Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Kura ya maoni: Zitto vs Dr Slaa

Ni nani ungependa agombee urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA?

  • Zitto Z. Kabwe

    Votes: 180 15.3%
  • Wilbrod P. Slaa

    Votes: 996 84.7%

  • Total voters
    1,176
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Nyie vjana wa cdm achen ujinga achen kijana mwenzenu agombee mbona ana uwezo?
 
Zito ni chaguo la CCM, hivyo ni bora kama tumekosa mtu wa kugombea kupitia chadema, badala ya kumpitisha Zito kabwe ni bora tuichague CCM yenyewe ambayo ndio inampigia DEBE.
Zito Kabwe ni mwanasiasa mnafiki sana na mbinafsi, na ndio maana hoja zake anataka zionekane ni za ZITO KABWE na sio za chama, sasa umaarufu wa mtu mmojammoja kwenye chama hauna tija.
 
Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:
Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.
kama ni uongo kamkamateni sasa au?
 
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.

Ningemteua DR. Wilbroad Slaa. kwa sababu
1.Amezoeleka sana huko vijijini kama mgombea wa urais Chadema ambako ndo wapiga kura wanajitokeza.
2.Busara zake kwa kiti cha urais zinafaa.
3.Amejaribu mara moja tumeona jinsi Chadema ilivyopata wafuasi wengi na # ya wabunge ilivyoongezeka.
4.Sasa hivi Zitto haaminiki tena kwa watu kama alivyokuwa zamani keshameza Ndoano.
 
Waungwana tuangalie watu wa kulinganisha katika masuala ya siasa.Tusifanye ushabiki ucokuwa na mantiki.DCT SLAA nafikiri alinganishwe na LIPUMBA na JK.KABWE zito alinganishwe na KUGA MZIRAI na DOVUTWA
 
Ningemteua DR. Wilbroad Slaa. kwa sababu
1.Amezoeleka sana huko vijijini kama mgombea wa urais Chadema ambako ndo wapiga kura wanajitokeza.
2.Busara zake kwa kiti cha urais zinafaa.
3.Amejaribu mara moja tumeona jinsi Chadema ilivyopata wafuasi wengi na # ya wabunge ilivyoongezeka.
4.Sasa hivi Zitto haaminiki tena kwa watu kama alivyokuwa zamani keshameza Ndoano.

We mke wake wa kwanza mpaka ujue busara zake..,,,cz jukwaan kazi yake kuropoka na maneno meng kuliko maelezo..!josephine hawezi kuwa our first lady n he cnt b pres..!!
 
Mtoa mada ameiunderrate Tanzania, kati ya hao wawili hakuna anayefaa kuiongoza Nchi hii labda wakope CCM Mtu kama Magufuli au Sita na waanze mapema wasingoje watakao temwa 2015 vinginevyo CCM hiyoooooooooooo!
 
Je tunataka rais wa nchi hii awe na majukumu gani? Hapo ndipo tuseme kati ya hao watajwa nani atayamudu? Kukimbilia kuwalinganisha watu wakati hatujawa na mtazamo moja juu ya kile rais ataenda kuteleza si sawa.
 
Tabia zao binafsi ziwe kioo kwa jamii, chimbuko lao lisiwe na mashaka, Wawe na hofu ya Mungu, walie na waliao wafurahi na wanaofurahi mzigo na mateso ya jamii uwe ni mzigo wao, Watanzania wanapolala njaa wayahisi maumivu hayo kwa vitendo, wanapokosa huduma za msingi kwao iwanyime usingizi, Watanzana wanapoibiwa wawe kidedea kukamata wezi na kuwashughulikia bila huruma. Wapambanishwaji hao hawana sifa hizo.
 
Nisingependa zito kabwe agombee urais kw sababu
1.zito haaminiki tena siku hiz,tofaut na yule wa buzwag
2. Hajiamin,anapenda kujipendekez(hasa kwa mafisad)ana pupa na madaraka.
3.analewa sifa mf.ubunge sio saiz yng.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom