Kusoma UDSM ni dhamana

Kusoma UDSM ni dhamana

kiukweli udsm ni patamu sana..hata mtu utoke na gpa ya 2 utalamba shavu tu.
 
Sijasoma content, maana heading tu ni pure arrogance, sasa ulitaka watu wakasome kozi kama Architecture na udaktari UDSM? Fala kweli we jamaa.., vilaza kibao toka UDSM tunawabebesha mafaili huku kitaa, mjinga sana wewe, tena futa liuzi lako.., stupid
 
Joka leo mzee baba kati ya siku zote umeandika ugoro kwa mara ya kwanza. Unaweza ukawa na sababu zako, ila kwa kuwa na wewe umesoma UDSM usitake kupitisha kauli hii kuwa sahihi mzee dingi umechemka hapa.

Ni viongozi wangapi wa nchi wenye nyadhifa kubwa ambao wamesoma hapo lakini ni wasomi uchwara tena wachumia matumbo?

Mimi nadhani kwenye mustakabali wa nchi na maendeleo kiujumla kipaumbele hakipaswi kuangalia eti mtu amesoma wapi. Tuangalie huyu mtu anajua nini na anaweza kuleta jipya gani.

UDSM wasomi uchwara kibao tu tumejazana humu mitaani.
 
Kusoma UDSM halafu unakaa miaka 4 huna ajira na wenzako wamesoma SAUT na wameajiriwa mwaka mmoja toka wamalize kipi bora? Ikiwa mlimaliza pamoja?

Kuna mmoja kamaliza hapo alikua sifa kibao kisa UDSM mwaka wa nne sasa yupo nyumbani.
 
Kwenye swala la ajira inategemea ni wapi, nenda viwandani huko ukajionee wahitumu na mainjinia wa Arusha tech aka. ATC, DIT na MUST walivyotawala anga na huwezi waskia wakijitapa kuhusu vyuo walivyotok utawatambua kwa kazi zao.

Kuhusu UDSM nakiheshimu sana hiki chuo maana ni chuo mama hapa nchini ila kinachoniskitisha ni viongozi wengi waliolitumbikiza taifa kwenye dimbwi la rushwa na ufisadi ni wahitimu wa hiki chuo chetu bora sasa sijui kwa upande wa maadili na uzalendo UDSM wamekaaje maana elumu bora bila maadili na uzalendo haiwezi kulikumboa taifa.
 
Back
Top Bottom