Kusaga, Ruge, na TCRA, Tusikubali Udhalilishaji Huu wa Shilawadu!. JPM Anaangalia!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi

Wale wenye access kuangalia Clouds TV, angalieni kipindi cha Shilawadu, leo wanatuonyesha upuuzi wa fumanizi la kupangwa!. Halafu kipindi hiki ndio rais wetu anakipenda na anakiangalia!. Ama kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji!.

Baada ya kusifiwa kwa kazi nzuri waliomfanyia msanii Wastara, kuliko iibua ikulu yetu na mabulungutu ya minoti last week, leo ndio wanatuletea makorokocho hadi aibu!.

Kwa vile rais ndie citizen no.1 wa nchi yetu, ukisikia rais wetu na 1st Lady wanapenda kuangalia kipindi cha Shilawadu, then Tanzania wengi tunaomkubali Magufuli, automatically tunakuwa attention kuangalia. Na beat ya ile stunt ya last week ya ubishoo wa mabulungutu ya minoti ya ikulu kumsaidia msanii Wastara, viewership ya leo imeongezeka maradufu.

Tulichoonyeshwa leo ni aibu!. Halafu ukifikiria mkuu wetu wa nchi ndio anaangalia...

Issue yenyewe ni fumanizi la mtu na mke wa rafiki yake!. Kinachoonyeshwa ni udhalilishaji wa hali ya juu!.

Kila siku wake za watu wanatongo..., na sio kosa kisheria kwa mtu kumtongo... mwanamke yoyote above the age of majority regardless of their marital status, haya ni mambo ya faragha za watu, huku ni kuingilia their right to privacy!.

Kama kila mke wa mtu anayetongozwa, angemhadithia mme wake na kuweka mtego wa fumanizi, nani wangebaki salama?. Kwanza mwanamke anayejitambua, kutokewa ni kawaida!, hawezi kuwataja kila wanao mu approach, halafu mwanaume kamili, haumpelelezi mkeo anatongozwa na watu wangapi kila siku!.

Mambo kama haya ni mambo ya magazeti ya makorokocho, lakini unapokuja kwenye TV, kipindi chenye heshima ya kuangaliwa na Mkuu wa nchi, kwa maoni yangu, this is not right!.

Kusaga na Ruge, hongereni kwa kazi nzuri ya media kukuza vipaji, lakini kwa dunia ya sasa, tusivitegemee vipaji tuu pekee, baada ya vipaji, peleka vijana shule wakapigwe japo brush tuu ya kujua nini wanaweza kuonyesha na nini ni kuingilia the right to privacy za watu!. Mshukuru nchini kwetu hatuna sheria ya pro bono kwenye kesi za madai ya udhalilishaji, mgefunguliwa kesi ya udhalilishaji hadi mngefilisiwa!, na mtu angeshinda mpunga wa maana mapema tuu asubuhi.

Kwa kumbukumbu yangu, Clouds imewahi kutozwa faini na TCRA, kwa mambo kama haya kwenye kipindi cha Take One, hawajifunzi tuu?!.

Hawa vijana wana hatari!.
Paskali
 
Haki ya kila mtu faragha imetambuliwa kwenye katiba ya Jamuhuri ya Muungano kuanika maisha ya mtu kwenye vyombo vya habari bila ridhaa ni kosa kubwa sana. Tz watu hawajui haki zao kabisa, hawa watu pamoja na Clauds kama muajiri walitakiwa kushitakiwa kwa defamation kwa udhalilishaji wao wa kutangaza vipindi bila ridhaa consent ya wale wanao hojiwa, naamini ipo siku inakuja hawa jamaa, watashtakiwa. Issue sio ku balance story issue ni consent na ushahidi kutoka kwa wahanga
 
nawaonea huruma sana sudi na kwisa mwisho wao utakuwa mbaya sana,maana kuna watu wana evidence zao za kujihusisha na ubwiaji unga plus vitendo vya ushoga,mwisho wao utakuwa mbaya sana maana wanaongeza idadi ya maadui kila kukicha
wanajaribu kuiga tmz.com ila hapa sio USA huku ni shithole,shauri zao.
 
kifungu no. 16(2)
sheria ya mwaka 1984 ib15
(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.
SHILADU hapa watakuwa wameenda kinyume na sheria yetu.
 
Wanaonyesha fumanizi la kupangwa la mtu na shemeji yake huko Ukonga/Gongo la Mboto nimeacha kuangalia

Wewe tumeona kabisa Mtu kapigwa teke la Pumbuni / Kendeni na ' Kagumia ' kabisa halafu unasema la Kupangwa? Naomba Mimi na Wewe tupange kisha nikupige bonge teke la ' Kubong'oa ' au la ' dochi ' kisha utanipa mrejesho wako wa Kutukuka.
 
Back
Top Bottom