Columbus
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 2,002
- 652
Baada ya kuishi na mke wangu kwa miaka 14 hatimaye naelekea kushindwa kumuelewa. Nilibahatika kuoa mwanamke mwenye ajira na mapato yetu yanalingana yanakaribia jumla ya 4M kwa mwezi lakini jambo la kushangaza maendeleo yetu katika familia yanasuasua. Awali tulikuwa tunaishi mjini na kodi ya nyumba ilikuwa inanigharimu sana na kwa pamoja tukaamua kutafuta kiwanja shamba nje ya mji ili tujikwamue.
Mke wangu alipata kiwanja na alinitaka tukaangalie kiwanja ambacho sikukipenda kwa kweli,kilikuwa bondeni na kinatosha nyumba tu ikatulazimu tuendelee kutafuta eneo lingine, kwa bahati nilifanikiwa kupata eneo ekari 2 kasoro na nikamjulisha mke wangu kuwa kiwanja hiki kitatufaa kwa sababu tunaweza pia kuwekeza miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku. Nilipojaribu kumshirikisha kuhusu fedha za kununulia eneo hilo alikataa na mimi niliamua kulinunua eneo hilo kwa kudunduliza mara mbili.
Nilipojaribu kumshirikisha tujenge nyumba ili tuepukane na adha ya kodi zinazopanda siku hadi siku alikataa na ikanilazimu kuanza kujenga japo kwa taratibu, baadaye niligundua aliamua kukinunua kile kiwanja cha awali na kuamua kujenga nyumba ambayo mpaka sasa anadai ni yake.
Baada ya muda wa mwaka hivi tulifanikiwa kuhamia katika nyumba ndogo ndogo niliyojenga haraka haraka japo alikuwa hataki. Kutokana na kukataa kushirikana na mimi kwa muda mrefu, niliamua kijanja kumuachia matumizi ya chakula kwa kiasi fulani ikiwamo ada ya mtoto mmoja tuliyenaye kwa vile nilikuwa naendelea kujenga nyumba nyingine yenye hadhi ya familia yetu na eneo lenyewe.
Kwa sasa tunaishi kwetu kwa uhuru, na yeye nilimsaidia kujenga banda la kuku na amefanikiwa kuwa na kuku wa mayai kama 1000 hivi, 500 wanataga na waliobaki wanakaribia kuanza kutaga na fedha zinazopatikana anajua mwenyewe anafanyia nini. Chochote ninachojaribu kumueleza tushirikiane kifedha anakataa na kudai yeye ni msaidizi tu ikiwa atapenda kufanya hivyo na mimi nina jukumu la kumtunza.
Sasa ni hivi majuzi tu ametoa kauli ambayo iliniogopesha, anadai hiyo nyumba ninayoendelea kujenga sitaimaliza na badala yake itakuwa gofu eti kwa sababu namdharau. Nimeshindwa kuelewa mimi namdharau kwa vipi, au kwa sababu simshirikishi tena kwa kazi zile ninazoamua kufanya mwenyewe kwa fedha zangu?
Baada ya kufikiria jambo hili kwa wiki nzima nimeamua kunusuru familia yangu hii, Nimeamua kuanzia sasa nitumie mamlaka kama baba wa familia kumuandikia mke wangu msimamo wangu ambapo pasipo kuufuata basi hatutaweza kuishi kama mume na mke. Nimepanga kumueleza kwamba kila mwezi tutalazimika kutoa theluthi mbili ya mishahara yetu na kumkabidhi yeye kwa ajili ya matumizi ya chakula,umeme, mishahara ya housegirl na houseboy,ada ya mtoto na ujenzi unaoendelea na kutunza kumbukumbu hizo. Pia nataka nitumie nafasi hii kumjulisha yeye kama mke wangu wa ndoa kuwa vyote tulivyonavyo ikiwemo pick up niliyonunua mwenyewe ni mali yetu kama familia ikiwa ni pamoja na nyumba aliyojenga kwa siri hapo awali.
Wanajukwaa wenzangu mnalionaje hili? nitakuwa nimeharibu au natengeneza? na je ni njia gani nzuri mbadala ambayo ningeweza kuitumia? nimekwama jamani maisha magumu.