Kutembea wawili wawili

Kutembea wawili wawili

Hakuna familia isiyo na mapungufu, hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu,tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake,tumevunjana moyo na kukatishana tamaa,kwa hiyo hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.

Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.

Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo,eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa,jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu, huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.

One love.
 
Nijuze wanajukwaa,hivi mume na mke kutembea barabarani wakiwa pamoja( wakati mwingine wamempakata mtoto)',kanisani wote, mvua au jua wore in UPENDO WA DHATI AU DANGANYA TOTO!!!
hayo ni maisha baina ya wanandoa mengineyo ni mtazamo wako maana maamz ya couple yapo ndan yao wenyew na wala cdhan kama ni busara kupoteza muda kutaft nn maana ya yafanywayo na wana ndoa
 
Nijuze wanajukwaa,hivi mume na mke kutembea barabarani wakiwa pamoja( wakati mwingine wamempakata mtoto)',kanisani wote, mvua au jua wore in UPENDO WA DHATI AU DANGANYA TOTO!!!


Hiyo ni sinema tu kwani baada ya hapo mwanaume au mke anakwenda kuchapa nyumba ndogo au kuchapwa na mshua wa kitaa. Sinema hizi Bongo ni nyingi sana na wala hazina lebo ya TBS.
 
Back
Top Bottom