Kusitishwa kwa huduma za kifedha na kibenki toka Falme za Kiarabu kuja Tanzania

njomloli

Member
Oct 23, 2010
67
33
Habari za mchana ndugu zangu,

Jana kumekuwa na shida kuanzia saa nane mchana saa za Dubai/UAE kuhusu kutuma pesa Tanzania kwa njia zote: Western Union, Mpesa, Instant Cash, na bank transfers.

Mashirika haya yanadai kumekuwa na memo toka Central Bank ya Tanzania kuhusu utumwaji wa pesa Tanzania until further notice. Je, kuna mwenye habari kuhusu jambo hili? Na ni nini hasa kinaendelea? Watu wetu wanasumbuliwa. Mwenye uelewa wa jambo hili atueleze ama kutufikishia ujumbe tafadhali.
 
hivi inawezekana kutumiwa pesa m pesa kutoka nje,mfani US, natanguliza shukrani
Kwa nchi za wenzetu nyingi tu inaeezekana sababu wameruhusu matumizi ya PayPal kupokea pesa .Sisi nchini kwetu serikali inaruhusu tu PayPal kutumika kwa kulipia nje sijui ni kwa sababu sisi tuna mipesa mingi ya kigeni kwa hiyo hatuhitaji kupokea ? Sielewi.Wangeruhusu PayPal kupokelea pesa unakuwa na uwezo wa kutumiwa pesa moja kwa moja kwenye simu yako au akaunti yako.

Kwa Sasa Mpesa yetu uwezo wake ni wa kupokea pesa za Kenya tu toka kenya
 
Hongera serikili ya awamu ya 5,hii itatufikisha Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.
 
hivi inawezekana kutumiwa pesa m pesa kutoka nje,mfani US, natanguliza shukrani
Ndiyo inawezekana. Tigo pesa, Airtel money, Mpesa, na Ezypesa. Unatumia website ya kampuni ya kutuma fedha inayoitwa Worldremit. Pia wana application ya simu. Fedha zinaingia direct kwenye Mpesa nk dakika hiyo hiyo. Unaweza hata kumnunulia mtu aliyepo Tanzania salio (muda wa maongezi) kwenye simu yake.
 
Back
Top Bottom