Kama unapata elimu na haikuwezeshi kuwa na fedha bado elimu haijakusaidia. Watu wengi wamesoma sana ila wanafeli kuzitumia elimu zao kuyamudu mazingira ili wapate mahitaji muhimu.
Actually waafrika wengi hawajui kwanini wanasoma au naweza sema kwamba asilimia kubwa ya africans wanasoma ili wapate ajira then wapate pesa hakuna kingine zaidi ya hapo.
So hapo ukiangalia kwa makini utakutana na ubinafsi pia umasikini.
Na mpaka hapo inamaanisha mtu huyo hajitambui.
Utakuta mtu ni amesomea physics.
Amesoma physics ili akaajiriwe means akikosa kuajiriwa basi atakufa masikini.
Na ukiangalia kwa makini kwenye jamii na mazingira yetu kuna vitu vingi vinavyohitaji utatuzi kwa kutumia hiyo physics.
Sasa kama mtu huyo angejua kwanini amesoma, angekuwa sio mbinafsi na asingekuwa na tamaa ya pesa za faster.
Basi lazima angeitumia elimu yake kutatua changamoto za jamii na mazingira na ukishatatua changamoto lazima faida irudi ambayo ni pesa.
Bty huwezi kutatua changamoto yoyote kubwa bila kuwa na pesa ya kutosha considering wewe ni masikini.
Na ukiangalia kwa makini wasomi wetu wengi hawawezi kuanzia chini sababu hawajitambui wanategema kupop-up na utajiri kama Facebook ads.
Well hapo ukikosa ajira basi unakufa masikini na vyeti vyako kabatini panya wakivifanya dinner.
Kuna vyanzo vingi vinavyofanya wasomi wa kiafrika wafe masikini ila nikianza kuandika sitomaliza sababu kila chanzo kinazalisha chanzo kingine.
Ila solution ni kufundisha wanafunzi kuhusu kutatua changamoto zinazotuzunguka kwa kutumia elimu means hapo ni kuchange education system yote.
Pretty sure that's not gonna happen considering walimu wenyewe nao walisoma ili waajiriwe wapate pesa.
Matokeo yake serikali haiwezi kuajiri kila mtu na hao wasomi kufa masikini na kuwa mzigo kwa taifa.