Kusoma na biashara kipi bora?

Fanya biashara tu mkuu Canada utakayoipata ndio usomee kwa badae ili kuongeza maarfa ila usisome ukategemea ajira itakula kwako wenzako yupo tu kutwa kwenye mbao za matangazo kuangalia ajira.
 
Umenichekesha sna sijawah kusikia neno "Unazi" ndo nimesikia kwako, hapa nspata mawazo kwa walionitangulia kwaiyo akili kichwan mwangu mkuu.
Barikiwa sna mkuu
 
bora ni kufanikiwa sasa utajua wewe ni wapi upande wako kufanikiwa kama ni biashara ndo unaona njia sahihi fanya kama ni kitabu piga kitabu hakuna limitation in ways of successful
 
Nionavyo mm, hana maana ya kusoma ili niajiliwe ila anataka niwe na ufaham zaidi, endapo itatokea case yoyote niweze kuisimamia vzr. Maana watu wanaajiliwa ili wapate pesa ila kwangu pesa sio tatizo, tatizo niwe na ueleawa mpana wa kun'gamua mambo.

Kumbe tayari jibu unalo....kasome hachana na hayo mambo ya bihashara....hakuna kitu kinaleta heshima duniani kama una Elimu na una pesa....Mwangalie jabari wangu Makonda level alifikia ata kama alifeli angeenda shule kwa jina lilelile hakuna ata mmoja ambaye amgemtetelesha Dar hii.....shortcut sio nzuri rudi scur.
 
Hapo kuna ukakasi, mara kozi uliyopiga ni ngumu kupata ajira kwa level yako, inabidi usomee kitu kingine.
Halafu unasema unataka usome ili uelimike upate kuyakabili maisha na changamoto zake mbeleni na si kuajiriwa.
Kwanini hujaendelea degree kwa kozi hiyohiyo na badala yake wataka kuanza kutambaa tena?
Lengo hapa kwamba usome upate ajira, sema tu kuwa ulikataa vijembe humu ndani ukisema kuwa wataka kuajiriwa.
 
Elimu ni investment kubwa sana iwapo utasoma na kuelimika. Hata hivyo iwapo utarudi shule kusoma ili upate cheti kitakachokusaidia kuppata ajira, inabidi ujiulize mara mbili kwa sababu kupata ajira kunategemea factors nyingine nyingi sana zaidi ya cheti. Ingawa sijui ulisomea nini, ninadhani kuwa elimu uliyonayo ina opportunities nyingi sana zaidi ya ajira. Fanya tathmini inayoitwa SWOT halafu ukatumia strengths zako kwa kila opportunity itakoyotokea bila kuchelewa utafanikiwa sana na kuwa financially independent.
 
Mimi ninavyoona bora urudi kusoma, ninaamini biashara nyingi hapa nchini anaweza kufanya mtu yoyote ilimradi tu ajue kusoma nakuandika haijarishi unataaluma ama huna, endapo tu utakuwa namtaji, ila taaluma yamtu haiwez kuingiliwa namtu ambaye ajaisomea kwahiyo mimi ninachoona ukiwa naelimu naukawaweza kufanya biashara unakuwa unavitu viwili kichwani chakwanza niuwezo wakufanya biashara nachapili unakuwa nataaluma fulani kuliko huyu ambaye anafanya tu biashara bila kuwa nakitu kingine chaziada kichwani, kwahiyo me nakushaur soma ili uwe navitu vyaziada kichwani
 
"ishike elimu usiiache iende zake" mkuu hakumaanisha hii elimu ya kukariri maandishi, ila ni elimu dunia na kiroho kwa level yake bora afanye biashara, kusoma anaenda kupoteza muda tu
 
Mkuu elimu inayozungumzwa pale umewahi kuijua? Hivi tunaacha kupeana maarifa halisi juu ya maisha ya kweli ya mwanadamu tunakomazana kuhusu pythagoras theorem? Hiv pythagoras mwenyew alikuwa na elimu yetu hii ya kiwango gani? Vip Galileo Galilei tuache kupotezeana muda na hizi taka taka tunazoziita elimu eti hapo zamani ulikuwa nyani ili usikoseshwe na mwalimu sema ndio daaaah My dear Africa una safar ndefu ya kwenda.
Back to the point endeleza biashara mlizonazo usifungue nyingne wala usiende chuo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…