OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,199
- 103,733
Kwa mara ya kwanza nilimuona Bwn.Joseph Kasheku (Msukuma) akiwa kwenye kipindi cha siasa Star TV, akatambulishwa kama Mwenyekiti wa CCM Geita.
Sikumtilia maanani sana kwa kuwa alijaa majigambo kuliko hoja, tofauti na makamanda wa SAUT ambao walijenga hoja nzito. Alionekana bwana mdogo tu hivi!
Ghafla nikasikia Mh. Mwigulu anakata mawimbi na "Chopa la Msukuma". Na leo pale kwenye Safari isiyo na Matumaini kafanya taiz kutua na Chopa.
Sasa wanaomjua vizuri watupe details, huyu ni nani hasa, katoa wapi mapesa haya yote, halafu kama vile kwa umri mdogo!!
Huyu Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita anayeitwa Joseph Kasheku ‘Msukuma'.
Alitumia helikopta kwenda kwenye mkutano wa Edward Lowassa ambao aliubatiza jina la Mwanzo wa Safari ya Matumani.
Kama hiyo haitoshi, alifanya juhudi zote kuhakikisha anatua kati kati ya kiwanja kuonyesha ulimwengu uwepo wake pamoja na uwezekano wa kuhatarisha maisha ya wananchi.
Huyu Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita hakuishia hapo, alizunguka mikoani na Edward Lowassa kusaka wadhamini na kilele chake kilifikia pale alipojitokeza mbele ya vyombo vya habari wakati Lowassa anarudisha fomu na kudai CCM haina uwezo wa kuzuia mafuriko ya Lowassa na kufanya hivyo ni kujidanganya. Kwa lugha nyingine, alitaka CCM imteue Lowassa hata bila kufuata vigezo 13 iliyojiwekea na kutokufanya hivyo ni CCM kukumbwa na mafuriko ya Lowassa.
Kuonyesha kama alichokuwa anakisema kiligubikwa na ujinga au upumbavu, Kamati Kuu ilimkata Lowassa. Haikuishia hapo, bali Mkutano Mkuu ulimteua mwanachama ambaye siyo kwamba anatoka katika mkoa wake bali pia ni ndugu yake.
Na kama hiyo haikuishia hapo, Magufuli alienda kukaa kwenye kiti ambacho ni jirani na kiti cha huyu Joseph Kasheku kabla matokeo hayajatangazwa.
Magufuli alichokuwa anakifanya kwa Joseph Msukuma ni psychological taunting and torture.
Picha zinasema mengi yaliyokuwa yanapishana ndani ya ubongo wa Joseph Kasheku 'Msukuma'.
Kuna msemo wa kiswahili unaosema usibebe mayai yote kwenye kapu moja, hii ikimaanisha uchukue tahadhari maana ukipata ajali, mayai yote yatapasuka!
Mayai yote ya Joseph Kasheku ‘Msukuma' yamepasuka!
John Magufuri akiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita anayeitwa Joseph Kasheku ‘Msukuma' ndani ya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Wafanyakazi wa Usalama wa Taifa wakimzunguka Magufuli kabla ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura za kugombea Urais.
Picha inayoonyesha baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa mbali mbali walioambatana na Lowassa kwenda Makao Makuu ya CCM-Dodoma kurudisha fomu zake za ugombea Urais wa Tanzania. Mwenyekiti Joseph Kasheku 'Msukuma' (Geita) Mwenyekiti Bwarafia Silima (Unguja) Mwenyekiti Jesca Msambatavangu (Iringa) Mwenyekiti Madabida Madabida (Dar es Salaam), Mwenyekiti Hamisi Mgeja (Shinyanga), Mwenyekiti Msindai (Singida), Mwenyekiti Odo (Ruvuma), Mwenyekiti Sinani (Mtwara), Mwenyekiti Sanya (Mara), Mwenyekiti Mlao (Pwani), Mwenyekiti Kabouru (Kigoma) na Wenyeviti 3 (Pemba na Unguja).