KUTEKWA KWA MDUDE NA SAUTI YA KANISA NCHINI

KUTEKWA KWA MDUDE NA SAUTI YA KANISA NCHINI

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,708
Reaction score
35,719
Ndugu Mpaluka Said Nyangali (Mdude) amepatikana jana usiku akiwa hajitambui kule Inyala Mkoani Mbeya. Leo nimeona video yake na picha akiwa anaongea kwa tabu hospitalini asubuhi hii. Ninamshukuru Mungu kwa kusikia maombi, vilio, na sauti za watu wengi waliokuwa wakiomba Mdude asiuawe na kuwafanya watekaji wake wasiutoe uhai wake.

Niliposikia habari za kupotea kwake nilihudhunika na kuugua sana moyoni. Kijana huyu simjui lakini nafsi yangu ilinitaka niwe miongoni mwa watu wakupaza sauti ili kutetea uhai wake. Nilipoanza kuandika kuhusu tukio lake wako watu waliotaka ninyamaze! Kwao waliona kama Askofu anafanya siasa! Hawakuzoea Askofu katika Nchi hii kufanya kwa namna au staili yangu! Lakini walisahau kuwa hatufanyi kwa mazoea. Matukio haya hayakuwepo huko nyuma hivyo isingekuwa rahisi kumuona Askofu akitetea matukio ambayo hayapo. Matukio ya watu kutekwa na kupotea yalianza kama mchezo na sasa yameshamiri na hata kufikia kuzuka kwa kundi la 'watu wasiojulikana'! Hatuwezi kunyamaza kimya wakati uhalisia wa hofu kujengeka nchini unaonekana wazi. Kila mtumishi wa Mungu hutumika kulingana na zama zake na hupambana na maovu ya wakati huo!

Ninaomba tuendelee kumuombea Mdude ili Mungu amrejeshee afya yake. Wakati mwingine nitakuja kusema na mioyo ya watekaji na wale waliowatuma (kama walitumwa). Lakini hapa nataka niseme na moyo wa Mdude. Ninapenda Mdude aelewe kuwa Mungu anampenda sana! Yeye aliyemuokoa kutoka katika mikono ya watekaji anatufundisha kuwasamehe waliotukosea. Ninamuomba Mdude amuombe Mungu amsaidie kusamehe. Ninaomba wamsomee Zaburi 23 ili aone jinsi Mungu alivyomfanya avuke salama katika bonde la uvuli na mauti.

Mwisho ninapenda niongee na Maaskofu, Wachungaji na Watumishi wenzangu. Nchi hii imetumbukia katika maovu na mambo mazito ya kutisha na yanayomchukiza Mungu. Tukumbuke kuwa wito wetu ni pamoja na kutokufumbia macho maovu. Tusiogope kuonya, kukemea, na kutahadharisha. Ni rahisi sana kukemea maovu yanayofanywa na vibaka na machangudoa kuliko kukemea maovu yanayohusisha makundi ya watu wenye nguvu, pesa, mamlaka, au ushawishi. Maovu yanayoratibiwa (organized crimes) ni hatari zaidi katika jamii ye yote ile.

Lakini tukumbuke kuwa sisi ndio tunatakiwa kupaza sauti na tusipopaza sauti tutakuja kudaiwa na Mungu wetu. Mara nyingi mambo haya hayana taarifa! Tusisubiri vikao vya Halmashauri zetu (ingawa vina umuhimu) kukaa ndipo tupaze sauti! Tukifanya hivyo tutatoa nafasi maovu kujiimarisha. Kila Askofu au kila Mchungaji anao wajibu wa kupaza sauti kama yeye na kukemea au kuonya au kutia moyo. Tujikumbushe vizuri kuhusiana na sauti ya mtumishi wa Mungu katika Biblia katika kitabu cha Ezekieli 33:1-20. Katika kifungu hiki na Biblia nzima hakuna mahali ambapo jukumu la kupaza sauti limeamriwa lisubiri Halmshauri au Sinodi au Kamati au Mikutano mikuu. Nasisitiza kuwa jukumu hili ni la kila mtumishi kwa nafasi yake ingawa umoja una nafasi yake. Watu wakisikia sauti ya Askofu watakuwa wamesikia sauti ya Kanisa na Askofu akinyamaza Kanisa litakuwa limenyamaza na Kanisa likinyamaza litakuwa limekoma kuwa NURU!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
FB_IMG_1557388564133.jpeg
 
Kanisa, na hasa Kanisa langu la RC lina kitu cha kujibu mbele za Mungu. Uovu na waovu hawastahili kutengwa na Kanisa lakini wanastahili kuonywa. Ni kosa na ni chukizo mbele za Mungu wetu, Kanisa kujishikamanisha na uovu na waovu.

Kanisa badala ya kukemea uovu na waovu, linaposhikamana na waovu, na kuwasafisha waovu, tena bila ya toba, ni kufuru kubwa mbele ya mkuu wa Kanisa, ambaye ni Kristo Mfufuka. Tusizinajisi madhabahu za Bwana, kwa kuzitumia kuwasafisha waovu na mawakili wa shetani.

Mungu wetu wa Hekima, tunamwomba, awajalie viongozi wetu wa dini hekima ya utambuzi dhidi ya uovu na unafiki.
 
RC wao ndio waanzilishi wa mateso mauaji na kila aina ya ufedhuli Roman empire ni mama wa maovu
 
Kanisa, na hasa Kanisa langu la RC lina kitu cha kujibu mbele za Mungu. Uovu na waovu hawastahili kutengwa na Kanisa lakini wanastahili kuonywa. Ni kosa na ni chukizo mbele za Mungu wetu, Kanisa kujishikamanisha na uovu na waovu.

Kanisa badala ya kukemea uovu na waovu, linaposhikamana na waovu, na kuwasafisha waovu, tena bila ya toba, ni kufuru kubwa mbele ya mkuu wa Kanisa, ambaye ni Kristo Mfufuka. Tusizinajisi madhabahu za Bwana, kwa kuzitumia kuwasafisha waovu na mawakili wa shetani.

Mungu wetu wa Hekima, tunamwomba, awajalie viongozi wetu wa dini hekima ya utambuzi dhidi ya uovu na unafiki.
Kweli kanisa katoriki,linapaswa kujitafakali,Mara mbili,waovu wapo ndani ya kanisa wanapaswa kuambiwa watubu kwanza ili washiriki ibada ya ushirika mtakatifu
 
Wanamteka wenyewe, wanamtesa wenyewe, wanamjeruhi Karibu ya kumuua, wanamtupa porini wenyewe, wanamuokota wenyewe, wanampeleka hospitalini wenyewe, halafu wanakuja kumuhoji wenyewe.
Hawa ni watu wapumbavu kabisa.
Inyala Ndiyo Kuna kituo cha kutesea mahabusu, kama Sitaki Shari ilivyo kwa DSM
 
haya jamaa ni kenge sana
 
Back
Top Bottom