Kutoka Arusha: wabunge wa CHADEMA ndio wanapelekwa mahakamani

Dec 11, 2010
3,321
6,328
Wakuu.

Mtakumbuka kuwa jana wabunge wa chadema pamoja na waombolezaji wengine zaidi ya 70 walikamatwa na jeshi la Polisi kwa kile kilichoitwa kukusanyika bila kibali walipo kuwa uwanja wa SOWETO kwa ajili ya kutaka kuaga miili ya wahanga wa mabomu.

Wabunge hao wa CHADEMA ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.

Ni Tundu lissu (Singida Mashariki), mustafa Akonay (Mbulu), Mbunge wa Mpanda ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara, Mzee Said Amour Arfi pamoja na mbunge wa viti maalum Joyce Mukya wa Arusha.

Yupo pia afisa habari wa Chadema bwana Tumaini Makene.

• Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali

• Zaidi ya waombolezaji 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.

» Tutaendelea kujuzana yanayojiri.

• Polisi wameamua kuto kuwapeleka mahakamani na sasa inaonekana hakuna kesi ya kujibu, dhamana itatoka kituoni (polisi).

• Wabunge wote na wanachama na mashabiki wengine wameachiwa baada ya Polisi kuona kuwa hakuna kesi yoyote ya kujibu, hivyo hawakupelekwa kabisa mahakamani japo walipandishwa kwenye karandinga.

Makene atakuja kueleza vizuri kilichoko nyuma ya pazia punde.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Una taarifa na mashtaka gani wanapelekwa nayo? Chagonja yuko huko. ni mtu wa kutumia nguvu zaidi kuliko kichwa, no doubt ni shinikizo lake tu
 
Wabunge wa chadema ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.

Ni Tundu lissu, mustafa Akonay, na Said Arfi

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

Serikali hii haiana kazi zingine? Sasa hao wanakosa gani?
Kwa nini wasisumbuke na wahujumu uchumi wa nchi hii??
 
Poleni sana makamanda wa ukweli ili uweze kuinuliwa na mungu lazima upitie majaribu ukombozi unakuja soon na mwisho atakuwa wa kwanza.
 
Serikali hii haiana kazi zingine? Sasa hao wanakosa gani?
Kwa nini wasisumbuke na wahujumu uchumi wa nchi hii??
Kosalao kubwa ni kutotii amri ya jeshiletu tukufu la police. Kwahiyo wacha wakanyee debe.
 
Hakuna hata mtuhumiwa yeyote wa mlipuko soweto amefikishwa mahakamani? Magamba aibu hawana! mnawapeleka waombolezaji mahakamani ili maiti mzike ninyi? shame on you!
 
Wabunge wa chadema ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.

Ni Tundu lissu, mustafa Akonay, na Said Arfi

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
Aisee babangu, unataka uniambie mpaka sasa Mbowe na Lema hayaja kamatwa?
 
Hivi hii serikali inajielewa lakini? Mbona inatumia nguvu nyingi kupambana na wapinzani kuliko inavyopambana na ufisadi,rushwa na ujangili mambo yanayosabisha raia wanakuwa masikini? Kwa mwendo huu naamini tukiipa CCM miaka 10 mingine kuongoza zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania tutakuwa tunavaa nguo zenye viraka,wastani wa umri wa kuishi waweza kushuka na kufikia miaka 30 na miundo mbinu yote itakuwa hoi bin taabani. Kwa kuwa tuu serikali inadhani wajibu wake ni kupambana na upinzani.
 
Isije ikawa ni mkakakati wa kuhamisha attention ya wana Arusha toka kwenye mabomu,msiba na mazishi na kuihamishia mahakamani.
 
...Kwa kweli michezo ya sarakasi inayofanywa na jeshi la polisi TZ inachekesha... naomba tu wapige hesabu ya gharama watakazotumia katika sakata zima na watanzania wajue ni kiasi gani cha pesa za walala hoi zinapotea bila sababu ya maana... Polisi hawatumii busara hata kidogo katika mambo mengi....
 
Una taarifa na mashtaka gani wanapelekwa nayo? Chagonja yuko huko. ni mtu wa kutumia nguvu zaidi kuliko kichwa, no doubt ni shinikizo lake tu

Hata jana alivyokuwa anaongea unaona kabisa anatumia nguvu badala ya hekima.hili ni tatizo kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…