Kutodurusu baada ya mwanafunzi kufeli mtihani kidato cha pili ni siri iliyojificha kuhusu elimu bure?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kwakweli hili suala linatia ukakasi mkubwa sana, hii ni aibu kubwa kwa taifa, sasa lazima tuamini kwamba serikali yetu haina nia njema kabisa na kulibadili taifa hili, huu sio uungwana hata kidogo. Tunajali maslahi yetu ya kisiasa lakini tunasahau wajibu wetu kwenye jamii tunayoihudumia.

Sitaki kuamini kabisa kua maamuzi haya ni kuogopa kumgharamia huyu mwanafunzi atakayerudia mwaka baada ya kufanya vibaya kidato cha pili kabla ya kuingia kidato cha tatu, ni kukwepa gharama za usahihishaji mitihani pamoja na mambo mengine awapo shule?Hivi ni kweli ndio tumeamua kuruhusu aina hii ya utoaji elimu kwenye taifa letu? Wote tuliopitia sekondari hatujui umuhimu wa mitihani wa kidato cha pili kweli? Kwanini tu nataka kuangamiza watoto wetu kifikra kiasi hili? Alaumiwe nani hapa kama sio serikali yetu hii?


Prof Ndalichako, na wewe huoni umuhimu wa kidato cha pili kweli? Katika watendaji ambao mwanzo tuliamini kua wewe ni chanzo na chachu kubwa kwenye mabadiliko ya sekta ya elimu nchini wewe ulikua ni mojawapo na sasa ni kinyume kabisa.Ni wapi tunalipeleka taifa?

Kwa wengine ambao tumefanya kazi hii ya kufundisha kwa muda mrefu, ni kwamba umuhimu wa mitihani ya kidato cha pili ni kupima uwezo wa mwanafunzi ndani ya miaka miwili tangu aingie kidato cha kwanza, hapa mwanafunzi hupata fursa ya kujielewa na kujitathmini ni vipi amepata uwezo wa kwenda kukabiliana na kidato cha tatu na nne. Nakumbuka enzi zangu wakati nilipofanya mtihani wa wa taifa kidato cha pili ambapo matokeo yalikua yakitolewa na kanda yetu ya kaskazini, nilipopata wastani wa daraja A kwenye mtihani huo wa taifa nilijiamini sana na kuondoa hofu kua hata kidato cha nne lazima performance iwe nzuri. Hii ilinipa moyo sana nikasoma kwa bidii zaidi iliyonipelekea kufanya vizuri zaidi kidato cha nne, kwa wale ambao walinusurika kurudia mwaka walisoma kwa bidii wakiwa kidato cha tatu na kuwapelekea hata kujiamini hadi kufaulu vizuri kidato cha nne.

Siasa inatuangamizia taifa na hakuna anayejali, watu wanataka watimize ahadi zao walizoahidi wakati wa kampeni kuongeza idadi ya madarasa na madawati bila kuangalia umuhimu na ubora wa elimu inayotolewa. Lazima tuambizane ukweli, huku ni kubana matumizi na kuangamizana kwenye uwezo wa kufikiri.

Mungu alinusuru tu taifa letu kwa uwezo wake.Kama mbunge ni darasa la saba,diwani la saba, mwenyekiti wa kijiji na kitongoji ni darasa la saba, tutegemee uchumi wa viwanda lini? Mbunge wa darasa la saba anaelewa mini kuhusu mtihani wa kidato cha pili? Atachangia kitu gani bungeni jamani? Atapeleka hoja gani zaidi ya kupiga meza tuu?


Hili halikubaliki!! Lazima tubadilike!!
 
Una hoja nzuri, nje ya mambo ya kisiasa na siasa zetu uchwara za Kitanzania. Utaungwa mkono kisiasa na kupingwa kisiasa, japo hoja ni yenye mantiki.
 
Mzee we fanya yako,
Hakuna namna kama mwl fundisha tu.
Ulimwamini Joyce ambaye hapo NECTA aliharibu hadi akaondoka?
Leo uje umuamini kwenye siasa?
 
Back
Top Bottom