Na swali hili akiwauliza waliotahiriwa? Kila kizazi kinakuja na mambo ya kuwakera wazazi wao. Kuanzia mavazi, muziki ili mradi kumnyima raha dingi. Kama alivyosema Lunanilo,dengilizi ilikuwa vazi la kihuni, michinjo iliwaudhi sana wazazi, bichkoma n.k. Usiangalie alichovaa bali angalia tabia yake. Vinginevyo unagombana na ukuta. Mzee Morgan Freeman, Spike Lee, Michael Jordan, 50 cent wote wametoga na hawa ndiyo role models wa vijana wetu. Tuombee tu wapite katika umri huo mgumu wa u-tineja bila madhara yeyote na wao watakujashangaa vioja vya watoto wao!
Kibunango yuko sahihi kabisa. Huku kukemea uvaaji ni morals tulizoiga kutoka kwa hao waliotutawala na kutuletea dini. Wanaume kwa wanawake walijiremba, walitembea nusu uchi bila ya matatizo yeyote kabla ya kuja hao wageni. Leo tunapandisha kwa sababu kijana katoga sikio!
Amandla......