Kurusha Mtoto Darasa . . .

Kurushwa darasa sio sheria, ni hiari.

Mie wasiwasi wangu ulikuwa kuitumia hiari hii, hao walio Tandahimba na mwalimu mmoja kama ulimi acha wafuate mfumo huo.

 
Asante kwa mchango huu

Kuna watu watu unaishi nao unakuwa unashangaa, kumbe yaweza kuwa walirushwa madarasa?

 
Watoto wanaorushwa madarasa wana mafanikio zaidi ya watoto ambao hawakurushwa madarasa?

Na mafankio ya mtoto yanapimwa kwa 'monetary value' tu? Vipi saikolojia ya mtoto? Kumpokonya utoto wake? Hivi Michael Jackson alifanikiwa?

Mafanikio ita tegemea na mtoto jinsi alivyo
personally nmesoma kwa kurushwa madarasa mengi na nlitoka class 5 to form 1 saikologically sikua affected ila kuna age ilifika still 12 niko class ya watu wa 16 hapo ilikua kimbembe maana nlikua nna wauliza maswali ya kipuuz na nlivyofika a level still a kid sasa nako pakawa shida maana akili haikua imekomaa vya kutosha
Ila katika masomo ya darasani i was smart n leading
 

#watu8 fanya fasta my kid will be among the first students hapoo ukiwa wa anza kuchakarika niambie nilete mtoto dunian nikijua shule ipo lol
 
Last edited by a moderator:


yeah huu ni mtizamo tofauti...naona walengwa wakuu hapa ni wale 'wenye uwezo' kuwasomesha watoto wao huko St Academia.

Nikiri kwamba wa kwangu pia wako huko ila sikubaliani sana na dhana ya kuwarusha darasa kwa sababu zilizoelezwa na Himidini, Kongosho, snowhite, Kaunga na wengineo. Tusiangalie fedha tu ila tuangalie makuzi ya jumla ya mtoto...maana elimu ya msingi ndio Msingi mkuu wa utambuzi na uelewa wake wa maisha na mazingira yanayomzunguka kwa ujumla
 
Last edited by a moderator:
Mie mwenyewe sikusoma la saba. Sijaona any side effects on my part. La saba ni marudio. Sema shida labda inaweza kuja kama waajiri hasahasa serikalini wakitaka vyeti vya la saba (mfano pccb).
mkuu hao pccb naona wamefikiria mbali sn namoja wapo hili la dot com generation kurushwa madarasa. kikubwa mtoto aanze shule mapema ili amalize la saba na umri mdogo.
 
kama anafanya vizuri kwanini uzimrushe darasa!!!!!!

mie nilisomaga na huyo mkaka alikuwa na akili ile mbaya.....he was a genious

yani hata mwalim akiuliza swali woote mkishindwa ye akifika kwake tu anatoa jibu......

alirushwa darasa sijui yuko wapi yule mkaka "J" namtafuta hadi kesho
 

makuzi kiaje Kaizer........

kwamba akirushwa darasa atakuwa hana akili!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kushindwa ku-cope na jamii inayokuzunguka kwa urahisi zaidi sio tatizo?

Elimu maana yake ni kuweza kabiliana na mazingira yako? Au nimepotoka?

 
makuzi kiaje Kaizer........

kwamba akirushwa darasa atakuwa hana akili!!!!!!!!
Heaven on earth hapo namzungumzia mtoto "as a whole" and not "sum of parts"

kwamba suala la kuwa na 'akili nyingi' darasani hakumfanyi asiwe mtoto. MAkuzi yake ni zaidi ya masomo ya darasani...ana networks za marafiki, ana walimu wake, ana wazazi, wazazi wa marafiki zake nk. ambao wote wanachangia katika 'kumuumba' awe mtu kamili. Ukimrusha darasa, kwa maoni yangu na wengine, unaharibu kabisa mfumo wake huu wa makuzi, na huenda ikawa na athari hasi huko mbeleni...ikiwemo kutokujitambua, kujisikia mpweke, na hata kuathiri uwezo wake kiakili kutokana na kwamba anajikuta mahali, na watu kwa wakati usio sahihi kwake kiumri.
 
Last edited by a moderator:

Mbona hujatoa 7bu ya kuiweka thred yako hapa?
 
Last edited by a moderator:
Haswaaaaa, je kumrusha mtoto kunasaidia zaidi katika hili?

Mfano mtoto karuka darasa la nne, yale maarifa ya darasa lile atabaki nayo vipi?

Na kuna watu husema darasa la saba ni marudio, je marudio hayana nafasi katika kuongeza maarifa ya mtoto?

je kumrusha mtoto kunasaidia zaidi katika hili?

Mmmh!!!
Unajua Konnie, mfumo wa elimu ya Tanzania kidogo upo tricky...kwa ngazi zote maarifa yatolewayo shuleni huwa ni mahsusi kwa wakati uliopo.
Soma uwezavyo lakini ukishindwa tu kufanya vyema katika mitihani pasi na shaka utaonekana hujaelimika...kwa kifupi wanafunzi wanasomea 'pass mark' na waalimu wanafundisha wanafunzi kupata 'pass mark'.

Sasa kwa mantiki hiyo basi, hapa Tanzania hata ukimrusha mtoto darasa bado haina shida na itamsaidia mtoto kutopoteza muda maadam uwezo anao. Maana tunachokizingatia sisi sio yale maarifa atayobakia nayo bali ni ule ufaulu ataouonesha.

je marudio hayana nafasi katika kuongeza maarifa ya mtoto?

Ubongo wetu sisi wanadamu huwa haufanani katu...A Study of Brain Anatomy inaelezea hilo
1. Wapo watu/wanafunzi wenye uwezo mkubwa sana wa kuelewa na kuhifadhi aliyoyaelewa wala yasimponyoke...
2. Wapo wengine wanaelewa kwa wakati uliopo tu lakini baada ya muda husahau kabisa...
3. Na mwisho wapo ambao hata ueleze vipi hawezi kuelewa katu.

Mtu/mwanafunzi wa kundi la kwanza ni dhahiri kuwa marudio ya namna yoyote ya jambo analolifahamu huwa ni kero tu.
Mwanafunzi huyu ni bora umbadilishie aina ya 'challenges' au maarifa, hapo ndipo suala la kurusha darasa/madarasa linapotakikana.
 
Unajuaje mtoto yuko juu kilevel na wenzie?

Anakua ana urahisi na uharaka wa kufahamu. Yuko makini, kwa ufupi tukubali kuwa kuna wale watoto intelligent kupita wenzao lkn kuna wtt wako gifted. Wao kila kitu kwao inakua kujifunza.
 
mkuu hao pccb naona wamefikiria mbali sn namoja wapo hili la dot com generation kurushwa madarasa. kikubwa mtoto aanze shule mapema ili amalize la saba na umri mdogo.

Wengi mnaosema hivi ni kwa kuwa mmeguswa na aina moja tu ya mfumo wa elimu ulioletwa na uwepo wa Capitalism....wenzenu ilikuwa lazima uguse sikio ndio uandikishwe.
 

ni kama nimeanza kukuelewa Kaizer...........

we mtoto wao akiwa genious hauwezi kumrusha darasa
 
Last edited by a moderator:

sasa si ungejirusha.!

BACK KWA TOPIC...
KAMA ANAKUTANA NA MARUDIO YA ALICHOKISOMA HAMNA SHIDA KUMRUSHA... SAIKOLOGIA SI KESI... FORM 1 FORM 2 WOTE NI AGEMATE..
 
Last edited by a moderator:
Wengi mnaosema hivi ni kwa kuwa mmeguswa na aina moja tu ya mfumo wa elimu ulioletwa na uwepo wa Capitalism....wenzenu ilikuwa lazima uguse sikio ndio uandikishwe.

tunasema hivi ili mtoto aweze kupata cheti cha primary level, vinginevyo ka uwezo wake ni mkubwa kwa madarasa ya katikati anaweza rushwa lakin darasa la saba amalize.
 

Umenigusa wewe! mpaka machozi yamenitoka kwa kumbukumbu ya dreams zangu!
 
Watoto wanaorushwa madarasa wana mafanikio zaidi ya watoto ambao hawakurushwa madarasa?

Na mafankio ya mtoto yanapimwa kwa 'monetary value' tu? Vipi saikolojia ya mtoto? Kumpokonya utoto wake? Hivi Michael Jackson alifanikiwa?

Nimetoa mfano wa Nyerere na hakuna alisema kitu
labda tuseme shule na walimu ndi waamue na sio wazazi
halafu madarasa yarushwe ya chini lakini mtihani wa mwisho lazima afanye
mfano arushwe la kwanza hadi la sita,lakini la saba iwe lazima asome na afanye mtihani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…