Kususia Mchakato wa Katiba ni Kama Kumsusia Mlevi Pombe-Prof Kabudi

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
Kauli hii aliizungumza juzi pale LHRC wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kituo hicho na kusema we should not shun from problems rathe challenges them

Hii kauli inahitaji tafaluri tunduizi jamani
 
UKAWA kwa kutoka nje ya Bunge Maalumu la Katiba (BMK), walikuwa sahihi kabisa kwa sababu:-
1: Kwa vile CCm ilikuwa imekwisha fanya lobbying kwa wajumbe wengi wa 201, hivyo matakwa yao yangepita tu!
2: Kushiriki mpaka mwisho huku mkiwa mnaburuzwa kwa wingi wa CCm, ilikuwa ni sawa na kubariki matakwa ya CCm.
3: Hata kama waliokuwa wanataka Rasimu ya Tume ndiyo ijadiliwe kwa kutoa hoja zenye mashiko (Nguvu ya Hoja), CCm wangetumia wingi wao na nguvu ya pesa kupisitisha wanachokita.
4: Kawaida Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa ilitakiwa ijadiliwe na mwisho wa mchakato wote CCm wangeenda kuipinga kwa wananchi na si kuigeuza na kuleta ya kwao-Huu utaratibu haupo popote duniani.
5: UKAWA wakagundua yote hayo na wakaamua kuwapisha CCm wapitishe wanachokitaka bila wao kuwa sehemu ya maamuzi hayo.
 
umejenga hoja

Kwa ufupi ukisha badili sura ya kwanza na sita, basi huko mbele hutakuwa na nafasi ya kujadili serekali tatu na badala yake utakuwa ukijadili maboresho ya serekali mbili.
 
Kwani UKAWA wamesusia mchakato wa katiba au wamesusia BMK?! Kama wamesusia mchakato wa katiba mbona wapo kwa wananchi wakitoa ELIMU ya kuikataa rasimu itakayoletwa na CCM kama haitakuwa na maoni ya wananchi.
 
kwa ufupi ukisha badili sura ya kwanza na sita, basi huko mbele hutakuwa na nafasi ya kujadili serekali tatu na badala yake utakuwa ukijadili maboresho ya serekali mbili.

maana yake hata mchakato wenyewe niubatili na kujilisha upepo
 
kwani ukawa wamesusia mchakato wa katiba au wamesusia bmk?! Kama wamesusia mchakato wa katiba mbona wapo kwa wananchi wakitoa elimu ya kuikataa rasimu itakayoletwa na ccm kama haitakuwa na maoni ya wananchi.

basi tuseme kususia bmk, bado hoja inabaki palepale kwani lila na fila havitangamani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom