Kutembea ukiwa usingizini

Kuna mdogo wangu alianza kutembea akiwa usingizin hadi umbali wa km 1 na zaidi pindi akiwa shule mpaka sasa tatizo lishakuwa kubwa (kifafa) tumezunguka hospital kubwa zote hapa nchin hatujafanikiwa tumejaribu tiba mbadala napo hakuna matumain je tumsaidiaje huyu mgonjwa ili apate nafuu aendelee na masomo yake
 
Mmh kwakweli hapa ni ngumu kusema kuwa naweza kusaidia chochote kama huko kote imeshindikana ila ngoja nitapita huku na kule nione kama anaweza kusaidika
 
Nimekupata mkuu, ahsante kwa majibu, jengine Mara nyingi hua tunakwenda na kupita kwenye shamba lake, sikumbuki hata siku moja kumuona analima au anapalilia hata kupanda, wala sijabahatika kumkuta mtu akifanya hiyo kazi, kwa miaka yote niliokaa pale. Lakini hilo shamba liko safi, rutuba ana mazao ya kumwaga.
 
Linahudumiwa na vibarua ila nyie hamuwaoni, inawezekana ni misukule au ni watu tu wengine lakini nyie hamuwaoni
 
Naomba kuuliza hili linanihusu mwenyewe. Nilivyokuwa kijijini ndoto zangu nyingi huota kuwa ninaruka, kuvuka bahari nahata milima nawakati mwengine kwenda nchi mbali mbali ambazo hata sizifahamu. Baada ya miaka kazaa nikabahatika kusafiri kwa kiasi, na baazi ya nchi mzingira yake yanafanana na nchi zile nilizokuwa naota. kilichokuwa kinanishangaza, miaka ilipoenda, hata kama niko kwenye mji wowote ule mkubwa kwa mfano NY,nikilala naota niko kijijini na naishi maisha ya ufukara sana. jengine huota naendesha gari cha ajabu nakuwa naendesha bila kuona mbele au naendesha gari inarudi nyuma tena kwa spidi kubwa. Kilichonitisha kabisa nimeota nimepata kichaa naishi na kula kwenye majalala. Hebu nipe fikra zako
 
Naomba nipe muda kwenye hili tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…