Kutengeneza ngozi kwa kutumia vitu asilia

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
26,305
50,477
Habari yenu warembo na watanashati?

Katika maisha yetu ya kila siku tunapitia mambo mbalimbali yanayosababisha ngozi kuharibika, kufubaa au kupata chunusi, mapele na madoa,lakini haimaanishi kuwa hauwezi tena kurudia urembo wako wa asilia.

Tatizo kubwa ni matumizi ya vitu vyenye kemikali ambapo badala ya kurudisha ngozi katika uasilia, unazidi kuiharibu katika maisha yetu ya kila siku kuna mimea na vitu asilia vinavyotuzunguka ambavyo waweza kukupa muonekano bomba na wa kudumu.

Tuanze na habawtsoda (black seeds) hizi ni mbegu ambazo husagwa na kutoa unga, ama mafuta ambayo yanaweza kutumika kuondoa chunusi, harara, kung'arisha ngozi na matumizi yake ni nafuu sana.
9fcfed29c3c929378aa271cfb54eda46.jpg
b97fb809cd21610ea3982ed6356cfdba.jpg

Bentonite clay huu ni udongo asilia ambao unasaidia kusafisha ngozi, kuondoa chunusi mba na kung'arisha ngozi inayofubaa
matumizi yake pia ni nafuu.
f841b2629364d223105130cce05e0856.jpg

Manjano (turmeric) hii unaweza kuitumia ikiwa katika unga uliosagwa kutokana na manjano yenyewe iliyofanana na tangawizi manjano hii inafaa kusafisha uso, kung'arisha ngozi inayofubaa, kuondoa chunusi mba na harara kwenye ngozi.

Hivi ni baadhi tu mwaweza kuongezea na nitaongeza kadri muda utakavyoniruhusu.
3b142aec1966d72eee8e665063efd745.jpg
 
Kuna njia ya kutumia
Udongo..wachanganya na asali it works pia..., waweza weka na Tango pia.. unanawa uso vizuri then wapaka mchanganyiko wako... au badala ya udongo waweza weka Manjano... I hate manjano cos inabidi uwe extra careful yale manjano
 
Helow @stablewoman unatumiaje manjono nipe procedure plz..!
Huwa nayatwanga kwenye kinu kidogo halafu yakilainika vizuri naanza kujipaka usoni kwa kuyasugua polepole hadi nahisi vinyweleo vinafunguka hivi, nakaa na majimaji yake had yakauke kwa dk kama5 hv then naenda kuoga na sabun ya kawaida! Ni mazuri nimeyazoea
 
Kuna njia ya kutumia
Udongo..wachanganya na asali it works pia..., waweza weka na Tango pia.. unanawa uso vizuri then wapaka mchanganyiko wako... au badala ya udongo waweza weka Manjano... I hate manjano cos inabidi uwe extra careful yale manjano
Kwahiyo tango linakuwa limesagwa au likiwa zima??
 
Kwahiyo tango linakuwa limesagwa au likiwa zima??
Unakata kipande unakamua juisi yake unapaka usoni,unakaa nayo kidogo mpaka ikaukie kisha unanawa,unaweza pia kuchanganya juis ya tango na nyanya ukapaka usoni vile vile,baada ya muda unanawa,matokeo yake si ya papo kwa hapo,hivyo unatakiwa uwe mvumilivu kidogo.
 
Unaweza pia kuchanganya unga wa dengu na yai la kienyeji,unachanganya vizuri kisha paka mchanganyiko wako usoni na sehemu yote ya shingo.unakaa nao kwa dk kama 15 mpaka ukaukie vzr kwenye ngozi,inakamata ngozi kama facial mask,kisha unanawa,you will feel the changes instantly. Ngozi inakua laini kama ya kitoto kichanga.
 
Unakata kipande unakamua juisi yake unapaka usoni,unakaa nayo kidogo mpaka ikaukie kisha unanawa,unaweza pia kuchanganya juis ya tango na nyanya ukapaka usoni vile vile,baada ya muda unanawa,matokeo yake si ya papo kwa hapo,hivyo unatakiwa uwe mvumilivu kidogo.
Nimekupata boss wangu! Asante
 
Dah wanawake wanamambo mengi kweli. Yani vyakula badala ya kuliwa vinageuzwa mafuta..........nilikuwa napita tu...
 
Back
Top Bottom