Kutahiri watoto wa kiume sasa ni hatari

vevenononombo

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,289
420
Habari iliyotangazwa Leo na kituo cha televisheni cha jijini Mwanza (Star TV) juu ya watoto wawili mkoani Singida kupoteza uanaume wao kwasababu ya kutahiriwa vibaya na jamaaa anaejifanya kuwa mtaalam wakufanya hivyo .

Ni rai yangu kuwa wananchi wasitumie huduma hizo za vichocholoni kwani zinaharibu maisha ya watu fikiri hao watoto wakiwa wazima itakuwaje?
 
Ajali kazini.. kama vipi wazazi wa hao watoto wafanye mpango wamuhasi huyo mtaalamu feki
 
Ukilibakiza zongo pia ni pia sababu kama huku Rwanda mwanamke akikuta ni kipra wazi anakimbia anasema ukoma huo!
 
Aisee maumivu ni makali sana. Haswa kwa sisi tulioenda jando la kienyeji miaka ileee. Nakumbuka mpaka katika utu uzima huu. Jando bila ganzi. Unazamishwa mtoni asubuhi katika baridi Kali ndio ganzi yako hiyo.
 
Habari iliyotangazwa Leo na kituo cha televisheni cha jijin mwanza (star TV) juu ya watoto wawili mkoani singida kupoteza uanaume wao kwasababu ya kutahiriwa vibaya na jamaaa anaejifanya kuwa mtaalam wakufanya hivyo ni rai yangu kuwa wananchi wasitumie huduma hizo za vichocholoni kwani zinaharibu maisha ya watu fikir hao watoto wakiwa wazima itakuwaje?
Mbona kichwa cha habari na maelezo yapo tofauti? ungaliandika WAZEE WAWAPELEKE WATOTO KUTAHIRIWA KWA WATAALAM. Hapo tatizo jamaa alikuwa hana utaalamu ndio tatizo likatokea.
 
Kupelekwa jando bila ganzi ilikuwa ni ushujaa,halafu ilikuwa ni kwa wakubwa tu.
 
Back
Top Bottom