Kutekwa kwa MO Dewj kwaanza kuanikwa, vipi Roma? Saanane? Azory Gwanda? Kupigwa risasi Tundu Lissu? Wengine je? Polisi mmepewa neno leo, shughulikeni.

Siku zote Bashite anapokuwa ikulu kwenye hafla mbalimbali hata za kuapisha maskari waku huwa hahoiji hilo, leo Bashite yupo Bukoba kwenye msiba wa Ruge ndio anahoji?! Haahaaaaa, kweli nimeamini Bashite ni zaidi ya wote mpaka mkuu ana muhofia..
 
Kwanini anaulizwa Mo wakati kuna wengi tu ambao mpaka Leo hawajarudi na haijulikani walipo bora Mo kapatikana, nadhani suala la mwandishi wa mwananchi Azory na wengine ndiyo lingekuwa bora zaidi kupima weledi wa jeshi letu

Mtu anapotea kwa kutekwa mpk leo hajulikani na polisi wapo wala hawatoi hata taarifa juu ya hatua gani wamefikia ktk utafutaji kuonyesha kama wanajali yaani wapo tu kana kwamba aliyepotea ni mdudu tu kumbe ni baba wa watoto, ni mme, ni mtu anayetegemewa na jamii yake wao hawajali hayo. Hii ni hatari kwa chombo ambacho ndicho kinalinda usalama wa raia na watu kama hao ndiyo Rais anapaswa kuwaulizia

Hao wengine waliopotea tulishaambiwa wamekwenda kutafuta maisha. Kwa hiyo wala polisi hawahangaiki na hata kauli ya mkuu inathibitisha hilo.
 
Katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na na polis walioteuliwa, leo Raisi amedokeza kuhusu ukimya wa tukio la kutekwa kwa Mo Dewji.

Amesema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi."

Hii ni TAA NYEKUNDU! Kama Polisi hawafanyi uchunguzi, kikwazo ni nini au ni nani? Tuanzie hapo.

Lakini je, vipi kuhusu kesi za kutekwa Roma?, Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye?, Mwana Habari Azory Gwanda? na wengine kesi zao zimefika wapi?

Vipi kesi ya kupigwa risasi Tundu Lissu, upelelezi umefika wapi? Anasubiriwa arudi TZ?
Kama rais analalamika na sisi wananchi tutafanyeje?yeye si ndiye mwenye uwezo wa kuchukuwa hatua? Ili maswali hayo yajibiwe?
 
Asitake kujisafisha hata yeye awajibike,maswali ni mengi tumetulia nayo mioyoni siyokuwa tumesahau bali tunajua !
Anataka kuwasukumia zigo polisi waangaike nalo,na yeye aonekane hausiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa!Mtu badala ya kuchukuwa hatua, analeta unafikia eti "wananchi siyo wajinga", yes siyo wajinga, kwasababu wanafahamua anatakiwa achukuwe hatua na siyo hizi blah blah!
 
2019
2020......!
Kwanini sasa ,yeye ndie amiri jeshi mkuu walikuwa wapi Siku zote ,vipi wengine walikpotea Azory,kanguye ,Lissu , yaani anatuona watanzania mazuzu kweli mastermind .
tunatapeliwa mchana kweupeeeee!
mzee ashaanza kuomba saiti..amewasha endiketa za kulia
"I wish I cud be IGP", Pombe, mjasirimali wa vitambulisho.

Albadiri inaanza kufanya kazi yake.
 
Katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na na polis walioteuliwa, leo Raisi amedokeza kuhusu ukimya wa tukio la kutekwa kwa Mo Dewji.

Amesema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi."

Hii ni TAA NYEKUNDU! Kama Polisi hawafanyi uchunguzi, kikwazo ni nini au ni nani? Tuanzie hapo.

Lakini je, vipi kuhusu kesi za kutekwa Roma?, Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye?, Mwana Habari Azory Gwanda? na wengine kesi zao zimefika wapi?

Vipi kesi ya kupigwa risasi Tundu Lissu, upelelezi umefika wapi? Anasubiriwa arudi TZ?
Katika kitu ambacho wahindi, mungu aliwajalia ni ushirikina, unalogwa mpaka unachanganyikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[QUOTrch81, post: 30626064, member: 455130"]Tutegemee soon kupata kamanda mpya wa mkoa wa bashite

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE]
Siyo huyo tu bali mambo now na siro wajiandae kwani kati ya walioapishwa mmojawapo ni aigipi mpya!
 
Leo nimemwelewa Rais wangu,kumbe na yeye anakereka na jinsi jeshi la polisi lisivyotimiza majukumu yake kwa visingizio kibao.Kumbe suala la waliotekwa kikwazo sio maelekezo kutoka juu,bali ni uzembe,rushwa,upendeleo na weledi mdogo kwa jeshi letu.Najua hawapendi kuonekana wao ni wazembe na tena kama wangekuwa wananifahamu leo ningekiona cha mtema kuni!,ila wao kisingizio ni maelekezo toka juu,mara watu wasiojulikana n.k.Wakiulizwa kwa nini hampelelezi kesi za waliotekwa jibu ni rahisi maelekezo toka juu,kwa nini mnawaachia watuhumiwa waliokamatwa na vidhibiti jibu maelekezo toka juu yaani kila kitu ni majibu rahisi tu.Sasa rais kawaruka, hili la MO ni mfano tu, yapo mengi kuanzia watoto wa Njombe,vikongwe kanda ya ziwa,kupotea kwa wanaharakati mpaka kupigwa risasi kwa lissu,Polisi sasa hamkeni toeni majibu sasa,msione aibu rais kaonyesha mashaka kwenu ......
Nimeelewa kuwa watanzania walikuwa wanaunganisha dots za matukio mwishowe wanaona kuwa serikali inahusika kwenye matukio na tena wakaenda mbali zaidi kumuhusisha moja kwa moja mkulu na yule mkuu wa mkoa,lakini ni wao tu kwa sababu zao pengine kujipendekeza kwa kufanya kazi kwa staili ya sinema za hollywood wakiona labda mkulu anapendezwa na comedy.mfano mambosasa na dereva kwenye suala la mo.
Mweshimiwa rais jitenge na wote wasiofuata maadili ya kazi wakidhani wewe ndio unapendezwa nao.Sisi tunafarijika sana unapojitenga na haya makandokando na tena yapo mengi mkuu,naamini kwa uwezo wa MUNGU yote yatafunuliwa na mwishowe watajikuta wapo peke yao.
 
Ndiyo anakereka, lakini yeye kama bosi wao kachukua hatua gani?

Mbona wengine anawatumbua? Mfano: wale wa kikokotoo, wa korosho na wengine.
 
Back
Top Bottom