Kutapeliwa

Kutapeliwa

Magari damu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2020
Posts
443
Reaction score
778
Wakuu habari yenu, jana kuna kitu nlimuuzia jamaa fulani hv. Yeye alisema yuko mkoani, so ikabidi tufanye arrangements ili tukutane na ndugu yake alieko Dar uko, ili nimpe mzigo wake.

Baada ya yule ndugu yake kuuona na kuridhika, ikabidi ampigie mteja wangu kwamba mzigo uko vizuri. Nikawa nimeongea nae akasema atanitumia kwenye number ya airtel iko kiasi tulichokua tumekubaliana. Kwa kua mimi sina number ya airtel ikabidi nimwambie rafiki yangu kuwa kuna muamala utatumiwa kwenye simu yake maana yeye ana line ya airtel.

Basi, kama baada ya dakika nane yule rafiki yangu anaetumia line ya Airtel akanambia ameona pesa imeingia kutokea NMB. Mimi nikasema sawa, nikamkabidhi yule ndugu yake mzigo tukaachama pale.

Ile message inaonekana imetokea NMB, kwamba katumia huduma ile ya benki mkononi kunitumia hela. Basi, kwa kua ilikua ni jioni sana hata mabenki yalikua yamefungwa nikasema asubuhi ya leo nitawahi bank nikaihangaikie. Cha ajabu nafika bank wananiambia hakuna muamala wa dzain hiyo kwa benki yao. Sikukata tamaa ikabidi niwacheki pia kwa mitandao yao ya kijamii (instagram) ila majibu yakawa ni yale yale.

Mteja wangu nliefanya naye biashara, wakati niko bank nilikuwa najaribu kumpigia ila hakupatikana, ila dakika 20 kabla ya kuanza kuandika huu uzi nlijaribu kumpigia akasema ngoja amcheki wakala ambae alimtumia kunitumia hiyo hela. Ndo niko namskilizia hapa.

Naombeni ushauri kama kuna mtu anaweza kuwa na idea na hiki kitu au anaeweza kuwa na wazo lingine anisaidie wakubwa.

Natanguliza shukrani.

IMG_2364.jpg
00c9e59a-f848-4741-a172-b0f450944557.jpg
 
Pole Sana, vuta subira upate majibu kutoka kea WAKALA mtuma pesa pia nakushauri pita kea mawakala was NMB Uwaulize Kama issue Kama hizo huwazinajitokeza wafanyapo miamala? Calm down
 
Utapeli umezidi sasa, kabla ya kukamilisha dili na mtu hebu jaribu kumpigia mtu wako wa karibu ili akushauri. Pole.
 
Nina wasiwasi nilo neno NMB kwenye picha yako ya meseji mbona ina nukta mbele? (NMB.) why?
IMG_9732.jpg

Hiyo ni meseji niliyotumiwa kutoka NMB lakini haina nukta huko mwisho, ila meseji yako ina NUKTA hapo mwisho., au ni kwangu tu
 
Nina wasiwasi nilo neno NMB kwenye picha yako ya meseji mbona ina nukta mbele? (NMB.) why? View attachment 1488576
Hiyo ni meseji niliyotumiwa kutoka NMB lakini haina nukta huko mwisho, ila meseji yako ina NUKTA hapo mwisho., au ni kwangu tu

Asante ndugu, Na mimi pia ndo wasiwasi wangu ukianzia hapo. Nilijaribu kuangalia hata message za tigo pesa ila sikuona hiyo nukta kwa mbele. Ikaniongezea mashaka zaidi
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Pole Sana, vuta subira upate majibu kutoka kea WAKALA mtuma pesa pia nakushauri pita kea mawakala was NMB Uwaulize Kama issue Kama hizo huwazinajitokeza wafanyapo miamala? Calm down

Asante ndugu... masaa mawili sasa yamepita tangu anambie anawasiliana na wakala. Ila kwa sasa hv hapokei simu zangu
 
Kwani muamala wa Bank unachagua laini? Kwanini atake Airtel? Aisee kuwa makini huenda ni wakala wa Airtel kafanya maujanja.

Inaweza kua ndugu. Ila sasa kilichonipa amani ni kwamba yule rafiki yangu alinambia imetoka NMB moja kwa moja. So nikawa nimemake conclusion kwamba itakua imefika. Kumbe its a fraud.
 
Kwenye hiyo message umeona sender ameandikwa (NMB.) Mchezo wote uko hapo mkuu.

Pole sana,nmb hawawezi kukusaidia,hawahusiki hapo.

Thank you ndugu... what would you advise me to do. Nifanye go-ahead gani?
 
Kila kukicha wajinga wanazaliwa.

............pesa ndefu kama hiyo kwanini hukumpa akaunti namba akadeposit huko?

Asante kwa kutambua ujinga wangu Kuhusu kumpa account, Soma vizuri tena boss. Ilikua jioni, so banks pia zilikua zishafungwa. Na pia nisingekubali aje akanitumie labda kesho yake. Ingekua ngumu ndugu yangu
 
Back
Top Bottom