wiseboy
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 2,930
- 3,310
kujistukia ni mwanzo wa ukombozi
mods sielew majina yanayotumika humu siku hizi....yani copyrite au jamaa kanihack? ngoja nibadili user name aisee
kujistukia ni mwanzo wa ukombozi
Tabia yangu hii ya kuwa natamani kila mwanamke mrembo, naichukulia kama ujinga wa hali ya juu nilionao,yaani huwa sipitwi, akionekana binti yeyote mrembo hasa aliyejazia makalio vyema, mrembo wa sura, walahi tena mwili huwa unanisisimka mie, hadi mate hunitoka kwa udenda.
Huu ni ujinga wa hali ya juu kabisa nilionao, sijui nitaacha lini ujinga huu, hili ni pepo la ngono ninalo kwa kweli, wakuu naomba sana jamani kila mmoja kwa sala na imani yake aniombee, hata mie sipendi kuwa hivi, nimejitahidi sana kuacha nimeshindwa, pombe mie na wanawake, halafu MUNGU amekuwa akiniepusha na majanga sana kama UKIMWI.
Nimepima sana afya yangu, nikajikuta niko ok, hata jana pia nimepima niko fresh, MUNGU ananilinda kwa kusudi maalumu si bure, ila kwa ujinga wangu nashindwa kutambua ukweli, laiti ningelikuwa nimetulia kitabia ningelikuwa mmoja wa vijana matajiri wakubwa katika nchi hii kwa mapesa niliyowahi kuyashika, ila dhambi ndo imenipa umaskini huu kwa ujinga wangu, MUNGU NIREHEMU NIWEZE KUKURUDIA MUUMBA WANGU,NAKUPENDA MUNGU WANGU.
mods sielew majina yanayotumika humu siku hizi....yani copyrite au jamaa kanihack? ngoja nibadili user name aisee
Mkuu unaonekana mumeo anapenda kukununulia sana vitenge vya wax, yaani hukosi kuvitaja kila siku. Hongera kwa hilo.
habar yako mkuu
Wew sio ujinga huoo
Ni uanaume....huoni zizi lenye ng'ombe kumi dume ni moja, tu
Make a step kwa kile unachotak kama vp endelea au punguza, UKITAKA KUACHA MUONE mangatara akupe mwongozo
merengo90;
Miye nnani hata niweze kumpa mwongozo? Wataka nifanya miye Mungu? Ni huyo huyo Mungu wake anayesema kuwa anampenda ndiye tu amsaidie.
Tembea hata majumba yoote ya ibada, bila weye kujitambua ni bure. Uzuri wake huyu, tayari kishajitambua kuwa analo tatizo. Atafute tu tiba ya tatizo. Si kila king'aacho ni dhahabu.
Jifunze kutokana na hao ulioshawahi tembea nao bila uhakika kwani ungekuwa na uhakika usingenda kipima. Sasa, ulishawahi jiuliza kama kwa siku hiyo hiyo uliyompata, weye ulikuwa wa ngapi? Ulishawahi jiuliza, kuna tofauti gani kati ya yule wa jana na huyu wa leo?
Nasema, hakuna tofauti, hata aweke uudi na nazi, wote wamoja tu, ingekuwa tofauti, tusingalifikia mshindo.
Wenzako tunalilia kuwa huko wewe watakakuja sugua bench huku,utaweza kula kwa macho?
mkuu ebu nipe mbinu kwanza, unawataje hao?
Kama Mungu yupo tu,atakiwa hoi juu ya kitanda ukitubu anasamehe..