hii stori nilijua inahusu madungadunga 🙂🙂🙂🙂😛ole sana kijana kwa kusimama kwenye daldala. hakuna tofauti na kutembelea ****** then ukakaa kwenye foleni kwa zaidi ya masaa 3 , na usiombe ukajikuta AC hamna utakoma
Kweli mwamba, nami sijasahau nilisimama kwenye treni toka DSM mpaka Mwanza. Almost 40 Hours njiani, tena kwenye corridor la katikati ya viti ambapo watu hupita kila wakati kwenda mbele wengine kwenda nyuma wakikanyaga chochote na hawasikii ukilalamika. Unamwona aliyekaa analalamika ati kachoka kukaa lakini haruhusu kukupa nafasi ukae kidogo. Niliapa nikipangiwa kufanya kazi Mwanza naacha kazi. Siku hizo kulikuwapo ndege na treni tu. Mabus hayakuwapo. Ndege labda uwe na kauhusiano na kina Rostam wa siku zile, maana hata uuze kila kitu chako hufikii hata nusu ya bei ya ticket. Unamuuliza Mungu, "Nimekukosea sana kuliko binadamu yeyote hata niteseke kiasi hiki?" Weacha tu.nilishawahi kusimama kwenye treni toka dar hadi kigoma.
Hi hi hi hii! Umenikumbusha safari yangu ya treni kutoka Mwanza hadi Tabora, Mwanza nilipata room, sasa tulipofika Shinyanga nikaambiwa nitoke kwenye hicho chumba na TT maana kuna watu wanataka kuingia mle, basi ikabidi nitoke niende third class, na mizigo niliacha room niliyofukuzwa/nilikolala kabla, dah nilipata shida sana, nilikuwa std V kipindi hicho!Kweli mwamba, nami sijasahau nilisimama kwenye treni toka DSM mpaka Mwanza. Almost 40 Hours njiani, tena kwenye corridor la katikati ya viti ambapo watu hupita kila wakati kwenda mbele wengine kwenda nyuma wakikanyaga chochote na hawasikii ukilalamika. Unamwona aliyekaa analalamika ati kachoka kukaa lakini haruhusu kukupa nafasi ukae kidogo. Niliapa nikipangiwa kufanya kazi Mwanza naacha kazi. Siku hizo kulikuwapo ndege na treni tu. Mabus hayakuwapo. Ndege labda uwe na kauhusiano na kina Rostam wa siku zile, maana hata uuze kila kitu chako hufikii hata nusu ya bei ya ticket. Unamuuliza Mungu, "Nimekukosea sana kuliko binadamu yeyote hata niteseke kiasi hiki?" Weacha tu.
Siku moja nimesimama mara kaingia baba mmoja mnene anatoa mijasho kisha anatoa harufu huyo...ilikua balaa!Mwenyewe wala hajali !Mambo ya kusimama kwenye hizo dala dala hasa za route ndefu!.halafu usimame na foleni za jiji hili utajuta.
Hahahahaa! Pole sana mkuu!! Bora umeweza kumvumilia safari yote, mimi kuna siku nilipanda daladala nimezungukwa na majimama manene kweli mbele na nyuma, sasa kulikuwa na mama mmoja alikaa kwenye siti alipoinuka ili ashuke unaambiwa huyo mama hakuweza kupita maana njia ilikuwa nyembamba katikati ya daladala, unaambiwa wote waliosimama mbele karibu na mlango wa konda washuke ili majimama yashuke kwanza na ndipo huyo mjimama yakashuka, sasa cha kuchekesha, abiria alipaza sauti na kuuliza nani atashuka karibu, mjimama akajibu kuwa yeye atashuka karibu, huyo abiria akatoa amri "Wewe mama unayeshuka mbali ingia ndani kabisa kwanza alaf waingie abiria mbaumbau na huyo mama wa karibu upande maana kupishana ni mateso tu". Abiria wote walicheka sana siku hiyo!Siku moja nimesimama mara kaingia baba mmoja mnene anatoa mijasho kisha anatoa harufu huyo...ilikua balaa!Mwenyewe wala hajali !Mambo ya kusimama kwenye hizo dala dala hasa za route ndefu!.