Laiti ungejua wanawake huwa wanawaza nini akilini mwao ungebadili kichwa cha habari cha hii thread yako.
Nimewaza tuu kuwa;
1. Yaweza kuwa huyu mama anaishi nyumba ya kupanga na ananyanyaswa hivo alijibana kununua kaeneo na hapo hela ya ujenzi hana akilini mwake amejipa uwezo wa kujenga nyumba japo matofali yamepinda ila anataka walale huru yeye na wanae.
2. Yawezekana mumewe ni mlevi au amefariki hivo hana msaada wa mahali pa kuishi hivo anapambana kujenga kwake ili alale na wanae hata kama hatakuwa na chakula.
3. Yawezekana hicho ni kibarua hali ngumu anafanya hivyohivyo kwa shida watoto wake waende shule na wapate chakula.
4. Ukiona mwanamke anahangaika kufanya kazi ngumu ujue nyuma yake kuna wazazi wanaomtegemea au watoto wasio na malezi ya baba au ana wadogo zake wanaomtegemea.
Hata hivyo mpiga picha kama sio wewe ndo anajua nini kinaendelea kwa huyu mama, laah kama ni wewe ndo Umempiga picha na ameamua tuu kufanya hiyo kazi bila sababu yeyote au kuwa na shida yeyote basi itakuwa anaigiza muvi au kidogo hayupo sawa.
Usiku mwema.