Kutimiza Ahadi ni Rushwa! - Dr. Hosea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutimiza Ahadi ni Rushwa! - Dr. Hosea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 28, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, kumbe hata kutimiza ahadi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu pia ni Rushwa, sambamba na ugawaji wa pikipiki, baiskeli, vifaa vya michezo etc kuelekea Uchaguzi Mkuu zote ni rushwa, ikimaanisha serikali ya CCM na vinara wake ndio makuwadi wakuu wa rushwa!.

  Hayo yemethibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa PCCB, Dr. Edward Hosea, ambaye yuko live kwenye kipindi cha Power Breakfasr kinachorushwa na Clouds FM.

  Clouds are doing really good!. Hii ni mara yangu ya kwanza kuwasikia wamemkaribisha mtu high profile ya status kama Mkurugenzi Mkuu wa PCCB.

  Endelea Kufuatilia.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Pasco.. soma ukosoaji wangu wa ile sheria ya Gharama za Uchaguzi na watu wakaniona miye sijui sheria, sijui tafrisi yangu ni wrong.. ati hamnazo.. .. niliposema ni sheria mbaya na mbovu sikuwa natania! Sheria yao ile hata baada ya kusainiwa kwa mbwembwe bado ni sheria mbovu..
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Je, Hosseah amefanya nini kwa wana CCM ambao wamekuwa wakigawa t-shirt na vitu vingine wakati wakielekea kwenye kura za maoni? Ngoja tutaona kama hayo anayoyasema ataweza kuyasimamia.

  Kwenye hatua za nominations within CCM watatoana makucha. Lakini ikishaingia kwenye kipindi cha kampeni, hiyo sheria itawekwa pembeni in favor of wenye nchi.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Mwendeshaji wa kipindi, Gerald Hando, alimchomekea Dr. Hosea, kumbe hata mkuu wa nchi namakamanda wake wanavyozunguka nchi mzima kutimiza ahadi, au kusisitiza kutimizwa kwa ahadi pia ni rushwa?

  Dr. Hosea akalikwepwa swali na kutoa ufafanuzi kuwa kama kutimiza ahadi kwa manufaa ya taifa, kama kuwapatia watu wote maji, umeme au huduma za jamii kwa mujibu wa ilani za vyama kitaifa, sio rushwa , kutimiza ahadi kwa rushwa, ni pale tuu waheshimiwa huko majimboni waliahidi hiki na hiki, halafu hawajatimiza mpaka mwaka wa uchaguzi, utimizaji huu ni rushwa!.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hosea hamnazo kabisa. Tangu kesi yake ya Richmond namuona anabwabwaja tu mambo asiyoyajua. Anadhalilisha udaktari wake na anamkosea Mungu sana kwa unafiki wake.

  Hajui kitu anasema na wala hajui kitu anafanya na madhala yake kwa taifa hili kwa wakati huu na wakati ujao.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Dr. Hosea anasisitiza, demokrasia ya kweli ni uchaguzi ulio huru na wa haki.

  Uwepo wa rushwa, au mazingira yoyote ya rushwa, yanabatilisha moja kwa moja uhuru wa uchaguzi na kupoteza haki ya wapiga kura.

  Ametoa onyo kwa wanasiasa, kujielimisha kwa bidii sana hii sheria mpya ya ghara za uchaguzi, na kusisitiza kuwa tayari wanayo listi ndefu ya viongozi wanaopita wakigawa pikipiki, baikeli, fulani hata kalenda tuu kwa lengo la ushawishi, hawa watakiona cha moto kabla hata ya uchaguzi wenyewe.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  tatizo ni hiyo sheria..
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Dr. Hosea amefafanua kuwa sio kila msaada ni rushwa, msaada ambao ni rushwa, unatokana na dhamira. Kama wewe ni tajiri, hauna dhamira ya kujishughulisha na siasa, ukatao miasaada ya kimaendeleo kwa jamii fulani kwa lengo na dhima ya kuleta maendeleo au kusaidia tuu kama wahanga wa mafuriko, misaada hiyo siyo rushwa, ila kama misaada hiyo itatolewa na taasisi fulani kwenye eneo fulani bila sababu ya msingi ya msadaa huo, itageuka kuwa rushwa kwa lengo la kumpigia chapuo kiongozi fulani, au chama fulani.

  Mathalani benki fulani ikipeleka misaada ya mafuriko Kilosa, kwenye jimbo la Mkulo, huu utakuwa ni msaada halali na sio rushwa, ila benki hiyo hiyo ikipeleka msaada Urambo bila sababu ya msingi, ni kumpigia chapuo fulani au chama fulani.

  Wanabodi, the deviding line between rushwa na sio rushwa is very thin!.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, natamani nikushukuru ili kukujulisha nilikusoma, browser yangu asubuhi hii, haina kitufe cha thanks,
  Thanks!.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Tangu tumepata uhuru, kwa awamu zote 3, Tanzania imewahi kushughulia kesi kubwa 2 tuu za rushwa!, awamu hii ya Nne, imepeleka kesi kubwa 18 za Rushwa.

  Absolom Kibanda kauliza kuhusu kauli ya rais kuhalalisha takrima - Dr. Hosea amemtetea mkuu wa nchi kuwa pale ametolea mfano tuu, na kukiri kuwa suala la takrima ni challenge.

  Amemfagilia Kibanda na wanahabari wote wakiamua kulivalia njuga suala la rushwa kwenye magazeti yao, na kusisitiza "wewe Kibanda, mimi nakuaminia sana kwenye gazeti lako, ukiamua unaweza!".
   
 11. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Mimi namkubali sana Gerald, hata hivyo kipindi chao ni kipindi ambacho kina manufaa sana kwa wananchi. Kudos Gerald & PB crew
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Unazungumzia Uhuru wa TAKUKURU unaishia kwenye uhuru wa kuchunguza bila kuingiliwa na kufikisha mbele ya sheria. Amesema TAKUKURU inaweza kuomba bajeti na serikali huamua kuitekeleza inavyoweza.

  Amesema suala la independence ni relative, vyombo vyote vinategemeana, hakuna absolute independence, Bunge linatunga tuu sheria lakini anayeitafsiri hiyo sheria ni mahakama na anayeitekeleza ni serikali. Kila chombo kina uhuru unaishia kwenye mipaka yake bila kuingilia uhuru wa chombo kingine.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Kibonde nae kauliza swali kuhusu watchdog wa PCCB ni nani, Dr. Hosea kajibu ni wananchi, akasisitiza, hakuna mtu yoyote ambaye yuko above the law, kama watu wanaona TAKUKURU inafanya madudu, waibandike magazetini, wamulikwe etc.

  Kumbe Kibonde sometimes is sensible, mlio karibu na Kibonde, mjulisheni kuwa ana kipaji kikubwa cha comedy lakini lazima a-balance serious issues na mizaha ili kuilinda heshima yake, na Gadner apunguze kumchagiza au kuitia utambi pale anapotapika utumbo na hapo hapo kumeza ma..shi yake!.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Yes Pasco hapo juu nami nimelisikia hilo nakuona huo nao ni udhaifu; inakuwaje unakuja na ahdi ya kutimiza kitu 2013; una uhakika gani tutakurudisha madarakani? Well mnyonge mnyongeni haki mpeni pia!

  Clouds FM hongera pamoja na kuwa kuna vitu vingi mnakwenda tofauti na mtazamo wangu! Endeleeni kutuleta hawa ikiwezekana hata waliotoa hukumu ya Liyumba na Kamanda Mwema! Hata Presida mwenyewe eeh ndiyo bana!
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Thanks Max. Leo kitufe cha thanks kimenigomea, ni mimi tuu au?.
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ilinipita hiyo post; naomba link nikaisome
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Pasco tatizo hapa na hilo la uchaguzi huru na wahaki maana vyombo vinavyo simamia huo uchaguzi vyote vipo kwa niaba ya serekali.

  Sasa Hosea anasema anayo orodha ya waliotoa zawadi kuelekea uchaguzi na asilimia kubwa ya waliofanya hivyo ni kutoka CCM sasa tusubiri hiyo hatua maana tunaona na tunasikia kupitia vyombo vya habari watu wkitoa zawadi na kuchangia shughuli mbalimbali.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,318
  Trophy Points: 280
  Dr. Hosea keshamaliza, ila pia alifafanua kuhusu ugawaji wa vijizawadi kama pikipiki, baiskeli, t-shits etc kuwa vijana wake watawaita wahisani na hao wafadhili wote na kuwahoji pesa wamepata wapi and why now, wakikosa maelezo ya kutosheleza safari yao kisiasa itaishia kizimbani (sio kile cha Zanzibar).

  Kama ni zawadi, zitolewa kwa chama husika, hala ni uongozi wa chama utaamua mahali hapa ndipo tupeleke msaada huu na sio mtu anawania Tandahimba, huyo na mapikipiki 100 kuwagawia vija na Tandahimba, hiyo ni rushwa!.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa nafikiri ulitaka kusema PJ au sio mkuu?
   
 20. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mzee Mwanakijiji,

  Hakuna sheria ambayo iko kamili, sasa je wewe unaona ilikuwa bora hii sheria kutokuwepo?

  Pamoja na mapungufu yake mimi bado naamini ni bora hii sheria imeanza kufanya kazi na kama PCCB watatimiza wajibu wao basi huenda kukawa na mafanikio hata kama haitakuwa asilimia 100.

  Hata sasa kuna sehemu ambako waliokuwa wanajiandaa kumwaga mapesa sasa wamekaa kimya baada ya kuona sheria inawabana. Hilo pekee tayari ni mafanikio.
   
Loading...