Kutafuta mume/mke kwenye mtandao wa jamii

earl

Senior Member
Joined
Aug 30, 2012
Posts
142
Reaction score
192
Habari za jioni wanaJF. Poleni na majukumu.

Kama maada inavyojieleza hapo juu. Je, ni kwamba sasa hivi lipo kundi la vijana ambao wametingwa na majukumu kiasi kwamba hawana muda kabisa wa kukutana na kujumuika na marika (agemates) wao katika jamii na kuweza kujenga urafiki ambao unapelekea kuwepo kwa mahusiano? Je, phonebook za simu zao zimejaa majina ya watu gani?

Wengi wa vijana hawa wanaotafuta wenza katika mitandao wanakuja na vigezo fulani, elimu, kipato, n.k. Je, huku sio kutafuta hadhi (status) katika jamii na mtafuta mume/mke anakua amesahau kwamba mapenzi ya kweli hayajengwi na vitu hivi? Mapenzi ya kweli yanakuja bila vigezo (unconditional).

Halafu hili la kukutana na mtu ambae ni mgeni kabisa (a complete stranger), na ndani ya muda mfupi anakua mume/mke limekaaje? Mimi nadhani ile hali ya kuwa marafiki, wachumba, halafu mnakua mume na mke ina raha yake. Mnapitia mengi pamoja ambayo yanajenga upendo wenu na yanawajenga kiakili na kisaikolojia kwa hilo ambalo mnaliendea - ndoa na baadae familia.

Kuna mwalimu wangu wa sekondari aliniambia kwamba, "There is no shortcut to maturity" (Hakuna njia ya mkato katika hatua ya ukuaji). Mtu utaishi katika jamii yako inayokuzinguka, utakutana na vijana wa rika lako, ufahamiana nao na yupo ambae utavutiwa nae, na huyo utampenda, atakua rafiki yako, mchumba wako na hatimaye mtaoana.
 
Well said mate............................
 
Attachments

  • FB_IMG_1492574914946.jpg
    FB_IMG_1492574914946.jpg
    48.3 KB · Views: 75
Hayo ni mawazo yko...kila anae tafuta huku mpnz ana maana yke
 
Ukikutana na mtu sokon ukampenda Ni sawa sawa na kumkuta Facebook.jf au insta

Tupo kwenye ulimwengu wa information.....

Mambo yanabadilika, swala la mlikutana wapi halikigarantii kilichobora. Ila swala la umakini tuu.

Mkikutana kwenye mtandao lazima mpite stage kadhaa urafiki,uchumba hata ndoa.

Kibaya Ni kuruka stage.

Muhimu Ni kuwa makini na unachokitafuta na kusimamia unachokiamini.
 
Hii ni moja ya tamaduni tulioiga toka kwa wazungu!!!
Si lazima kila mmoja aikubali.
Watu wanakutana mitandaoni na wanaishi kwa mda mrefu tu...
 
Mie tulikutana mtandaoni, tunatimiza mwaka was 5 mwezi was tisa
 
Ukikutana na mtu sokon ukampenda Ni sawa sawa na kumkuta Facebook.jf au insta

Tupo kwenye ulimwengu wa information.....

Mambo yanabadilika, swala la mlikutana wapi halikigarantii kilichobora. Ila swala la umakini tuu.

Mkikutana kwenye mtandao lazima mpite stage kadhaa urafiki,uchumba hata ndoa.

Kibaya Ni kuruka stage.

Muhimu Ni kuwa makini na unachokitafuta na kusimamia unachokiamini.
Kwel kabisa chief
 
Natafuta mpenzi wa kike wa kuchati.
Umri wowote.
Dini yoyote.
Rangi yoyote.
Elimu yoyote.
Kazi yoyote.
Ila awe msiri.
SMS zote zitajibiwa...

Kwa aliyeko serious anitafute kwa namba 07651765

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji115][emoji115][emoji115]
 
Internet imerahisisha maisha, angalia mifano hii hapa chini:-

1. Sihitaji kusafiri kwenda nchi za nje kununua bidhaa, unafanya online kila kitu mpaka mzigo unafika.

2. Nikitaka kujua bei ya hotel, au kama vyumba vipo sihitaji kufunga safari kuuliza, naingia mtandaoni nachagua hotel nayotaka nalipa, siku nikifika ni kulala tu.

3. Sihitaji kwenda airport au stendi kukata ticketi, namaliza online.

4. Kipindi cha nyuma kujuliana hali ni mpaka muonane, siku hizi kuna group whatsapp makundi ya marafiki, familia, workmates nk, kila mara mnajuliana hali.

5. Sihitaji kwenda Kona Bar, Kwa Wahaya, Kimboka kupata malaya, naingia kwenye mtandao tu nachagua ninayemtaka tunawasiliana, tunakutana hotelini.

Same same kwenye kutafuta mke, unaweza kutumia mtandao huu huu na ukapata mke/mme bora kabisa, maana sisi hawa hawa tulioko kwenye mitandao ndo tulioko nje.

Kazi ni Kwako.
 
2017 - 12 = 2005, hii itakuwa Marafiki.com au ulisoma nje mkakutana kwenye mitandao ya nje.

Otherwise punguza miaka mkuu.
Nipunguze kwa nini wkt kweli? Yes 2005 hujakosea na haikuwa marafiki .com.
 
Back
Top Bottom