Kutafuta wenye CORONA ni sawa na kutafuta wenye mafua makali Afrika

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,271
12,568
Waafrika kusini mwa jangwa la Sahara ni wahanga wakubwa wa umaskini (poverty), magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya hewa kama TB, flu kali kabisa. Magonjwa haya yamezoeleka sana ndani ya jamii hizi lakini hakuna watu wanaoyaundia task forces ili kujua nani ana flu na TB na nani amekufa ili kuwalinda watu wengine wasiambukizwe.

Hali yetu ya mavumbi, misongamano, na kuishi kwenye nyumba zisizokuwa na ventilation ya kutosha inasababisha magonjwa haya yaonekane ya kawaida kwenye jamii ingawa tunashuhudia yakingalimu maisha ya watu wetu kila siku. Ndiyo maana Hata leo hii wananchi na hata watoa huduma za afya wanashindwa kutofautisha kati ya mgonjwa mwenye mafua makali tuliyoyazoea siku zote na mgonywa mwenye Corona wanapokutana nae. Kuna wakati kila unaekutana nae mtaani na hospitali analalamika kuwa amebanwa na mafua makali. Watu huwa wanakambilia kusema kuwa ni mabadiliko tu ya hali ya hewa, msimu wa maua ya maembe, nk ilimradi tu kujustify sababu za outbreak ile ya mafua kwa kila mtu.

Na ndiyo maana hata wagonjwa tunaodhani wana Corona huwa wanapona wenyewe na inawezekana wapo wenye korona majumbani lakini wamepona wenyewe kwa kulamba tu asali, ndimu na tangawizi majumbani.

Watu wetu kwa maelfu huwa pia wanaliwa na Malaria kila siku; watoto, wajawazito na hata watu wazima ambao wanasababisha misululu mirefu hospitalini, wodini, kwenye klinic na hata kwa waganga wa kienyeji kusaka matibabu. Afrika huwa haihangaiki sana na kuunda task forces kujua ni kaya gani wacha tu kuwa na mgojwa wa malaria bali hata aliyekufa kwa malaria.

Kufa kwa Malaria kumezoleka pia kwenye jamii zetu. Tunayo idadi kubwa sana ya watu wetu hawaendi makazini, shuleni, na kwenye shughuli zao mbalimbali kwa sababu ya malaria tu. Nchi zetu zinatumia hela nyingi sana kuhudumia wenye Malaria, lakini hakuna task forces za ugonjwa huu.

Sasa ni nini tofauti kati ya vifo vinavyotokana na mafua yetu makali ya siku zote, TB, Malaria na vifo vinavyotokana na COVID-19 kwa Afrika, au ni kwakuwa COVID-19 inaua sana huko kwa wakubwa?

Je, Afrika hofu ya flu, TB, Malaria, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa ni ndogo kuliko hofu ya COVID-19?, au ni kwakuwa COVID-19 inaua pia wakubwa?

Je, Afrika tunapaswa kuwa na hofu kubwa ya COVID-19 kuliko ya ile ya flu yetu, TB, Malaria, HIV, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa?

Je, Afrika tunapaswa pia kuiga njia zote zinazotumiwa na wakubwa huko majuu katika kupambana COVID-19?

Je, ni kweli COVID-19 ndilo tatizo letu kubwa la kiafya kuliko matatizo mengine?

Je, Afrika inahitaji zaidi misaada ya haraka ya kupambana na COVID-19 kuliko misaada ya kupambana na flu, TB, Malaria, HIV, Ebola, Dengue, ajali za barabarani, na njaa?

Kuwatafuta wagonjwa wenye CORONA kwa Mwafrika ni sawa na kuwatafuta wagonjwa wenye mafua makali, sio issue kwao na wanaweza hata wenyewe wasijue kama wana CORONA, issue kubwa kwao ni poverty, elimu bora, mikopo ya elimu, riba kubwa za mabenki, afya bora, njaa, ajira, siasa chafu, malaria, TB, Ebola, ukosefu wa bei na masoko ya mazao yao,

Kwangu mimi hii ni "survival of the fittest" haihitaji very special attention, hii kampeni ya sasa ya kunawa mikono na kuepuka misongamano ilipaswa iwe ni kampeni iliyoanzishwa siku nyingi sana zilizopita kuzuia kuenea flu, TB, measles, mamps, Ebola, minyoo ya tumboni, fungus, upele, typhoid na kipindupindu.
 
Ndio maana mkuu wetu alisema wazi kua haka kakorona ni ka mafua tu,
Na sisi waafrika mafua hayatupi shida sana kama yanavyowaua wazungu.
Inawezekana mpaka sasa haka kakarona kakawa kameenea zaidi Afrika kuliko hata ulaya ila kwa vile sisi watu weusi miili yetu ni imara yenye kinga madhubuti kutokana na mazingira yetu ndio maana mpaka sasa hivi hatujapata athari kubwa kama wenzetu wazungu.

Maendeleo hayana chama
 
Duh! 🤔
 
"Nafiikiri nimeumwa Corona mara Tatu,na mara zote hizo nimepona niliishia kuweka kitunguu chini ya mto ninapo lala.
Na asubhi kula tembe za vitunguu swaumu"
Aliskika mpita njia akiwasiliana na mtu kwa njia ya simu.
Watanzania wameshagundua tiba ya Corona kabla ya USA tunastairi tuzo
 
"Nafiikiri nimeumwa Corona mara Tatu,na mara zote hizo nimepona niliishia kuweka kitunguu chini ya mto ninapo lala.
Na asubhi kula tembe za vitunguu swaumu"
Aliskika mpita njia akiwasiliana na mtu kwa njia ya simu.
Kama mimi aiseee, nimekula vitunguu maji vya kutosha. Nahisi vitunguu nilivokula na kulalia vinajaza kile kiroba kinachotumika kuvileta sokoni😂😂😂
 
Unajua sijaelewa kwa nini Wafrika tunakataa kwa nini chanjo ya COVID-19 isijaribiwe kwetu huku. Yaani tumekaa kaa tu, watu huko Ulaya wanakesha kutafuta tiba afu wakiomba tutumike kama majaribio sisi tunakataa. Chanjo ikipatikana tunaanza kuomba watusaidie chanjo za bure.......smh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote uliyosema yanawezekana... Ila kila zama na zama zake...

Ni sawa na kue na mlipuko wa kipindupindu, alafu useme haka ni kaugonjwa cha kuhara tu, katapita, waAfrica mbona tushazoea... siyo sawa...

Cc: mahondaw
 
Kama hiyo chanjo haijafikia stage ya kujaribiwa kwa binadamu, wanaiharakisha ili itumike haraka kutokana na wazungu kufa wengi wengi. Hakuna anayeyajuwa madhara na ubora wa chanjo hizi, hivyo wanataka kuwatumia watu Kama guinea pigs kujua ubora na madhara yake.

Bahati mbaya wanatuona waafrika Kama watu tusiokuwa na thamani hata tukipata madhara au kufa kutokana na chanjo hizo. Hawataki kuijaribia kwa watu kamili (wazungu) Kama wanavyojiona wao.

Hivyo waafrika kukataa kujaribiwa sio mbaya ipitie hatua zote za kutengeneza chango au vinginevyo wajaribio kwao wenyewe.

Sisi wanataka tuwe Case na wao wawe Control kwenye utafiti huo, haikubaliki hiyo kimaadili.
 
Yote uliyosema yanawezekana... Ila kila zama na zama zake...

Ni sawa na kue na mlipuko wa kipindupindu, alafu useme haka ni kaugonjwa cha kuhara tu, katapita, waAfrica mbona tushazoea... siyo sawa...

Cc: mahondaw
Sisi huwa tunapigwa sana na magonjwa ya surua, kipindupindu, TB, Malaria, mafua, Ebola, tauni kule Lushoto lakini dunia yote iko kimyaa wakati waafrika wananyukwa na magonjwa haya ya kishenzi ambayo chanzo chake ni umaskini na uchafu, niajabu kuona Sasa hivi Africa inahangaika saaaana kupita kiasi na Corona kuliko inavyohangaika na Malaria, HIV, Ebola, surua, kipindupindu, TB, flu, vifo vya akina mama, na ajali za bodaboda magonjwa yanayozoa maisha yetu kwa mamilioni kila siku. Kisa ni kwakuwa wazungu wanakufa sana huko.
 
Vyombo vya magharibi vinaijuwa kazi yao. Hii na ile Hadith ya King terrible secretary. Kinyozi anayemnyoa mfalme amevujisha Siri kuwa mfalme ana mapembe kichwani ndio maana havui kilemba chake masaa 24 hata akilala na mkewe kitandani.

Dunia haijazoea kusikia wakoloni wanakufa kizembe hivyo, ndio maana dunia
 
Wewe ni mpumbavu mkubwa hujui hayo majaribio yatakuwa na athari gani katika miili ya wataojaribiwa? Au unachukulia hili suala Kama kumeza Panadol na kutulia kungojea upone?
Unajua sijaelewa kwa nini Wafrika tunakataa kwa nini chanjo ya COVID-19 isijaribiwe kwetu huku. Yaani tumekaa kaa tu, watu huko Ulaya wanakesha kutafuta tiba afu wakiomba tutumike kama majaribio sisi tunakataa. Chanjo ikipatikana tunaanza kuomba watusaidie chanjo za bure.......smh

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mpumbavu mkubwa hujui hayo majaribio yatakuwa na athari gani katika miili ya wataojaribiwa? Au unachukulia hili suala Kama kumeza Panadol na kutulia kungojea upone?

Sent using Jamii Forums mobile app
Waafrika tuna shida nyingi sana, tumeaminishwa kuwa wazungu Wana akili sana kupita waafrika, na Wana nia njema mara zote siku zote.

Kama waafrika tungekuwa hatuna akili Kama wazungu akina mbwana samatta na weusi wenzao wasingecheza mpira huko.

Tulichokosa sisi sio akili bali siasa chafu na sera chafu na elimu chafu na mipango michafu baaaasi!

Simpigii debe lakini Afrika ilikosa viongozi Kama Magufuli, ambao ni maskini jeuri
 
Back
Top Bottom