Kutekwa kwa MO Dewj kwaanza kuanikwa, vipi Roma? Saanane? Azory Gwanda? Kupigwa risasi Tundu Lissu? Wengine je? Polisi mmepewa neno leo, shughulikeni.

Mkuu wa kitengo cha watu wasiojulikana wanaoteka, kutesa na hata kuua pia Watanzania wasioena hatia yoyote.

Katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na na polis walioteuliwa, leo Raisi amedokeza kuhusu ukimya wa tukio la kutekwa kwa Mo Dewji.

Amesema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi."

Hii ni TAA NYEKUNDU! Kama Polisi hawafanyi uchunguzi, kikwazo ni nini au ni nani? Tuanzie hapo.

Lakini je, vipi kuhusu kesi za kutekwa Roma?, Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye?, Mwana Habari Azory Gwanda? na wengine kesi zao zimefika wapi?

Vipi kesi ya kupigwa risasi Tundu Lissu, upelelezi umefika wapi? Anasubiriwa arudi TZ?
 
watanzania sio wajinga hata yeye maigizo yake tulisha yazoea. aache kuigiza afanye kweli. watanzania hawezi kula maigizo wala hawawezi kulindwa na maigizo ya kichina na wala 50 million haziwezi kwenda kila kijiji kupitia kwenye TV. wala tundu Lissu hakuigiza kupigwa risasi, alphonce Mawazo,Bene sanane, na wengine wegi yaliyo wapata sio maigizo, familia zao bado zinamajozi.
 
Leo nimemwelewa Rais wangu,kumbe na yeye anakereka na jinsi jeshi la polisi lisivyotimiza majukumu yake kwa visingizio kibao.Kumbe suala la waliotekwa kikwazo sio maelekezo kutoka juu,bali ni uzembe,rushwa,upendeleo na weledi mdogo kwa jeshi letu.Najua hawapendi kuonekana wao ni wazembe na tena kama wangekuwa wananifahamu leo ningekiona cha mtema kuni!,ila wao kisingizio ni maelekezo toka juu,mara watu wasiojulikana n.k.Wakiulizwa kwa nini hampelelezi kesi za waliotekwa jibu ni rahisi maelekezo toka juu,kwa nini mnawaachia watuhumiwa waliokamatwa na vidhibiti jibu maelekezo toka juu yaani kila kitu ni majibu rahisi tu.Sasa rais kawaruka, hili la MO ni mfano tu, yapo mengi kuanzia watoto wa Njombe,vikongwe kanda ya ziwa,kupotea kwa wanaharakati mpaka kupigwa risasi kwa lissu,Polisi sasa hamkeni toeni majibu sasa,msione aibu rais kaonyesha mashaka kwenu ......
Nimeelewa kuwa watanzania walikuwa wanaunganisha dots za matukio mwishowe wanaona kuwa serikali inahusika kwenye matukio na tena wakaenda mbali zaidi kumuhusisha moja kwa moja mkulu na yule mkuu wa mkoa,lakini ni wao tu kwa sababu zao pengine kujipendekeza kwa kufanya kazi kwa staili ya sinema za hollywood wakiona labda mkulu anapendezwa na comedy.mfano mambosasa na dereva kwenye suala la mo.
Mweshimiwa rais jitenge na wote wasiofuata maadili ya kazi wakidhani wewe ndio unapendezwa nao.Sisi tunafarijika sana unapojitenga na haya makandokando na tena yapo mengi mkuu,naamini kwa uwezo wa MUNGU yote yatafunuliwa na mwishowe watajikuta wapo peke yao.
Lies,lies,lies! ?????????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na na polis walioteuliwa, leo Raisi amedokeza kuhusu ukimya wa tukio la kutekwa kwa Mo Dewji.

Amesema, "Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa

Tulioneshwa nyumba na dereva lakini hadi leo hakuna aliyepelekwa Mahakamani. Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa 'clear'. Mambo haya yanalitia doa Jeshi la Polisi."

Hii ni TAA NYEKUNDU! Kama Polisi hawafanyi uchunguzi, kikwazo ni nini au ni nani? Tuanzie hapo.

Lakini je, vipi kuhusu kesi za kutekwa Roma?, Mwenyekiti wa Halmashauri Kibondo Mr. Kanguye?, Mwana Habari Azory Gwanda? na wengine kesi zao zimefika wapi?

Vipi kesi ya kupigwa risasi Tundu Lissu, upelelezi umefika wapi? Anasubiriwa arudi TZ?
Mzee baba katumia mbinu ya kujificha. Baba ikimtoka gesi mbele ya hadhara ya watu husingizia watoto ili kuficha aibu yake, na kama wewe ni mtoto inabidi uwe mpole tu kuficha aibu ya baba ...wele wako ukanushe!!!
 
Hiyo ya kuwasukumia wenzie ndo tabia yake kuuu.kumbuka issue ya kikokotooo alivyomtosa yule mama wakati kwa mkono wake ndo aliesaini ule muswaada na kuufanya kua sheria.

Jamaa ni bingwa wa kujitoa mambo yanakua kombo.hata kwenye korosho alifanya haya haya.
Asitake kujisafisha hata yeye awajibike,maswali ni mengi tumetulia nayo mioyoni siyokuwa tumesahau bali tunajua !
Anataka kuwasukumia zigo polisi waangaike nalo,na yeye aonekane hausiki?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom