Kutimiza Ahadi ni Rushwa! - Dr. Hosea

Tangu tumepata uhuru, kwa awamu zote 3, Tanzania imewahi kushughulia kesi kubwa 2 tuu za rushwa!, awamu hii ya Nne, imepeleka kesi kubwa 18 za Rushwa.

Absolom Kibanda kauliza kuhusu kauli ya rais kuhalalisha takrima - Dr. Hosea amemtetea mkuu wa nchi kuwa pale ametolea mfano tuu, na kukiri kuwa suala la takrima ni challenge.

Amemfagilia Kibanda na wanahabari wote wakiamua kulivalia njuga suala la rushwa kwenye magazeti yao, na kusisitiza "wewe Kibanda, mimi nakuaminia sana kwenye gazeti lako, ukiamua unaweza!".

mmh.. sidhani kama huyo anasema ukweli kuhusu hiyo idadi; hivi walimuuliza hizo kesi mbili ni zipi... maana wengine tunakumbuka mambo ya kina Simbaulanga...
 
Mzee Mwanakijiji,

Hakuna sheria ambayo iko kamili, sasa je wewe unaona ilikuwa bora hii sheria kutokuwepo?

Pamoja na mapungufu yake mimi bado naamini ni bora hii sheria imeanza kufanya kazi na kama PCCB watatimiza wajibu wao basi huenda kukawa na mafanikio hata kama haitakuwa asilimia 100.

Hata sasa kuna sehemu ambako waliokuwa wanajiandaa kumwaga mapesa sasa wamekaa kimya baada ya kuona sheria inawabana. Hilo pekee tayari ni mafanikio.

tatizo la sheria hii ni kubwa mno kuliko ubora wake; kumwaga pesa kwenye uchaguzi siyo kosa na ndio maana naona tatizo la sheriahii. NI sawa na kuwaambia watu kwenye uchaguzi msizungumze sana mzungumze kidogo. Ni sheria ambayo imekuja kwa ajili ya kufanya geresha tu. Nilishachambua yaliyomo ndani yake na mapungufu yake na hadi sasa wao wenyewe (waliopitisha kwa mbwembwe) wamekubali inamapungufu.

Sasa kuna mapungufu ya kawaida ya sheria (kama ulivyosema kuwa si kamilifu) lakini kuna mapungufu ambayo ni makubwa sana kiasi kwamba kunarender the whole law kuwa absurd.
 
Dr. Hosea amefafanua kuwa sio kila msaada ni rushwa, msaada ambao ni rushwa, unatokana na dhamira. Kama wewe ni tajiri, hauna dhamira ya kujishughulisha na siasa, ukatao miasaada ya kimaendeleo kwa jamii fulani kwa lengo na dhima ya kuleta maendeleo au kusaidia tuu kama wahanga wa mafuriko, misaada hiyo siyo rushwa, ila kama misaada hiyo itatolewa na taasisi fulani kwenye eneo fulani bila sababu ya msingi ya msadaa huo, itageuka kuwa rushwa kwa lengo la kumpigia chapuo kiongozi fulani, au chama fulani.

Mathalani benki fulani ikipeleka misaada ya mafuriko Kilosa, kwenye jimbo la Mkulo, huu utakuwa ni msaada halali na sio rushwa, ila benki hiyo hiyo ikipeleka msaada Urambo bila sababu ya msingi, ni kumpigia chapuo fulani au chama fulani.

Wanabodi, the deviding line between rushwa na sio rushwa is very thin!.


That is always the case. Na ukianza kuongelea dhamira...hii inakuwa ngumu ku-prove. Maana hii wanaita the mental element. How do u prove the thoughts of one in this case? Inakuwa especially ngumu hapa maana action ni kutoa msaada! What kind of things will they look for to prove the rushwa intent?
 
Japo sikusikiliza maongezi yote kati ya Cloud FM na Dr. Hosea lakini pamoja na mambo mengine alisema hivi kuhusu RUSHWA. Dhamira na timing ni muhimu katika kueleza kwamba hii ni rushwa ama sio. Unaweza kutoa msaada huohuo ukawa rushwa mahali fulani na sio rushwa mahali pengine. Kwa hiyo ukitimiza ahadi wakati huu kwa kufanya jambo linalowasaidia watu wengi kama KUJENGA SHULE, DISPENSARI, KUCHIMBA KISIMA, KUJENGA BARABARA na kadhalika sio vibaya(sio rushwa) . Lakini ukitoa kitu kinachomsaidia mtu moja moja au kikundi kidogo katika jamii hiyo ni rushwa, mfano KUTOA KANGA,BAISIKELI, UNGA, CHUMVI, PLAU, BAHASHA na kadhalika hiyo ni rushwa.
 
Abdulhalim, Asante kwa maoni yako, nayaheshimu. ila pia sio vibaya nikukuelmu kidogo tuu kuhusu hiyi post #21.
Thread ilihusu reportage ya nini kinatokea, wapi na saa ngapi, ikijumuisha nani kasema nini. Usually kwenye reportage unatakiwa kuripoti umesikiani nini, nani kasema nini etc.

Baada ya repotage inafuatia analysis kuhusu hicho kilichoripotiwa au kilichosemwa wahat does it mean, na hizi ndizo fani za watu wake kama kina Mzee Mwanakijiji, mara baada ya sheria hii kusainiwa kwa mbwembwe, alishuka na nondo za kufa mtu kuhusu madhaifu ya sheria hii na kuiita ni sheria mbaya.

Baada ya analysis ndipo unaweza kutoa upinion. hiyo post 21, ni pesonal opinion yangu ndio maana imeanza "kwa maoni yangu", kwa vile haya ni maoni yangu, sio facts ni mtazamo tuu, unao uhuru wa kuyapinga, kutokukubaliana nayo, ikiwemo maoni hayo kuwa na thamani, woth au hayana thamani, wothless, ila bia ni kwa afya ya mjadala unapokuwa negative, unauhuru wa kuchambua madhaifu, ama kuyaacha ama kukoment chochote, japo afya nzuri ni kubishana kwa hoja, usiishie kusema ni wothless tuu na kuiacha hewani, zama ndani japo kidogo. Mathalan ukiibua hoja wewe Abudlhalim, mimi nikasema hoja yako ni utumbo utumbo au mbofu mbofu bila kujenga hoja ya msingi wa mtazamo wangu, inaweza ikatafsiriwa kama chuki tuu.

Hata hivyo bado naheshimu maoni yako hata kama ni matupu bila nyama, ni maoni na nitayazingatia.

Pasco ni hivi,

Huwezi ku-characterize utendaji wa mtu kwa kupitia maneno yake, ndio wahenga walisema 'matendo huongea kwa sauti zaidi kuliko maneno'. Hiyo mineno ya kumpamba Hosea ulioweka imenitia hasisa sana kwa sababu za kihistoria kuhusu ofisi yake kuhusiana na matendo ya upotevu wa pesa za umma unaohusishwa na maofisa wa serikali pamoja chama twawala. Hapa sijaona lolote la maana ambalo unaeza kusema ni end-product ya utendaji wake na taasisi yake. Hizi ahadi kuhusu uchaguzi blah blah zinaeza tolewa na yeyote. Umahiri wa kupiga porojo na propaganda hauna tija kwa taifa na si kipimo cha utendaji uliotukuka.
 
Back
Top Bottom