The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,105
Sheria mpya ya madini ya Prof. Kabudi ni kaburi la sekta ya madini. Hakuna atakayefanya uchimbaji wa madini ya Tanzania.
GGM wameomba mazungumzo na serikali. Wasipokubaliana, bila shaka watafuata njia hiyo hiyo ua Acacia
Waliokuwa wanajenga mgodi wa graphite Mtwara, wamefunga.
Waliokuwa wanataka kuanza kuchimba gas, wamefunga na kwenda Mozambique. Tumepoteza uwekezaji wa dola bilioni 30.
Makampuni ya nje yaliyokuwa yanafanya utafiti wa madini mbalimbali, yote yamefunga. Mengine yameondoka kabisa, machache yamesimamisha tafiti na kubakiza watendaji wachache sana kwenye ofisi zao kwaajili ya kusimamia taratibu za kufunga kampuni.
Ile sheria ya Prof. Kabudi haipo mahali popote Duniani. Kuamini kuwa sisi ndiyo wajanja kuwazidi wote, huenda sisi ndiyo tukawa wajinga kuliko wote.
Umesahau Dangote