Kurusha Mtoto Darasa . . .

Umeongea jambo la maana sana.

Mzazi inabidi ajue anafanya nini na mtoto wake yuko hatua ipi, ndio maana wewe hukusita kumshawishi asome darasa la saba.

Sasa kuna wengine mtoto kupata A tu, anamrusha darasa. Kuna wakati mtoto anapata A ila nguvu aliyowekeza kwenye A hiyo ni kubwa mno, darasani, twisheni, kujisomea, na kadhalika.

Ukimrusha darasa inaweza leta matokeo tofauti.

 
Hiyo inawezekana kabisa, hasa watoto wengi wanaofaulu hisabati huweza kufanya vizuri katika masomo mengine pia kwa shule za msingi.

Lakini swali langu, mafanikio ya mtoto kieleimu ni uwezo wake wa kukokotoa tu?

Mimi nakumbuka shule ya msingi nipo darasa la 5 naenda kusoma na wanafunzi wa darasa la 7 na bado shule inaenda vizuri tu,,,,,,,,,,,,
 
Kwa upande mwingine ni vizuri kuwaweka watoto kwenye level yao, bora kuanzishwe shule za watoto wenye vipaji maalumu. The Boss deal hilo tulikomalie au???

Kati ya mambo ambayo natamani yaje kutokea hapa kwetu Tanzania, ni mkazo kwenye kufanya 'incubation' ya watoto kielimu tokea wakiwa wadogo.

Wallah tena nchi yetu imepoteza na inaendelea kupoteza watu wengi wenye uwezo kiakili, nina mifano mingi sana ya marafiki zangu ambao mfumo umewapoteza kabisa.

Kuna jamaa yangu mmoja tulimaliza naye elimu ya msingi, alikuwa anajua sana hisabati na tulikuwa tunasumbuana sana darasani. Baada ya kumaliza darasa la saba mimi nilihama mkoa maana nilipangiwa shule huko Arusha, wiki kama mbili nimekutana na yule mtu amini usiamini anauza duka.....what a waste!!!
 
watotoa wengi wanaosoma hizi shule za academia huwa hawamalizi la saba..akifika la tano au la sita haooo form one!
kwangu mimi naona inasaidia maana kwanza watoto especially wa kike unakuta mtoto ameshakua sana.so ni bora asome fastafasta kabla akili haijawa exposed na mambo ya dunia.
besides watoto wanaanza shule mapemaa miaka mitatu kapo shule sasa asome tena miaka saba ya nini primary..kusoma na kuhesabu tu...inabore sana...zamani mtu alikuwa anaanza shule hata na miaka kumi ..ila sasa hivi wanawahi so ni bora wachange mazingira mapema pia
 
Mafanikio ya mtoto ya kieleimu yanapimwaje?

Unaeza kuta nakompliketigi mambo bure

Huwa wanasema ya kwamba, "Elimu ni yale maarifa ambayo mtu hubakiwa nayo baada ya kumaliza shule".

Nadhani hata mafanikio ya mtoto kielimu mwisho wa siku inabidi kuyapima katika kigezo hicho.
 

Ndio maana namchombeza The Boss tuanzishe shule ya watoto wenye vipaji maalumu, elimu ya msingi 4 years, secondanry 3 years na baadaye chuo, ambapo ukiweza maliza course works zote kwa mwaka wa kwanza, wa pili ni research unapata degree yako. At the age of 18 mtoto anafanya PHD. LOL
 
Last edited by a moderator:
Nkwa mfano umemrurha darasa la 5 mpk form 1,~na PCCB wakitaka cheti cha std 7 atakitoa wapi?
Hiyo imemkuta dogo mmoja.
Na athari nyngne ye kamaliza chuo kaka yake yuko form 5.Kisaikolojia ths is eating his bro
 
Hiyo inawezekana kabisa, hasa watoto wengi wanaofaulu hisabati huweza kufanya vizuri katika masomo mengine pia kwa shule za msingi.

Lakini swali langu, mafanikio ya mtoto kieleimu ni uwezo wake wa kukokotoa tu?

na mimi nitaendele kukujibu kwa namna tofauti tu,,,,,,,,,,,,,

vipi kama mtoto wako anapata A's za Darasani na hatumii nguvu nyingi sana kuelewa jambo lolote la kimasomo na zaidi anasoma na wale waliomzidi madarasa,,,,,,,,,,,,,,
hapo kumbuka siyo anaenda kufundishwa , hapa ni kuwa anaenda kufanya nao Discussion,,,,,,,,,,,

huyu naye atakuwa anapimwa kwa kukokotoa tu?
 
Ninyi wajumbe mmechangia mada vizuri na kutufungua akili na macho lakini tumesahau shule za vijijini au shambani ambapo hakuna hata mwl mmoja vinginevyo ni mwi mkuu tu ndio yupo mwanafunzi au mzazi atawezaje kurushwa darasa angali pia vitendea kazi havipo inayo shinikizwa wanafunzi kukaa chini au kukalia mawe bila kusahau wanachangia darasa moja kuanzia la 1 hadi 7
 
Hahaha...naam mkuu hujakosea Kitemango, Msungu, Kiringo, Lusujack R.I.P, Mama Mkwizu na wengine wengi.

:focus:

poa poa mkuu , ile ilikuwa zaidi ya shule,,,,,,,,,, wakati mwingine naiona ilikuwa ni kama taasisi.
 
mdogo wangu alirushwa pia, mwakani atamaliza degree ya sheria akiwa na miaka 20. nnachokiona toka kwake, aliwahi jitambua na kujipna mkubwa akiwa mtoto, form four akapata div 2.18 na advance akapata div 1.9. Chuo anaendea kumaliza na hajawahi pata supplimentary though sijui her gpa.
 
Kongosho mahusiano ya mtoto na wengine ni sehem ya elimu, na pia kila somo analosoma mtoto lina mchango katika maisha yake ya kila siku hata kama mchango wake ni mdogo sana.

kwa mfano wengi wa wanaowarusha watoto madarasa huhakikisha kwamba zile topic za darasa aliloruka mtoto anazisoma ingawa atazisoma kwa njia tofauti na ile tuliyoizoea.

ukiangalia syllabus ya mtoto wa darasa la kwanza kwa sasa, mtoto anafundishwa mambo muhimu 3 nayo ni kusoma kuandka na kuhesabu na nidham, akishapata msingi huu ndipo darasa la pili anapojifunza mambo muhimu ma3 tena nayo ni usafi, afya ya msingi, na mazingira. darasa la tatu mtoto huyu huingia ndani zaid na kuanza kujifunza jambo muhimu zaid nalo ni lugha, darasa la nne hapa mtoto huenda ndani zaid na kuanza kujifunza mambo kwa unyumbulifu zaid kwani huanza kujifunza mazingira kwa upana wake, afya, usafi, hesabu,lugha na siasa(uraia). mafundisho haya mtoto hukua nayo hadi amalize darasa la saba. na kila darasa lina aina ya vitu vya kumfunza mtoto.
 
Last edited by a moderator:
Nkwa mfano umemrurha darasa la 5 mpk form 1,~na PCCB wakitaka cheti cha std 7 atakitoa wapi?

Hilo ndilo tatizo na kasoro za mfumo wetu wa elimu ndugu yangu...

Je unahitaji mtu aliyemaliza madarasa saba au unahitaji mtu aliyefaulu kihalali mitihani ya mwisho ya Taifa?
 
Mtoto akimbilie nini wakati bado mtoto? Unaposema mtoto anakuwa amekua sana kivipi? Amekua ghafla au alicheleweshwa shule?

Kuharibikiwa kimaisha kunaendana na kusoma shule ukiwa mkubwa tu?

Mtoto akianza na miaka mitatu maana yake atamaliza na miaka 10 darasa la sana, unamaanisha mtoto wa aina hii umuwahishe zaidi? Inaleta maana kwangu ukisema aliyeanza na miaka 8 la kwanza, awahishwe walau, lakini wa miaka 3 naye awarushwe darasa pia?

Kwanza wanawahi nini? Au ni sie watu wazima tunataka watoto waishi ndoto zetu?

 
Hakuna madhara sana, ila atakua anakosa busara fulani za umri husika kulingana na level atakayokuwepo, unaweza pata mfano hapa, ingawa sikuwahi kuvushwa darasa ila niliwahi kuanza shule maana nilikua najifunza mambo haraka, so nilianza shule nikiwa mdogo sana, ila nilikuwa nikifanya vizuri sana class, lakini inapofikia mambo mengine nje ya darasa nakua na akili za kitoto, ilinisumbua maana kila shule niliyokua nikienda i was the youngest darasani, muda mwingi nakua najisomea mwenyewe, maana wenzangu ni wakubwa na mambo yao na lugha zao hatuendani, walioweka utaratibu wa madarasa na umri hawakukosea kabisa, kwa maana elimu inayotolewa mlisho wake unalingana na umri husika, ila kama kichwani zipo sawa unaweza mrusha madarasa lakini itafikia mahali itabidi kitabia afanye marudio ya yale aliyoyakosa kutokana na umri wake, mfano, watoto wa darasa la kwanza wanakua na tabia fulani, wakifika la pili wanakua na tabia fulani, hivyo hivyo mpaka chuo, first year ni tofauti kitabia na second, third na fourth year
 
Kongosho huwezi amini mimi kaka yangu wa mwanzo alirushwa madarasa mara 2. By the time anaanza form 1 alikua ana twelve years tena alipasi yale madarasa ya wtt wenye vipaji. This means kama mtt yuko vizuri upstairs si vibaya kurushwa madarasa. Lkn hio mara nyingi teacher ndio anae suggest na sio mzazi.

Hata mimi wakati nasomesha niliwahi kurusha wtt wawili madarasa coz inakua wako juu ki level kuliko lile darasa walokuwepo so wanapoteza muda tuu.
 
Haswaaaaa, je kumrusha mtoto kunasaidia zaidi katika hili?

Mfano mtoto karuka darasa la nne, yale maarifa ya darasa lile atabaki nayo vipi?

Na kuna watu husema darasa la saba ni marudio, je marudio hayana nafasi katika kuongeza maarifa ya mtoto?

Huwa wanasema ya kwamba, "Elimu ni yale maarifa ambayo mtu hubakiwa nayo baada ya kumaliza shule".

Nadhani hata mafanikio ya mtoto kielimu mwisho wa siku inabidi kuyapima katika kigezo hicho.
 
Unajuaje mtoto yuko juu kilevel na wenzie?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…