Kusema ukweli ndio kosa langu?

Kusema ukweli ndio kosa langu?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,300
wakuu habari, kuna binti mmoja, ametokea kunipenda sana, ikafikia hatua, mpaka akanionyesha vituko mbali mbali, haikishia hapo, akanieleza live, kuwa ananipenda kupitia sms,kama unavyojua mtoto wa kiume, hautakiwi kulaza damu, ukiletewa mzigo, wewe kula tu, ila kabla ya kula mzigo, nikamwambia kuwa nina mpenzi wangu, yupo mkoa fulani, kwa hiyo, kama utakuwa tayari kuwa na mimi, sawa, ila jua hilo, akakubali, tena akasema ataheshimu mapenzi yetu, basi penzi likaanza, sasa imepita miezi miwili, akaanza kunipangia kuwa sitaki, kuongea na mpenzi wako mbele yangu, mara, sitaki kuongea naye, mara, naomba uwachane naye, maana mimi natosha kwako. Jana, ndio nikampa live, kuwa nilikueleza hapo awali, lakini, ni utata tangu jana, leo kachukua namba ya yule mpenzi wangu, kampogia, na kumtukana, je wadau nimfanyeje huyu binti, na je ni kweli nimekosea kusema ukweli???
 
ulikosea kuwa nae kimapenzi wakati unampenzi wako baki njia kuu michepuko siyo dili
 
Mleta mada ni DHAIFU, huyo dada anatumia udhaifu wako kufanya yote hayo. Wanawake huwa wanaanza jambo kidogo kidogo, huku wakisikilizia majibu yako, ukiwa dhaifu kudhibiti mwanzoni inakula kwako.
 
Achana na huyo binti .ongea na mpenzi wako akusamehe muendelee name maisha.
 
Huyo mpango wako hakutakiwa ajue hata sura ya mpenzi wako.

Iweje simu inakaa kihasara hasara hadi anaichukua namba?

Mpo pamoja muda wote hadi wakati wa kuongea na mpenzi wako anasikia?

You're not smarter to handle mpango wa kando.
 
tatizo kua smarter as u said hebu imagine kama angekua hana mpango wa kando yangekua haya
Huyo mpango wako hakutakiwa ajue hata sura ya mpenzi wako.

Iweje simu inakaa kihasara hasara hadi anaichukua namba?

Mpo pamoja muda wote hadi wakati wa kuongea na mpenzi wako anasikia?

You're not smarter to handle mpango wa kando.
 
Ukichanganya za kwako na za kupewa zitakusaidia kujua ufanye nini!

Ulikuwa na mpenzi tayari why kuongeza mwingine?! Je ulitegemea mambo yangekuwa kama umekanyaga ganda la ndizi..?!
 
Player never get busted...au ndio ulikuwa unajifunza u player
 
Papuchi mchezo. na wewe mwanamke umtafune akubali kabsaa kuw spare tyre! Umekamatika kirahisi kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom