Barrick Buzwagi yakabidhi vituo 2 vya Raslimali Kilimo kwa Serikali mkoani Shinyanga

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
153
111


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme (kulia) akipokea nyaraka za umiliki na funguo za trekta kutoka kwa meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi,Rebecca Stephen katika hafla ya mgodi huo kukabidhi vituo viwili viwili vya raslimali kilimo (Agricultural Resources Centres) vya mwendakulima na Mondo kwa Serikali iliyofanyika wilayani Kahama.Katikati mwenye miwani ni Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme (kulia) akionyesha nyaraka za umiliki na funguo za trekta baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Rebecca Stephen (kushoto) katika hafla ya mgodi huo kukabidhi vituo viwili viwili vya raslimali kilimo vya mwendakulima na Mondo kwa Serikali iliyofanyika wilayani Kahama.Katikati mwenye miwani ni Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme (kushoto) na ujumbe wake, wakipata maelezo kuhusu uendeshaji wa kituo cha Mwendakulima.

Wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, na Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido (wa kwanza kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na Wafanyakazi waandamizi wa Barrick..

Moja ya nyumba kitalu katika vituo hivyo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, amewataka wakulima na wafugaji wilayani Kahama, kuchangamkia fursa ya kupata mafunzo ya kuendesha shughuli zao kwenye vituo vya mafunzo ya kilimo na ufugaji ((Agricultural Resources Centres) vilivyojengwa na Barrick Buzwagi, katika eneo lao ili waweze kujikwamua kimaisha.

Mndeme, alitoa wito huo jana wakati wa hafla ya kupokea vituo viwili vya uwezeshaji Wananchi katika sekta ya kilimo na ufugaji vilivyojengwa katika kata ya Mwendakulima na Mondo, kwa Ufadhili wa Mgodi wa Barrick –Buzwagi.

Alisema vituo hivi vitawawezesha wakulima kuachana na kilimo na ufugaji wa kujikimu na badala yake watalima kilimo cha kisasa na ufugaji wenye tija huku vituo hivyo vitakuwa kitovu cha upatikanaji wa maarifa kwaajili ya kilimo na ufugaji.

’’Napenda kuchukua fursa hii kutoa pongezi na shukrani kwa Mgodi wa Barrick Buzwagi, kwa kujenga vituo hivi ambavyo vikitumika ipasavyo vitaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo na ufugaji ambapo Wananchi watapata maarifa ya kuendesha kilimo cha kisasa na ufugaji wenye tija huku vituo hivyo vitakuwa kitovu cha upatikanaji wa maarifa kwa ajili ya kilimo na ufugaji.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Rebecca Stephen, alisema kazi zilizokamilika katika vituo hivyo ni ujenzi wa majengo ya darasa,majengo ya usindikaji ,kitalu kimoja kila kituo ,kaushio la mazao ,duka la pembejeo ,Ununuzi wa mashine za kusindikia Mpunga na Alizeti ,trekta moja kila kituo na zana rahisi kila kituo Ambapo kwa vituo vyote viwili vimegharimu shilingi milioni 976.5.

Aidha Amesema tangu vituo hivi vianze kufanya kazi mafanikio mbalimbali yamepatikana ikiwa ni kuongezeka kwa mavuno ya mahindi kutoka tani 1.5 hadi tani 3.0 ,mpunga kutoka tani 2.0 hadi tani 3.0 huku kaya 4,648 zimepatiwa mafunzo ya kilimo bora kupitia mashamba darasa ya mahindi, alizeti, mpunga na mbogamboga.

Baadhi ya wakulima waliohudhuria hafla hiyo walishukuru Mgodi wa Barrick Buzwagi kwa kufungua vituo hivyo vya kuwajengea uwezo kwa kupata maarifa ya kuendesha shughuli zao za kilimo ,samnamba na kuwakabidhi miradi ya kujikwamua kimaisha.

Mgodi wa Barrick Buzwagi, ambao uko katika mchakato wa kufungwa umebuni miradi mbalimbali endelevu ya kuwawezesha wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo kuendelea kujipatia mapato kwa lengo la kujikwamua kimaisha na kuboresha maisha yao.
 
Back
Top Bottom