Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na na polis walioteuliwa, leo Raisi amedokeza kuhusu ukimya wa tukio la kutekwa kwa Mo Dewji.
Amesema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa
Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi."
Hii ni TAA NYEKUNDU! Kama Polisi hawafanyi uchunguzi, kikwazo ni nini au ni nani? Tuanzie hapo.
Lakini je, vipi kuhusu kesi za kutekwa Roma?, Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye?, Mwana Habari Azory Gwanda? na wengine kesi zao zimefika wapi?
Vipi kesi ya kupigwa risasi Tundu Lissu, upelelezi umefika wapi? Anasubiriwa arudi TZ?