Kusimamishwa kazi kupisha uchungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusimamishwa kazi kupisha uchungu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Lutala, Mar 28, 2012.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa wale wanaojua sheria za kazi. Mimi ni mtumishi katika moja ya kampuni binafsi jijini Dar. Mwezi ulopita nilimjibu vibaya bosi wangu wa kitengo (idara). Siku saba baadaye akaniandikia barua ya kutaka nitoe maelezo kwanini nilimjibu vibaya. Wakati nipokea barua hiyo yaani ndani ya masaa matatu nilipata barua kutoka kwa mkurugenzi kunifahamisha kuwa nimesimamishwa kazi kupisha uchungu. Kinachonisikitisjha ni kuwa hata sijajibu barua ya kutoa maelezo sehemu ya hukumu ishapitishwa.

  Kwa wale manojua sheria za kazi hivi kweli haki imetendeka katika suala langu? Ni taratibu gani nifuate kujupata mustakabali wa suala langu?

  Naombeni msaada wenu wadau
   
 2. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Jamani mbona kimya?
   
 3. k

  kibebii Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  usijali wataalamu wanakuja, ila kwa kuanzia tu, inawezekana sana (kwa maelezo yako) utaratibu haujafuatwa, ila tazama human resource manual yenu, au kanuni za maadili ya kazi na adhabu zake, je ulimtolea mbovu wapi nayo ina nafasi yake, mbele za wafanyakazi wengine au.. ila usiwe na shaka kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi haina shida kama una uhakika huna tabia ya kutoa lugha chafu, kama umeshatukana wengine na ukapata onyo, jipange, kama kuna taaasisi ya wafanya kazi pia waweza washirikisha/ kuwapa taarifa. wanakuja
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  "Kupisha Uchungu" mhh tena umerudia mara mbili
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kosa lako linaitwa "INSURBODINATION" yaani kumdharau kiongozi wako. Kama umefikia hatua ya kumtukana kiongozi wako, wewe tafuta tuu kazi nyingine maana huwezi kufanya kazi na mtu ambaye humuheshimu.

  Kwa kusimamishwa kazi utaendelea kupata nusu mshahara na pindi ukirudi utapangiwa kazi nyingine kama korokoroni ili uwe na adabu kwa viongozi wako sehemu za kazi
   
 6. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Unajua tatizo bosi wangu huyo ni ilaza. Mimi nafanya kazi kama punda halafu yeye anataka kila nikifanya na yeye apate posho. Kwa kweli kwa kitendo hiki nikaona nimtolee uvuvi kwa kumwambia anatakiwa ana yeye afanye kazi ili kupata posho. Ndo hapo akasema nimemtusi
   
 7. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Ndachuwa unajua huyu jamaa amenichosha kwa dharau na kutaka mimi nimfanyie kazi kama punda wake. Yeye kazi yake ni kuvuta posho tu tena zaidi yangu kwa kazi ninayofanya mimi. Ndo maana nikaamua kumtolea mbovu. Aliyenisikitisha ni Mkurugenzi kunipiga benchi hata bila kusubiri maelezo ya barua yangu ambayo yanatakiwa yatolewa ndani ya siku 7.

   
 8. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Shapu unajua mwenzio nimechanganyikiwa. Yaani kukaa nyumbani tu noma. Nashukuru kwa kunisahihisha

   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Hyo barua ya kusimamishwa kazi kwa manufaa ya umma au kwa kumjibu vibaya boss wako?
   
 10. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa kumjibu vibaya boss wangu
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kosa la kujibizana na kiongozi wako vibaya ni Misconduct, hata kukataa alternative work given by your employer is a misconduct, which is a gross insurbodination.
  But the issue is not about the scale of misconduct, bali mtoa mada anataka kujua kama hatua zilifuatwa katika kusimamishwa kwake!

  Kwa kukusaidia kuelewa kama taratibu zilifuatwa ni hivi:
  Once ulipojibizana na bosi wako ama ulimtukana, bosi wako alitakiwa afuate taratibu za kuwajibishwa kwako. Jambo la kwanza ulitakiwa upewe barua ya wito wa mashauri (Disciplinary Hearing). Hapo ndipo utakapohojiwa na kamati kujua sababu za kufanya kosa, na ku determine aina ya adhabu stahiki kama ilithibitika kuwa ni kweli ulifanya kosa.
  Katika hatua hizo, kamati itakupa outcome of the hearing, ikonyesha maamuzi yaliyofikiwa na kamati ya nidhamu.
  Utakuwa na siku tano ya kukata rufaa ambayo itaanza kuhesabika tangu ulipopokea outcome ya DHC.

  Hata hivyo itategemea pia na Mkataba wako wa ajira una conditions za namna gani. Kwani kuna baadhi ya waajiri huingia mkataba na waajiriwa kukiwa na kanuni kandamizi, mfano kuna kuwa na kanuni labda inaelezea kuwa ukimjibu vibaya bosi wako adhabu yake ni kufukuzwa kazi bila kusikilizwa, na wewe unasaini tu haraka haraka kwakuwa unataka kazi.
   
 12. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tulia uchunguzi huo ufanyike obviously baada kukamilisha uchunguzi wao watakuita kwenye ''hearing'' ambako utapewa nafasi ya kujieleza na kujitetea then utapewa uhamuzi utakao kuwa umefikiwa kama ni termination au kuendelea na kazi yako, kinyume hapo hutakuwa hujatendewa haki kwa kutokusikilizwa, therefore itabidi ufike ofisi za CMA au Idara ya Kazi kwa ufafanuzi zaidi.
   
 13. A

  Awo JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hakuna tena kusimamishwa kwa nusu mshahara. Sheria inasema mfanyakazi atasimamishwa on a full pay. Kwa hiyo wakati umesimamishwa unatakiwa ulipwe kama vile uko kazini.
   
 14. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  pole ndugu yangu.
   
 15. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  sheria ya sasa ukisimamishwa kazi unalipwa full salary. Hakuna tena cha nusu mshaharar
   
 16. n

  nyariamani Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusaidie Ni Sheria ipi hiyo inaelekeza uliyoyasema
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Pole ndugu yangu mabosi vilaza wako wengi sana mofisini cha msingi ni kuwakwepa tuu ili kulinda your daily bread otherwise tafuta kazi kwingine.
  Samahani jinsia yako pls!Maana kuna binti aliwai mwambie boss wake siwezi kukuvulia chupi hauna hadhi ya kutembea na mimi.Bosi akampa adhabu kama yako kwa maelezo ya uongo!
  Kumbe mdada ana kibri as anatembea na boss wa boss wake.
   
 18. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145

  Kwa private sector sawa, ila kwa serikalini Standing Orders za 2009 zinasisitiza nusu mshahara. Kazi kweli kweli. Yaani labda mwajiri 'akupotezee' tu.
   
 19. B

  Bandio Senior Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu yangu, unatakiwa kurudi shule au kwa namna yeyote ujifunze jinsi ya kuwasiliana na watu wote bila kuwakwaza, na hasa watu wenye mamlaka juu yako kwa namana moja au nyingine.


  Hoja ya kwamba bosi wako alitaka kitu kidogo kutoka kwako sioni kama ilikuwa na uzito wa kutosha, kwani baada ya wewe kuona hali hiyo ulitakiwa kujipanga kukabiliana naye ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa kiongozi wa juu yake, taarifa TAKUKURU au kama uliona haifai basi ulitakiwa kujipanga kutafuta kazi nyingine badala ya kutoa lugha chafu kwa kiongozi wako. Angalia sasa unahaha!


  Umesema umesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, hapo nadhani unastahili kuendelea kupata mshahara wako mpaka siku ambayo uchunguzi utaisha na hatua alizozieleza ndugu Mungi kufuatwa.  Kumbuka Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya 2004 inazuia tabia ya zamani ya waajiri ya hire and fire ndio maana imeweka vyombo vya kushughulikia migogoro ya wafanyakazi na waajiri [CMA na High Court Labour Division]. Pia Kanuni za Utendaji Bora za 2007 zimeweka procedure mbalimbali halali katika kufikia kumuadabisha mfanyakazi mwenye makosa kama yako.


  Hata hivyo, usisahau kuwa kwa namna yeyote mwajiri hatakiwi na hana mamlaka ya kumfukuza kazi mfanyakazi bila kumpa nafasi ya kujieleza [akithubutu kufanya hivyo atakuwa amefanya kosa na hiyo ni unfair termination]. Haki ya kusikilizwa ni ya kikatiba.


  Once again, pole sana.
   
 20. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha uongo wewe, hiyo ni Sheria. Hivi kuna Standing Order iliyo juu ya sheria? Labda ni ya kwako!
   
Loading...