Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,328
Wakuu.
Mtakumbuka kuwa jana wabunge wa chadema pamoja na waombolezaji wengine zaidi ya 70 walikamatwa na jeshi la Polisi kwa kile kilichoitwa kukusanyika bila kibali walipo kuwa uwanja wa SOWETO kwa ajili ya kutaka kuaga miili ya wahanga wa mabomu.
Wabunge hao wa CHADEMA ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.
Ni Tundu lissu (Singida Mashariki), mustafa Akonay (Mbulu), Mbunge wa Mpanda ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara, Mzee Said Amour Arfi pamoja na mbunge wa viti maalum Joyce Mukya wa Arusha.
Yupo pia afisa habari wa Chadema bwana Tumaini Makene.
Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali
Zaidi ya waombolezaji 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.
» Tutaendelea kujuzana yanayojiri.
Polisi wameamua kuto kuwapeleka mahakamani na sasa inaonekana hakuna kesi ya kujibu, dhamana itatoka kituoni (polisi).
Wabunge wote na wanachama na mashabiki wengine wameachiwa baada ya Polisi kuona kuwa hakuna kesi yoyote ya kujibu, hivyo hawakupelekwa kabisa mahakamani japo walipandishwa kwenye karandinga.
Makene atakuja kueleza vizuri kilichoko nyuma ya pazia punde.
Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

Nipo hapa Kituo cha polisi Kati Arusha,nawaona Wabunge wa CDM na baadhi ya Kina mama wamepandishwa kwenye Karandinga saa 6:24.
Wa kwanza kupanda ni Mh Tundu Lisu akafuatiwa na Said Arfi na Mustafa Akunay.
Wamekalishwa chini kwenye Karandinga ni zaidi ya dk 30 sasa gari lipo tu halijaondoka na hawajapandishwa watu wengine isipokua Wabunge hao watatu diwani wa daraja mbili mgombea udiwani wa Kimandolu Mch Ngowi na baadhi ya kina mama kama sita hivi.
Nimejaribu kuwahoji baadhi ya watu na polisi hapa kwamba ni kwanini hawajapelekwa mahakamani hadi sasa wanadai kuwa wanacheleweshwa makusudi ili wakifikishwa Mahakamani Wanyimwe dhamana na waende Magereza.
Nitaendelea kuwajulisha kinachoendelea.