Jinsi ya kutengeneza kiuadudu cha asili kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini

Mashima Elias

Member
Dec 22, 2010
18
52
Jinsi ya kutengeneza kiuadudu cha asili kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini.

Okoa fedha na linda afya za walaji kwa kutumia viuadudu vya asili kudhibiti wadudu shambani kwako.

Fuata hatua zifuatazo kutengeneza kiuadudu kwa kutumia mbegu za mti wa mwarobaini.

Kwanza tafuta mwarobaini wenye matunda ambayo yana rangi ya kijani na manjano na kisha vuna matunda yenye rangi ya majano hayo ndiyo matunda yaliyokomaa au kuiva.

Vuna matunda hayo na yaanike kwenye jua kwa takriban siku 3 hadi 4 ili yakauke.

Hakikisha matunda yanageuka na kuwa na rangi ya kahawia.

Ponda ponda hayo matunda ili kutenganisha ganda la juu na mbegu bila kuvunja mbegu ya ndani.

Kisha pepeta ili kutenganisha maganda na mbegu au kiini cha ndani.

Baada ya hapo chambua mbegu nzuri na zilizokomaa unashauriwa kuchagua zile zenye rangi nyeusi zinafaa zaidi zile zenye rangi nyeupe unashauriwa kuziacha.

Weka mbegu ulizo chagua kwenye chombo kisha ziponde mpaka ziwe unga mlaini

Chukua unga wako na changanya na maji safi.

Uwiano mzuri wa uchanganyaji ni gramu 350 za unga wa mbegu za mwarobaini kwa lita 10 za maji safi.

Acha mchanganyiko utulie kwa masaa 24 kabla ya kutumika.

Chuja mchanganyiko huo kuondoa chembe ndogo zinazoweza kuziba Kichujio cha kinyunyizi au solo

Baada ya hapo kiuadudu chako kitakua tayari kwa matumizi.

Kinyunyizi chenye ujazo wa lita 15 kinapaswa kitumike kwenye eneo la takribani mita za mraba 400.



Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
SWALI: Baada ya kuchanganya Mbegu iliyopondwa gram 350 kwa maji lita 10. Hiyo dawa wakati wa kuitumia tatakiwa kuichanganya na maji tena. Ama ndio huo huo mchanganyiko wake. Kwamba Nikihitaji zaidi nikaponde mbegu nyingine?
 
SWALI: Baada ya kuchanganya Mbegu iliyopondwa gram 350 kwa maji lita 10. Hiyo dawa wakati wa kuitumia tatakiwa kuichanganya na maji tena. Ama ndio huo huo mchanganyiko wake. Kwamba Nikihitaji zaidi nikaponde mbegu nyingine?
Usichanganye na maji tena!! ukiongeza maji utapunguza nguvu yake hivo ufanisi wake utapungua, kama shamba ni kubwa jitahidi kupata mbegu za kutosha ziendane na mahitaji kwa mchanganyiko sahihi utapata matokeo mazuri shambani.
 
Unaweza pia ukachukua

* Sabuni ya unga , majani ya mwarobaini Yale yenye ukijani zaid .

* Yasage au ponda majani mpaka yaive ,chukua maji Lita 5 ,changanya na mwarobaini na yachuje,.

* Chukua sabuni ya unga changanya na mchanganyiko wa mwarobaini na maji ,yaweke juani kwa nusu saa.

Dawa yako itakuwa tayari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom