Kutoa shilingi na Kushikiria mshahara wa Waziri

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Ndugu zangu wenye fikra pevu!!!

Ninaomba kufafanuliwa maana ya dhana hizi zinazotumika katika vikao vya bunge letu. Dhana hizo ni KUTOA SHILINGI na pia KUSHIKIRIA MSHAHARA WA WAZIRI.

Nini maana ya dhana hizi mbili?
 
sijakuelewa kabisa. Ngoja niwasikie wadau wengne then i wil be back.
 
Yaani unakuta mbunge anachangia hoja fulani, kisha anasema kama waziri asipofanya A,B,C nitashikilia mshahara wake.
 
Matumizi yako ua L na R yanatuchanganya!
Hueleweki.

Mkuu mbona jamaa anaeleweka. anaulizia hii dhana ya kutoa shillingi ama kushikilia mshahara wa waziri hasa wakati wabunge wakiwa wamekaa kama kamati ya matumizi kupitia kifungu kwa kifungu makadirio ya mapato na matumizi ya wizara husika. Hata mimi nimekuwa nikisikia masuala ya kutoa shilling ama kushikilia mshahara wa waziri hasa inapofika wakati wa kupitisha kifungu ambacho kina mshahara wa waziri. Huwa sielewi kama ni shillingi moja ama hiyo shillingi inawakilisha kitu kingine. Na kama wakikubaliana kutoa hiyo shillingi nini kinaweza kutokea: kwenye wizara husika ama bunge kwa ujumla? Nadhani humu kuna wataalamu watatusaidia.
 
Mmmm,rejao ameeleweka bhanaa,hizi kauli hutolewa sana kwenye vikao vya bunge la BAJETI NA HASA WAKAT WA KUCHANGIA MIJADALA JUU YA WIZARA FULAN
Matumizi yako ua L na R yanatuchanganya!
Hueleweki.
 
Swali zuri sana hilo ndugu mimi mwenyewe huwa najiuliza sana ila nilikuwa nafikiri kuondoa shilingi ni kupinga kuunga mkono kifungu fulani cha bajeti sijui kama nikom sahihi au la. Naomba wenye idea juu ya manano haya watujuze.
 
Ndugu zangu wenye fikra pevu!!! Ninaomba kufafanuliwa maana ya dhana hizi zinazotumika katika vikao vya bunge letu. Dhana hizo ni KUTOA SHILINGI na pia KUSHIKIRIA MSHAHARA WA WAZIRI. Nini maana ya dhana hizi mbili?

mimi naona is too personal, kwa mfano kutoa shilingi kwenye msharaha wa waziri hii ni kuwacheka wananchi, kuwabeza na kutudhara, shilingi ina madhara gani kwenye mshahara wa mtu? hata kama analipwa Tsh 30,000 ukisoa shilingi hakuna anachojisikia, kwa sababu haina thamani anyway.

hii ingekuwa ni hadhabu kubwa kwa mataifa yenye uwajipikaji kama JAPAN na kwingineko ambako wato ujiwajipisha kulingana na makosa au kushinda ku deliver expectation , kwa mfano waziri wa nishati kwa nchi kama JAPAN sio tu angejiuzuru lakini pia kungekuwa na uwezekana wa kujinyonga kutokana fedhea ya nchi kuwa na GIZA TOTORO

kwa TANZANIA hakuna haja ya kutoa shilingi ila mambo ambayo hayako sawa yangekua yanarudishwa na kurekebisha kisha kurudishwa kwenye mjadara, kutoa shillingi si sawa na sanaa za kiana majuto, hii ni nchi jamani kuna mambo mengi yametufikisha hapa kwenye maisha haya.
hakuna mbunge ninaye mdharahu kama anayetoa shilingi kwenye bajeti au mshahara wa waziri.
nasikitika kusema hata Mkono wa kwetu ndio kazi yake hiyo kutoa shilingi sasa nini maana ya kuwa na wasomi nchini?

narudia tena tungekuwa JAPAN ni sawa lakini kwa TANZANIA ni no i mean BIG NO
 
Nimekuwa nafuatilia bunge letu la budget,si kwa lengo la kujifunza namna ya kuzungumza manake siku hizi huku mitaani ukiwa unaongea na watu wengine lazima watakuarifu kuwa hawataki utumie lugha ya kibunge.

Bunge linapokaa kama kamati ili kupitisha kifungu kwa kifungu,nimekuwa nawasikia wabunge wakisema anaomba maelezo ya kifungu fulani na majibu yasipomridhisha ''atatoa shilingi'',hiyo kutoa shilingi ndo maana yake nini?''

Nilimuona mh. Mnyika juzi akitoa hoja kama hiyo na jana Esther BulayA lakini sijaelewa hasa tafsiri yake na impacts zake ni nini?
 
naomba mwenye kujua anijuze, hii ni kauli inayotumiwa na wabunge wakiwa wanachangia hoja bungeni: sijui ina maana gani?
 
Kauli hiyo hutumika wakati bunge linapokaa kama kamati na kupitisha bajeti ya wizara husika. Wakati wa upitishwaji wa bajeti yanapofikia mabo ya kisera(policies) ndipo kauli hiyo hutumika pale ambapo mbunge mmoja anapokuwa hakubaliani na jambo fulani la kisera kwenye bajeti ya wizara husika.

Endapo akisema kuwa anatoa shilingi inamaanisha anapinga sera iliyopo na ku-introduce nyingine na atatakiwa aungwe mkon na wabunge wengine, kisha sera(hoja) aliyo introduce itajadiliwa kwa muda na baadae kuulizwa wabunge wanaokubaliana na hoja kwa kusema ndiyooooooooo au siyooooooo
 
Now, why shilling? itumike hapo? asili ya neno shilingi ni nini kwenye mshahara wa waziri?
 
naomba mwenye kujua anijuze, hii ni kauli inayotumiwa na wabunge wakiwa wanachangia hoja bungeni: sijui ina maana gani?

Now, why shilling? itumike hapo? asili ya neno shilingi ni nini kwenye mshahara wa waziri?

Ni propaganda ya kuwaonyesha wananchi wanaosikiliza Bunge ili wadhani kuwa Bunge ni kali sana kiasi kwamba Waziri akifanya mchezo linamkata mshahara.
 
Now, why shilling? itumike hapo? asili ya neno shilingi ni nini kwenye mshahara wa waziri?

Ninavyojua wanaondoa shilingi kwenye hiyo bajeti ya Waziri na sio Mshahara wa Waziri...
Kwahiyo kama bajeti ya wizara ya ujenzi waziri aliomba sh. 100.00 na Mbunge kutoa shilingi bajeti itakuwa sh. 99.00 kwahiyo haita tosha kutumika kwa Mwaka huo wa BAJETI sababu imepungukiwa shilingi

Kwahiyo Waziri atajaribu kuitetea - akishindwa wataunda bajeti mpya - Katibu Mkuu wa Wizara ndie Mhusika Mkuu

Na kama ikiendela na bila shilingi kurudishwa --- Ina Maana Rais anaweza kulivunja Baraza la Mawaziri au BUNGE
 
Ni propaganda ya kuwaonyesha wananchi wanaosikiliza Bunge ili wadhani kuwa Bunge ni kali sana kiasi kwamba Waziri akifanya mchezo linamkata mshahara.
Kumbe unajuwa kwamba kuna Propaganda!! sasa unavyojitiaga uchizi maana yake nini?
 
Back
Top Bottom