Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
Wengi tunatamani kweli kweli kujadili mijadala ya namna hii, si blah blah za majina na...
Najua mnataka niseme ntampigia:
MEMBE
SLAA
ZITTO
LOWASSA
MIGIRO
MBOWE
WASSIRA NK
Hapana. Kura ntampatia mgombea yeyote na wa chama chochote atakaye ahidi kunihakikishia yafuatayo:
(1) MAKAZI BORA, SIKUBALI KUENDELEA KUISHI KWENYE TEMBE
(2) AJIRA
(3) ELIMU BORA KWA WANANGU
(4) HUDUMA BORA ZA AFYA
(5) KUTOKOMEZA RUSHWA NA UFISADI
(6) KUHAKIKISHA HAKI KWA KILA MMOJA
(7) ATAKAYEACHA KUBEMBELEZA WAZENJ KUKAA KWENYE MUUNGANO, WAENDE WAKITAKA
(8) ATAKAYEUNDA "INDEPENDENT POLICE COMPLAINTS COMMISSION"
Suala la biashara ya demokrasia (hapa kuuza na kununua wapiga kura) ndiyo imeshika kasi Tanzania. Huu nu ugonjwa sugu ambao ni lazima wapiga kura waelimishwe sana. Kuna mwana falsafa mmoja alisema kuwa wafanye wapiga kura maskini ili mosi watawaliwe na elite class ambao kwa sasa ni watoto wa viongozi wetu, pili waweze kurubuniwa kirahisi kupitia matatizo yao ili wapige kura kwa chama hasa tawala. Kwa mantiki hii tumeona mosi ikifanya kazi kwa kasi sana na namba mbili umaskini unalazimu wapiga kura kuuza shahada kwa 5,000/= au kwa kanga na kofia kwa kuangalia tatizo la usoni bila kuona makubwa yajayo. Ni wakati sasa elimu itolewe na kuaswa kabisa kuuza demokrasia na kama ni rushwa wapokee ila siku ya uchaguzi anachagua anayefaa maana anayepigiwa kura hawezi kukulaumu maana hajui kama ni yupi aliyempigia kura. Kazi ipo Mchambuzi. Endela kutuchambulia tu.Lakini iwapo uzi huu ungekuwa unajadili PERSONALITIES fulani fulani ndio zinafaa, hakika mjadala ungefana, lakini kwa sababu unajadili ISSUES tunazotarajia wateule waje kuzifanyia kazi kama njia ya kutatua matatizo ya wananchi, wengi hawaupi mjadala huu uzito unaotakiwa; Lakini ni hawa hawa wenye hoja za personalities ndio wapo mstari wa mbele kusakama viongozi wasiofaa kwa hoja kwamba kuna masuala hawasimamii vizuri; sasa kwanini mnanunulika kuwaunga mkono kama hamjui watakuja kusimamia masuala yepi?
Hata hizo issue zikiangaliwa wanasiasa wetu wote ni waongo! Wataongopa kama wimbo wa prof. J lakini mwisho wa siku ni kujineemesha wao, familia zao, marafiki zao na wapambe wao. wengine tutaishia kukumbuka issues na kunyong'onyea tu.
Suala la biashara ya demokrasia (hapa kuuza na kununua wapiga kura) ndiyo imeshika kasi Tanzania. Huu nu ugonjwa sugu ambao ni lazima wapiga kura waelimishwe sana. Kuna mwana falsafa mmoja alisema kuwa wafanye wapiga kura maskini ili mosi watawaliwe na elite class ambao kwa sasa ni watoto wa viongozi wetu, pili waweze kurubuniwa kirahisi kupitia matatizo yao ili wapige kura kwa chama hasa tawala. Kwa mantiki hii tumeona mosi ikifanya kazi kwa kasi sana na namba mbili umaskini unalazimu wapiga kura kuuza shahada kwa 5,000/= au kwa kanga na kofia kwa kuangalia tatizo la usoni bila kuona makubwa yajayo. Ni wakati sasa elimu itolewe na kuaswa kabisa kuuza demokrasia na kama ni rushwa wapokee ila siku ya uchaguzi anachagua anayefaa maana anayepigiwa kura hawezi kukulaumu maana hajui kama ni yupi aliyempigia kura. Kazi ipo Mchambuzi. Endela kutuchambulia tu.
Pamoja na yote, lakini simply unamaanisha kura utampa Dr.Slaa, kulingana na issues ambazo umezi-list. Ni sawa na kusema nataka nikasome elimu bora ya Sheria, maana yake unataka ukasome UDSM Kitivo cha Sheria
huyo slaa kama familia imemshinda nchi ataiweza? Kama halmashauri chache zinazoongozwa na cdm zimeongoza kwa migogoro nchi ataiweza? Acheni mzaha inapofika suala la kujadili masuala nyeti ya taifa
mkuu nimeipenda hii,ila swala hapa nikuwa uchaguzi unafanyika kabla ya hayo yote,halafu wengi wa wanasiasa wanayazungumza sana haya kabla ya uchaguzi,swali mkuu,hakuna namna ya kuwawajibisha hawa wanasiasa pindi watakaposhindwa kutekeleza kile walichoahidi kuliko kukaa chini na kusubiria duru nyingine ya uchaguzi tena baada ya miaka 5?hilo unalizungumziaje kaka?
Post yako ni nzuri ila kama ni Ahadi na Kukuhakikishia hata mimi na kila mtu au Mgombea wanaweza kufanya hivyo.
Kikubwa hapa ni Uwezo, Mikakati, na Mipango haswa ndio tunataka kuona na kusikia kutoka kwa Wagombea Urais aka Taasisi ya Urais.
mchambuzi,
. nyamkang'ili is not talking about issues.
..he is openly campaigning for dr.wilbroad slaa.
..hakuna mgombea anayeweza kuyafanya hayo but dr.slaa.