Kura zimeshapigwa washindi walishapatikana, tuungane wana CCM kuwaunga mkono, hao ndio washindi

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
457
1,973
Wakuu tuliambiwa kuwa Uchaguzi wetu ndani ya chama uwe wazi wa haki na wa uhuru na tuchague kiongozi atakaeenda kushindana na vyama vya upinzani, maelekezo ya Mwenyekiti wetu magufuli kuwa kura ziwe za haki na za uwazi pasipo kificho yalizingatiwa.

Kila mgombea alishiriki kikamilifu kulinda kura zake na kila mgombea alishika kura zake na akazihesabu mwenyewe, kwa maana hiyo haikutokea vigisuvigisu yoyote na hakuna malalamiko yoyote na walioshinda ndio waliopita.

Hayo maneno kuwa waliopita hawakupita bali waliongozo ni maneno tu kama mbwembwe zingne, tunachokijua nikuwa kila mgombea alikabidhiwa kura zake akashikiria mwenyewe na akazihesabu mwenyewe.

Hivyo, hakuna kura zingne zitakazomfanya atangazwe mshindi labda Kama kuna watu wanawagombea wao mifukoni.

Uchaguzi ulishaisha na kila mtu amepata alichopanda hivyo ni wanaccm kuungana Kwa pamoja kuwa team na kuhakikisha kuwa tuliemchagua anashinda ubunge, urais na udiwani, hayo maneno mangine kuwa hayo yalikuwa maoni mngetuomba tu tutoe maoni hata kupitia kwenye ujumbe mfupi wa SMS, alieshinda ndio mshindi hata kama hutampenda inabid uvumilie hiyo ni haki yake na mapenzi yake na MUNGU wake tusije tukamdhulumu kwa kigezo cha unyonge wake na kuleta mvurugano mkubwa ndani ya chama na kuondoa sifa lukuki tulizopewa na dunia juu ya uwazi kwenye uchaguzi huu.

Tusije tukadhulumu haki za watu waliopata kwa visingizio, tuheshimu utu, haki na bahati ya mtu
 
Joisi mshindi ni Mr. MAGU tu kwa sababu kazi yake tunaijua, hao wengine inategemea na sera zao kwa sisi wananchi,historia na uwajibikaji wao, kupitishwa na ccm hakukupi dhamana ya kuwa mbunge au diwani , nashindwa kuelewa hiyo PHD unashindwa kujua jambo dogo namna hii
 
Back
Top Bottom