Kusingekuwa na magari ya mitumba (used cars)...

ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
43,604
89,931
Uzuri dunia hii lazima second hand ziwepo, kwa vile wapo wanaotumia vitu kwa mda mfupi na wakihitaji vipya basi huuza vya zamani na kununua latest.

Kwa mfano hizi babywalkers;
Toyota Passo toleo la 2017 mpya ni $14,000 kwa 2WD na $16,000 kwa 4WD.
Toyota Vitz model ya 2017 inaanzia $15,000 hadi $19,000
IST ambayo ni uniform kwenye mji kama Dar, toleo la 2017 ni $24,000.

Gari kama Rav4 ni gari inayotumiwa sana na watanzania, model ya 2017 bila $26,000 hadi $29,000 bado hujaikamata.

Zote hizo ni FOB, bado hujalisafirisha na kupigwa ushuru wa hapo bandarini, kweli wengi waliopo barabarani leo wangekuwa watazamaji tu. Leo hii gari unauzwa FOB $350 au/hata chini ya $100, damn asante mtumba.

Hakika bila mitumba tungepata shida sana, hata hizo nguo inabidi waendelee kuwaruhusu watanzania wanunue mitumba tu, bado sisi ni taifa lenye masikini wengi.
 
Car loan/finance ingeshika hatamu. Hivi unajua unaweza kukopa gari mpya na kulipa from $700? Nenda CMC au CFAO kaulize tena hizo ni high end motors.
Kwa small cars kama Vitz ingekuwa from $100 hivi. Nchi nyingi zilizoendelea wanaendesha brand new cars kwa utaratibu huu.
 
Serikali ipige marufuku ya magari ya mitumba ili tuheshimiane Muraa.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Car loan/finance ingeshika hatamu. Hivi unajua unaweza kukopa gari mpya na kulipa from $700? Nenda CMC au CFAO kaulize tena hizo ni high end motors.
Kwa small cars kama Vitz ingekuwa from $100 hivi. Nchi nyingi zilizoendelea wanaendesha brand new cars kwa utaratibu huu.
Tatizo wabongo uaminifu.......
 
Car loan/finance ingeshika hatamu. Hivi unajua unaweza kukopa gari mpya na kulipa from $700? Nenda CMC au CFAO kaulize tena hizo ni high end motors.
Kwa small cars kama Vitz ingekuwa from $100 hivi. Nchi nyingi zilizoendelea wanaendesha brand new cars kwa utaratibu huu.
Kwa nchi za kiafrika ambazo nyingi uchumi wa mtu mmoja mmoja haueleweki, ajira za mikataba ni chache, ni ngumu sana kufanya implementation ya hicho unachosema.

Nadhani AT&T, VERIZON etc wanakopesha simu kwa malipo kidogo kidogo, kwa nini tigo, voda wanashindwa/hawafanyi hivyo.

Hilo linawezekana kwa nchi zenye mfumo mzuri wa ajira na records.
 
Hao hao wachache wenye ajira/kipato cha kueleweka watafaidika na hio na kutatokea small companies zitakopesha wengine. Huu ni mkopo kama mkopo mwingine wowote.
Hata nchi zilizoendekea bila finance wengi wasingeendesha brand new cars or buying a house.
Mtu analipa kodi ya nyumba 750k mpaka 1m anashinndwa ku-finance gari ya $20,000 au nyumba ya 50m ?
 
Wakipiga marufuku magari 10yrs ++(yaani gari za kuanzia 2007-2017 ziruhusiwe), gari za 2006-- zipigwe ban wengi tunaendesha maguta.
Kujiendekeza mtu. Mtu ananunnua used car 50-80m atashindwa brand new car ya $30,000?
 
Hao hao wachache wenye ajira/kipato cha kueleweka watafaidika na hio na kutatokea small companies zitakopesha wengine. Huu ni mkopo kama mkopo mwingine wowote.
Hata nchi zilizoendekea bila finance wengi wasingeendesha brand new cars or buying a house.
Mtu analipa kodi ya nyumba 750k mpaka 1m anashinndwa ku-finance gari ya $20,000 au nyumba ya 50m ?
Ndio maana nikasema, wengi tusingeendesha hayo magari. Imagine mtu anajichanga hadi afikishe 10m ili anunue vitz FOB $500, hata akipata opportunities za loan hawezi kulipa mkopo wa gari yenye FOB $16,000. Itamchukua huyo mtu miaka mingapi kumaliza huo mkopo?
 
Back
Top Bottom