' umekaaje nchi hii? Hao wazee ni kina nani hasa na mtu anatakiwa awe na umri/qualification gani ili aweze kuingia kwneye hicho kikao cha 'wazee'? Je ni wale waliopigania uhuru? Kama ndivyo ni wangapi wapo hai, na kama wapo, wana uelewa gani wa mambo yanayoendelea sasa hivi duniani?
Naombeni msaada wenu katika hili, maana kila kukicha nasikia mara raisi analihutubia taifa 'kupitia wazee' mara leo atahutubia wabunge....jamani wabunge.....kupitia 'wazee' vilevile....sasa sijui tunakoelekea ni wapi? Na hapa sina maana ya kuwadharau wazee, hapana, ningependa tu kujua hao 'wazee' wa miaka yote ni kina nani hasa? Tangu uhuru?
Bunge letu linaanza vikao vyake leo asubuhi. Naomba wadau tupeana habari na kujadili hoja mbali mbali zitakazo tolea.
............Mgogoro ulikuwa kati ya Zito na waziri Ghasia..........
madai ni YA MSINGI lakini ZITTO amepoteza imani na watanzania kwa sasa!
May be Geoff Lakini afanye lipi kurudisha imani tuliyokuwa nayo????
Katika Bajeti nzima ni 29% tu ndiyo kwa maendeleo, ni pesa kidogo sana hasa ukilinganisha ukubwa wa nchi, idadi ya watu,umasikini uliopo, nishati na huduma za serikali. Asilimia 29 ni kama $2 bilioni. Katika bajeti nzima ina maana Bilioni $5.3 zinaenda katika kununua mashangingi, safari za nje, mafuta ya mashangingi, mishahara hewa, kununua viyoyozi vya wakubwa, marupurupu ya mawaziri 60 wasiojua kazi, semina na warsha.
Nataka kusema ule msemo wa NN lakini nitakuwa ninaiba hatimiliki.....