Kusudi la barua hii!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusudi la barua hii!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anyisile Obheli, Oct 26, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nawapenda sana nyote, na upendo wangu kwenu utazidi sana mkitumia busara na hekima kumpeleka Dr Slaa ikulu ili kuiongoza nchi hii na kuisaidia kiMaendeleo na kujenga utu wa Mtanzania wenye heshima
  [​IMG].!!!!
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  chademaaaaaaaa................
  People's................
   
 3. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Utu ni taasisi pana! Taasisi ambayo ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya mtu na jamii yake.

  Alikuwa JK Nyerere peke yake alikuwa anasubutu Kuusemea Utu na kuuweka kama kigezo cha ustawi wa Taifa!

  Bila Utu, ambao ndiyo asili ya Mtu, maedeleo yote hayana maana yoyote! Yanakuwa ni maendeleo ya vitu! Ni utu kwanza...

  Utu ni Uungu ndani mtu, hatuwezi kuusaliti... lazima utu kutangulia kila nyanja ya jamii bila hivyo hicho kinachoitwa ustawi na maendeleo haina maana.

  Maendeleo ya Utu ndio yatawale maendeleo na ustawi wa jamii na taifa, na si maendeleo ya vitu bila kuujali na kuujenga na kuendeleza utu wake kwanza..

  Utu unanyaushwa, kuharibiwa na kuangamizwa na UFISADI!

  Utu unarutubishwa na haki, upendo, maadili ya uongozi, kuheshimiana na usawa wa pato la taifa, matumaini na upendo!

  Ni hakika CCM na Kikwete wameutupilia mabali Utu ulioasili ya Mtu! Mengine yote yanafuatia hapo ni Mgawanyiko na Mtabaka kwa Taifa. Mgawanyiko na mtabaka hayo vinazaa Udini, ukabila, kuimarisha, ujinga, dhuluma, maradhi nk. Kisa Utu umewekwa kando, tumeisaliti asili yetu. Na kama utu haupo ...ina maana tuna kinyume cha utu...ambacho ni unyama ndani ya Mtu... Na usiombe kuishi ndani ya jamii au Taifa kama hilo!
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Chadema juuu
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  dah mkuu umemaliza kabisa,
   
 6. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Dr. SLAA kama alivyokuwa Nyerere amesisitiza juu ya UONGOZI BORA lakini Kikwete amesisitiza juu ya UTAWALA BORA. Ki nadharia na kiutendaji hivi ni vitu viwili tofauti vilivyo pishana kwa mapana na marefu, tena ni vitu vyenye impact kubwa katika dhana ile ya mabadiliko na ukombozi wa Mtanzania kutoka katika janga la Umasikini, Maradhi na Ujinga.

  UONGOZI BORA
  Katika hili ipo nia ya dhati ya kuwashirikisha wananchi juu ya mambo muhimu, ambayo wangependa yatendeke kwa manufaa ya wote. Hapa tunapata ushirikishwaji wa moja kwa moja wa wananchi kupitia mtu moja aliyepewa dhama ya kusimama kwa niaba ya watanzania wote. Unapokuwa KIONGOZI BORA wewe ni sehemu ya jamii husika hivyo kila unachokifanya kiwe kibaya au kizuri wewe unakuwa mmoja ya wale, aidha watakao sikia maumivu ama watakao sikia furaha kulingana na matokeo ya kazi husika. Hivyo basi na ungana na Dr. SLAA na Mwl Nyerere juu ya ukweli kwamba tanzania tunahitaji UONGOZI BORA kuliko UTAWALA BORA, Maana kupitia uongozi bora tunaweza kutoka hapa tulipo na kufika kule tunakohitaji.

  UTAWALA BORA
  Mtawala ni mtu aliye juu ya mtu mwingine, kisheria, kiuchumi, kinguvu/kimabavu hata Kisauti na kimaamuzi. Huyu huweza kufanya lolote wakati wowote bila kujali athari wala maumivu yatakayotokana na jambo alilolifanya. Utawala Bora upo pale ambapo Mtawala husika anapopata kile anachokihitaji kwa usahihi. Katika hili tunaona kwamba ushirikishwaji wa matakwa ya wananchi haupo kabisa, badala yake unakuwepo utimilifu wa matakwa ya mtawala. Mfano mzuri ni wakati ule wa ukoloni, pale tuliona UTAWALA, hata katika vitabu vyote vilivyoandika juu ya masuala ya ukoloni na kikoloni vilitumia sana neno UTAWALA maana kila kilichofanyika kilifanyika kwa manufaaa ya upande mmoja yaani Ukoloni na si kwa manufaa ya taifa wala wananchi husika. Hivyo basi wananchi hatuwezi kufaidika kwa kutawaliwa bali tutafaidika kwa kuongozwa.

  Kwa takribani miaka mitano sasa tangu tanzania tuwe chini ya Utawala wa Kikwete, tumeshuhudia mporomoko wa uchumi, Kushuka kwa ELIMU kwa kiwango cha kutisha, Kudidimia kwa maisha na pato la mtanzania wa kawaida. Lakini pia tumeshuhudi utajiri wa kutisha hasa kwa wale walio katika utawala, hili linawagusa Mawaziri, Makatibu wa wizara, Wafanya biashara hasa wanaounga mkono Utawala huu dhalimu. Imefika wakati sasa Watanzania tuamke. Tunataka kiongozi atakaye tuongoza kuelekea kule tunakokutaka na wala hatutaki mtawala au watawala watakaye tawala mali na haki zetu kwa jinsi wanavyotaka wao. Hii ni kweli tena itabakia kuwa kweli mtupu. Ndi maana Anyisile Obheli ametumia neno KUIONGOZA NCHI HII....... na sio KUITAWALA NCHI HII.....

  Thank you
   
Loading...