Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kuna maeneo kadhaa hapa nchini pamoja na nyumbani kwangu, ambapo matangazo ya ITV & EATV (Startimes) yamekuwa yanakwama sana na kutoa picha mbaya na tena ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Sasa ni hivi kwa upande wangu ninapoona matangazo ya ITV hayaonekani vizuri huwa ni bora nikazima TV kuliko kuangalia habari ya TBCCCM.
Nawasilisha wakuu.
KILAKA.
Haaa...!? bado mnatizama hizo tv?! habari za uhakika hupatikana NHK, CNN, DW, BBC na AL JAZEERA.
Hata kwangu itv ni tatizo kweli taarifa ya habari ya saa 2 usk kutazama ni shida kubwa,startimes haitufai tena WATANZANIA na hao wafanyabiasha wa kichina wafanye biashara waache ujinga unless watapata hasara kwa upumbavu wao
Mkuu mbona hata huko itv na eatv tatizo la kuganda lipo?????
TBC ina hisa za kumwaga STARTIMES kwahiyo haishangazi sana kwa yanayotokea, sema huu ni ushamba na kushindwa kiushindani
VP kuhusu king'amuzi cha Zuku? ITV na Chanel 5 hazisumbui?
mbona startimes wanapitisha maandishi kwenye screen wakiweka wazi tatizo ni nini?? hayo maandishi yanasema 'KUNA MUINGILIANO KWENYE CHANNELS ZA ITV NA EATV NA WAMESHAWAAMBIA TCRA WATATUE HILO TATIZO KWANI LIKO NJE YA UWEZO WAO' sidhani kama kuna hujuma hapo.
mkuu hujuma hipo, kwa sababu huo muingiliano huna mda maalum ambao ni saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Hii inatokana na nini???
Mkuu baada ya kuona Uzi huu Jana ilibidi niangalie taarifa ya habari ya ITV kupitia star times ikawa inakwamakwama ila now asubuhi iko fresh kabisa.
Kwahiyo hayo maingiliano ya mawimbi yanakuwepo jioni na usiku tu
kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kuna maeneo kadhaa hapa nchini pamoja na nyumbani kwangu, ambapo matangazo ya itv & eatv (startimes) yamekuwa yanakwama sana na kutoa picha mbaya na tena ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Sasa ni hivi kwa upande wangu ninapoona matangazo ya itv hayaonekani vizuri huwa ni bora nikazima tv kuliko kuangalia habari ya tbc.
Nawasilisha wakuu.
Kilaka.
waache visingizio ushindani umewashinda wanapotea polepole
Sasa jambaz nitumie king'amuzi gan ambacho akitasumbua kwenye ITV na eatv?
KILAKA
Ni kwamba ITV na EATV wanahujumiwa na Startimes au ni wao wanaihujumu Startimes? Kumbuka kwamba, IPP Media waligoma kuweka stations zao kwa Startimes na ilifikia wakati wakaziondoa lakini baada ya kukomaliwa na TCRA, ndipo wakazirudisha! Na si hao tu, hata Star TV nao waliondoa channel kwenye Startimes lakini wakarudisha kwa kulazimishwa! Wote hao, yaani ITV, Star TV na EATV zinapatikana kwa shida sana Startimes... lakini kupitia DSTV, hakuna matatizo!
Hivyo basi, kama kuna hujuma basi hujuma hizi ni kinyume na hivyo unavyosema!
Ikiwa unahujumiwa na Startimes basi fahamu kwamba hiyo itakuwa ni hujuma pendwa kwa ITV/EATV wenyewe kwa kuwa hawataki kuwapo Startimes... hawa wanaamini njia pekee ya kufanya ving'amuzi vyao vya Digitek kuuzika sokoni ni kuiondoa ITV kutoka Startimes ambako inapatikana bure kwa watazamaji wakati ndio kituo kinachotegemewa zaidi kwa habari!Mkuu hujuma hipo, kwa sababu huo muingiliano huna mda maalum ambao ni saa 11 jioni hadi saa 5 usiku. Hii inatokana na nini???
Iweje vipi si nimeshakufafanunulia? Hawa wote, ITV, EATV na Star Tv hawataki channel zao kuwa Startimes na walishawahi kuziondoa sema wakalazimishwa kuzirudisha! Usisahau kwamba, ITV/EATV wana ving'amuzi vyao (Digitek) na Star Tv wana ving'amuzi vyao (Continental). Walitaka kujiondoa Startimes kama njia ya kuwafanya watu wanunue ving'amuzi vyao sema ndo hivyo tena, sheria ikawabana!Unamaanisha star tv,itv eatv wao ndio wanavuruga matangazo yao???
ili iweje???
Iweje vipi si nimeshakufafanunulia? Hawa wote, ITV, EATV na Star Tv hawataki channel zao kuwa Startimes na walishawahi kuziondoa sema wakalazimishwa kuzirudisha! Usisahau kwamba, ITV/EATV wana ving'amuzi vyao (Digitek) na Star Tv wana ving'amuzi vyao (Continental). Walitaka kujiondoa Startimes kama njia ya kuwafanya watu wanunue ving'amuzi vyao sema ndo hivyo tena, sheria ikawabana!