Kutoa Mimba ni dhambi kuu

Kutoa Mimba ni dhambi kuu

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,446
Usikubali kutoa mimba kwani ni dhambi,ukitoa mimba yule mtoto atatoa ushahidi siku ya hukumu na hakika hutapona hukumu ya Mungu.

Nakushauri kama umewahi ktuoa mimba tubu haraka sana kwani hakika utahukumiwa,kuna wenye ndoa utakuta mwanaume anamsindikiza mke wake kutoa mimba ni dhambi kubwa

Usipotubu na kuacha tegemea hukumu!
 
Tena kama huna mtoto halafu unaitoa utajuta sana!!! huitaki kwanini unairuhusu ikuingie??
 
Kutoa mimba ni dhambi kubwa sana lakini siyo vibaya.
 
Among all sins, dont abort please. Nasema usitoe mimba, Mungu atakusaidia kulea hiyo mimba
 
Usifanye mchezo kubeba mimba usipotakiwa kubeba sio jambo rahisi hata kidogo.tena tubu naamini Mungu anasamehe kama bado unakumbuka ni mahubiri ya shetani kukurudisha nyuma.

Mimi nikibeba mimba ya mtoto wangu wa kwanza sikua nimeolewa na nilikua nimemaliza form six hata majibu bado.sikua nimewahi lala na mtu ndio mara ya kwanza.

sikujua imekuaje mpaka amenifanya maana nilikua namuogopa kidogo kutokana kwamba alikua giant na mimi nilikua na mwili mdogo.aliniita kwa kaka yake nikaenda sijui ilikuaje nilikua nshavuliwa kila kitu na yupo katika harakati za kuniingia nilibishabisha ila shetani alinizid nguvu nikakubali.

balaa lilianzia hapo.nilipata mimba nikasema nitaitunza maneno niliombiwa nyumbani bado nusu nijiue mpenzi aliikataa kabisa na pale kaka alihama nili attempt kujiua nikaogopa nikapiga moyo konde

ile mimba ilifika miez sita kwamisukosuko atlast ilitoka hakuna
kitu kiliniuma kama hicho kwani nilishaaibika kwanini ilitoka ,jamani kama sio roho ngum mimba unatoa.suala sio kujiachia ili upate hata uwe responsible kiasi gani bahati mbaya zipo
 
Ni amri ya ngapi inakataza kutoa mimba? Mbona mnapenda kufanya maisha kuwa magumu kwa kujitengenezea shambi zenu?
Acheni kutisha watu bana.
 
....waendelee kuzini na kufanya uasherati as long hawapati mimba....au sio...
...tuanze na mzizi wa tatizo...vingine vitafuata...
 
Nakuunga mkono dada Rosmari. Kutoa mimba ni dhabi kubwa sana. Nigpenda kuwashirikisha Wana Jamii kuhusu ukubwa wa dhamb hii, kupitia sehemu ndogo tu ya kitabu ninachoendelea kukiandika juu ya dhambi hii! Ni ushuhuda halisi.. unaoonyesha kiini cha ukubwa wa dhambi hii ya kutoa mimba... kweli inatisha, inatisha!!
 
wanawake ndo wana nafasi kubwa ya kuzuia mimba..kusema wanaume ndo wanastahili kubeba hiyo dhambi unakosea


Nakukaribisha usome sehemu hii ndogo ya ushuhuda unaohusu ukubwa wa dhambi hii ya kutoa Mimba.

Nimejaribu kutoa sehemu fupi fupi kwa vile ni chapta ndefu ya kitabu ninachondelea kukiandika:



KUTOA MIMBANDIYO DHAMBIKUBWA NA YA KUTISHA

ZAIDIKULIKODHAMBI ZOTE ZA MAUTI​
Kila mara damu ya mtoto mchanga inapomwagika katika tendo lautoaji minba, damu hiyo hugeuka na kuwa sadaka ya kuteketeza kwa shetani,ambayo humpatia nguvu zaidi shetani dhidi ya wanadamu wenyewe. Hata kama kwauelewa wa kibinadamu, tunaona kuwa mtoto huyu anayetolewabadohajaumbika ubongo, macho, miguuau bado hajaumbika mwili kwa ujumla, lakini tayari ameshakua na rohoiliyo kubwa sawa roho za watu wengine.

Wakati mtoto huyu anapotolewa katika tumbo la mama, roho yake humliliaMungu kwa sauti ya kutisha! Lakini kinyume chake ni kwamba,vilio vya watoto hawa wanapotolewa mimba,huwa furaha na ushindi kwa mashetani wa jehanamu/ kuzimu. Furaha hiyo yamashetani kuhusu vifo vya vichanga vinavyotolewa mimba, tunaweza kuilinganishakama vile ambavyo mashabiki wa mpira wa miguu, wanavyofurahia na kushangiliaushindi wa fainali ya Kombe la Dunia wakiwa uwanjani!

Fikirieni jambo hili ilimuweze kuona picha hiyo ya watu wanavyopigwa na mzuka wa kushangilia ushindi wakombe la dunia kwa nchi yao!
Ni nderemo,vifijo na shamrashamra zisizoweza kuelezeka! Basi ndivyo hivyo hivyo ambaposhetani na pepo wake, wanavyoshangilia tendo la kutoa mimba! Wanavyoshangiliamauaji ya watoto hao wadogo wasio na hatia! Kwa sababu shetani hupokea tendohilo kama sadaka ya kuteketeza!

Yaani mama, kwa kwa dhamira mwenyewe ameamuakumtolea shetani sadaka ya kuteketeza ya mtoto au watoto wake mwenyewe! Huu niushindi na furaha kubwa sana kwa shetani!........
sababu ya pili ni kule kuua watoto wachanga walio tumboni,ambao hawana hila,ambao hawawezikujitetea, ambao damu zao huitajika sana na shetani ili kuwa sadaka yakujipatia nguvu zaidi dhidi ya wanadamu wenyewe ambao walikombolewa kwa Sadakaya Kristo msalabani.

Shetani huamurumauji hayo toka huko chini aliko…….
Mtoto mchanga ni kama kondoo asiye na hatia wala mawaa! Jemnajua ni nani huyo kondoo asiye na hatia wala mawaa? Ni Yesu Kristo mwenyewe!Kwa hiyo mtoto mchangani mfano wa Yesu,ambaye ndiye kondoo asiye na mawaa.Sasainapotokea kuwa mama huyo, ndiye anayewaua watoto wake mwenyewe, mama huyohuingia moja kwa moja katika uhusiano na nguvu za giza zinazotoka chini zaidikuzimuni, pasipo yeye mwenyewe kujijua.

Mama huyo mtoa mimba anapokuwa bado haikatika dunia hii anaona
mambo yote yakosawa, lakini siku ya kufa kwake ndipoatakapotoa hesabu ya uovu huumbele ya Mungu, kama ilivyokuwa katika kesi hii yangu ninayosimulia…….
Katika kutoa mimba mama hujitoa na kujidhamini kwa shetanikwa kuua mtoto wake mwenyewe, na hivyo kuruhusu nguvu za giza na mapepo watokewengi zaidi kuzimuni ili kujakuwatawalawanadamu na kuwafanya wawe watumwa wa dhambi za kila namna tunazozishuhudiakatika dunia hii.

Kitendo cha kutoa mimba ni sawa na kuivunja mihuri,vifungo...!
Mihuri ambao Mungu aliifungaili kuzuia maovu kutoka nje ya kuzimu kuja duniani. Kwa hiyo kilamimba inayotolewa inafungua milango hiyo. NaMilango hiyo inapokuwa wazi humwaga zaidi na zaidi duniani mabuu wa kutisha,ambao ndiyo mapepo wa kila namna!Mapepohao wanatoka kuzimu, kuwafuata na kuwapatiliza watu.Pepo hawa wanapokuwa duniani huwafanya watukuwa watumwa wa kila namna ya maovu tunayoona na kusikia katikadunia……
Mnajua nini kilitokea wakatidaktari alipokuwa akitoa mimba yangu?

Bwana alinifanya nione wakati daktari aliyekuwa na mkasi na
koleo ya kutolea mimba yangu, jinsialivyokuwa akimkamata mtoto wangu tumboni nakumkata vipande vipande!Mtoto huyoambaye kwa macho na ufahamu wakibinadamu alionekana kana kwamba hajaumbika bado vizuri,lakini Bwana alinionesha kuwa roho ya mtotoyule ilishakuwa kubwa sawa na roho za watu wengine! Kwa hiyo wakati daktarialipokuwa akimkatakata mtoto yule,rohoyake ililia kwa nguvu sana mbele ya Mungu baba!

Ndugu zangu ninapenda kuwaaambia kile nilichoonyeshwa na Yesu kuwa,dakika au tuseme sekunde ile ambapo chembechembe zalishi ya mwanamke ambayohuitwa "yai" na chembechembe zalishi ya mwanamume ambayo huitwa"spermatozuni" vinapoungana kupitia tendo la ndoa/ kujamiiana, rohoya kiumbe huyo tayari imeshafanyika kikamilifu kabisa na roho hiyo huwa kubwasawa na roho za watu wengine wote!

Roho hiyo pia huwa na haki kamili mbele yaMungu sawa na roho za watu wengine wote. Kwa hiyo hata kama
mimba hiyo inatolewa dakika moja au sekundimoja au siku moja au mwezi mmoja baada ya kutungwa,ni lazima tufahamu kwamba tunamuua mtotomwenye roho kubwa na iliyoumbwa kikamilifu sawa na roho za watu wengine!Tofauti iliyopo ni kwamba roho hiyo ambayo huumbwa na Mungu, haikui kamaunavyokua mwili. Roho hufuata umbo jinsi unavyokua tangu utotoni hadi uzeeni.

Na roho hiyo hufanywa na Mungu katika muda uleule ambapo mbegu ya kiume na yaila kike vinapoungana…...
…… kwamba mara moja baada yachembechembe ya kike na ya kiume kuungana ndani ya mwili wa mama kupitiatendo la ndoa, hutokea cheche za mwanga mzuri ajabu. Mwanga huo huonekana mkalikama ule wa jua. Mwanga niliouona ulitoka katika Mwanga wa Mungu Baba. Papohapo ulipotokea mwanga ule, ndipo roho ya mtoto huyo huumbwa na Mungu na huwatayari roho kamilifu na iliyokomaa, ambayo huchukuwasura na mfano wa Mungu Mwenyewe!

Kiumbe
huyo ambaye kwa macho na akili ya kibinadamu tunamwona kama bado buu auzaigoti, au kilenge, ukweli ni kwambatayari amezama katika Roho Mtakatifu, anayetoka katika Mungu mwenyewe…..
…… Wanapomuua mtoto huyo katika tendo la kutoa mimba, roho yamtoto huyo hulia hadimbingu yoteinatetemeka! Bahati mbaya, hapa dunianihatuwezikuona au kusikiakitendo hiki!
 
Nadhani kwa tuliooa nivyema kumuuliza mkeo kama aliwahi kutoa mimba katika maisha yake. Na ukishajua usimuache Bali muongoze atubu kwani hii kitu mtu asipotubu huleta balaa katika familia na huleta madhara ambayo yanaweza sababisha hata ndoa kuvunjika. Mambo ya roho ni magumu sana wakati mwingine usipo ya jua.
 
Back
Top Bottom