kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Waafrika kusini mwa jangwa la Sahara ni wahanga wakubwa wa umaskini (poverty), magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya hewa kama TB, flu kali kabisa. Magonjwa haya yamezoeleka sana ndani ya jamii hizi lakini hakuna watu wanaoyaundia task forces ili kujua nani ana flu na TB na nani amekufa ili kuwalinda watu wengine wasiambukizwe.
Hali yetu ya mavumbi, misongamano, na kuishi kwenye nyumba zisizokuwa na ventilation ya kutosha inasababisha magonjwa haya yaonekane ya kawaida kwenye jamii ingawa tunashuhudia yakingalimu maisha ya watu wetu kila siku. Ndiyo maana Hata leo hii wananchi na hata watoa huduma za afya wanashindwa kutofautisha kati ya mgonjwa mwenye mafua makali tuliyoyazoea siku zote na mgonywa mwenye Corona wanapokutana nae. Kuna wakati kila unaekutana nae mtaani na hospitali analalamika kuwa amebanwa na mafua makali. Watu huwa wanakambilia kusema kuwa ni mabadiliko tu ya hali ya hewa, msimu wa maua ya maembe, nk ilimradi tu kujustify sababu za outbreak ile ya mafua kwa kila mtu.
Na ndiyo maana hata wagonjwa tunaodhani wana Corona huwa wanapona wenyewe na inawezekana wapo wenye korona majumbani lakini wamepona wenyewe kwa kulamba tu asali, ndimu na tangawizi majumbani.
Watu wetu kwa maelfu huwa pia wanaliwa na Malaria kila siku; watoto, wajawazito na hata watu wazima ambao wanasababisha misululu mirefu hospitalini, wodini, kwenye klinic na hata kwa waganga wa kienyeji kusaka matibabu. Afrika huwa haihangaiki sana na kuunda task forces kujua ni kaya gani wacha tu kuwa na mgojwa wa malaria bali hata aliyekufa kwa malaria.
Kufa kwa Malaria kumezoleka pia kwenye jamii zetu. Tunayo idadi kubwa sana ya watu wetu hawaendi makazini, shuleni, na kwenye shughuli zao mbalimbali kwa sababu ya malaria tu. Nchi zetu zinatumia hela nyingi sana kuhudumia wenye Malaria, lakini hakuna task forces za ugonjwa huu.
Sasa ni nini tofauti kati ya vifo vinavyotokana na mafua yetu makali ya siku zote, TB, Malaria na vifo vinavyotokana na COVID-19 kwa Afrika, au ni kwakuwa COVID-19 inaua sana huko kwa wakubwa?
Je, Afrika hofu ya flu, TB, Malaria, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa ni ndogo kuliko hofu ya COVID-19?, au ni kwakuwa COVID-19 inaua pia wakubwa?
Je, Afrika tunapaswa kuwa na hofu kubwa ya COVID-19 kuliko ya ile ya flu yetu, TB, Malaria, HIV, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa?
Je, Afrika tunapaswa pia kuiga njia zote zinazotumiwa na wakubwa huko majuu katika kupambana COVID-19?
Je, ni kweli COVID-19 ndilo tatizo letu kubwa la kiafya kuliko matatizo mengine?
Je, Afrika inahitaji zaidi misaada ya haraka ya kupambana na COVID-19 kuliko misaada ya kupambana na flu, TB, Malaria, HIV, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa?
Kuwatafuta wagonjwa wenye CORONA kwa Mwafrika ni sawa na kuwatafuta wagonjwa wenye mafua makali, sio issue kwao na wanaweza hata wenyewe wasijue kama wana CORONA, issue kubwa kwao ni poverty, elimu bora, mikopo ya elimu, riba kubwa za mabenki, afya bora, njaa, ajira, siasa chafu, malaria, TB, Ebola, ukosefu wa bei na masoko ya mazao yao,
Kwangu mimi hii ni "survival of the fittest" haihitaji very special attention, hii kampeni ya sasa ya kunawa mikono na kuepuka misongamano ilipaswa iwe ni kampeni iliyoanzishwa siku nyingi sana zilizopita kuzuia kuenea flu, TB, measles, mamps, Ebola, minyoo ya tumboni, fungus, upele, typhoid na kipindupindu.