Justine_Dannie
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 1,962
- 1,622
Habari!
Poleni na msiba wa Ndugu yetu Mutahaba kwa wale wote ambao mmeguswa na msiba huu,Hongereni mliompokea Lowassa na poleni mlio mpoteza.
Kwenye mada moja kwa moja....
Nikiwa katika kituo cha kuweka/kuongeza mafuta kwenye gari, hua kuna kitu kinanishangaza kidogo,
Ni hivi,
Anaweza tokea bwana/Bibi mmoja anaweka mafuta mpaka tanki lijae (full tank), Kisha baada ya kujaa mtu huyo huanza kulitikisa gari kana kwamba anashindilia mafuta yaendelee kuingia ilihali mashine ya mafuta imeshakata ishara ya kwamba mafuta hayana tena pa kwenda na wakati huo huo anayaona kwa macho kwamba mafuta yapo pomoni kabisa.
Swali langu..
Je kitendo hiki ni mbwembwe au kina mantiki fulani, au baada ya kitendo hicho Kuna sehemu mafuta huingia na kutengeneza nafasi kwa mafuta mengine kuendelea kuingia?
Maana nijuavyo mimi mafuta ni kimiminika (liquid) huwezi shindilia..maana dumu la maji likijaa pomoni,huna cha kufanya kutengeneza nafasi zaidi bila ya kupunguza kilichomo..
Naomba ufafanuzi wakuu.
Asubuhi njema.
Sent using Jamii Forums mobile app