UKAWA kwa kutoka nje ya Bunge Maalumu la Katiba (BMK), walikuwa sahihi kabisa kwa sababu:-
1: Kwa vile CCm ilikuwa imekwisha fanya lobbying kwa wajumbe wengi wa 201, hivyo matakwa yao yangepita tu!
2: Kushiriki mpaka mwisho huku mkiwa mnaburuzwa kwa wingi wa CCm, ilikuwa ni sawa na kubariki matakwa ya CCm.
3: Hata kama waliokuwa wanataka Rasimu ya Tume ndiyo ijadiliwe kwa kutoa hoja zenye mashiko (Nguvu ya Hoja), CCm wangetumia wingi wao na nguvu ya pesa kupisitisha wanachokita.
4: Kawaida Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa ilitakiwa ijadiliwe na mwisho wa mchakato wote CCm wangeenda kuipinga kwa wananchi na si kuigeuza na kuleta ya kwao-Huu utaratibu haupo popote duniani.
5: UKAWA wakagundua yote hayo na wakaamua kuwapisha CCm wapitishe wanachokitaka bila wao kuwa sehemu ya maamuzi hayo.