Ni kumkosea Adabu na heshima Dr Slaa kumlinganisha na Zitto, ningewaelewa kidogo kama Zitto angeshindanishwa na mtu wa level yake kama Mnyika. Dr Slaa ni habari nyingine kabisa.
Nakunaliana nawewe kuwa Zito hajafikia wala pengine hatafika kushindana na Dr. Slaa ila sikubaliani na wewe katika ulinganifu wa pili. Zito kwa tabia na hulka zake anaangukia kwenye kundi la kina Lema. Lema ni size yale zito kabisaaaa!!!!. Mnyika yuko dunia nyingine ya mtu anayeonekana kuwa na sifa hasa za kiongozi.Mimi siwezi kutoa maoni.....kumuweka dr.slaa na zitto kishoka nadhani ni dharau sana......zitto hajafika hata robo ya dr.slaa kwa hiyo kura ya maoni ni dharau kwa kiongozi mwenye heshima km dr.slaa.....sijui labda zitto umshindanishe na shibuda ingefaa kwani hata kwa mnyika au lema haingii
tuacheni dharau kwa rais wetu
Kweli hili jamvi lina mambo.. nimejaribu kupitia posts za wachangiaji wengi. Mhh inavyoonekana wasiokubaliana na Zitto wanakosa hata uvumilivu wa kumpa credit anazostahili.. hakika kuna credit nyingi anazostahili kupewa.
Zitto ni kati ya vijana wachache wasomi, wenye uwezo wa kujenga hoja, kufanya tafiti na kusimamia anachokiamini, na kupitia sifa hizo amejikuta baadhi ya makundi ya vijana hayamuamini na na pia haya mkubali, ila vijana hao wanasahau kwamba penye mvutano wa kifikra kama mawazo huru yanazingatiwa husaidia kutufikisha kwenye mafanikio.
Ni ajabu wengi humu hudiriki kusema Zitto hastahili kulinganishwa na Mnyika, Lema nk, lakini ukiichambua cdm utagundua kwamba Zitto anahistoria ndefu yaliyokiletea chama mafanikio.. yawezekana kabisa asilingane na hao anaolinganishwa nao. Tuweke ushabiki pembeni tujadili hoja, kisiasa kuna mengi ya kupitia na yeye kwa sasa kuna mambo kadhaa yanamgharimu (kama la kutangaza kuwania urais 2015) lakini historia ya mema aliyoyafanya haifutiki na si kigezo cha kumshusha hadhi kiasi cha kumlinganisha na Shibuda. Lema namfahamu naye ananifahamu.. ukweli ana safari ndefu ya kisiasa lakini anaonekana anaanza kuimudu. Mnyika ni komavu kwenye siasa za upinzani na bado anazidi kujijengea umaarufu kama wengine, hivyo kuna kila sababu ya kujali mchango wa kila mmoja kwa nafasi yake.
Hii nidharau kubwa.Huwezi kupambanisha Barcelona FC na Lipuli ya Iringa.
ndo waliofungua ID nyingi nyingi mpya ili wampigie kibaraka mwenzao kura lakinibado naona hazitoshi, nimeshangazwa kupata 15% badala ya 0.001%Ni kweli mkuu lakini itasaidia kukata kilimilimi cha wafuasi wa Magamba hapa jamvini.Na ndiyo maana vibaraka nguli wa Magamba hapa JF wanachungulia tu hii thread na kukimbia.
Weka kura yangu kwa daktari, Mfumo wenu unakataa kunipa fursa ya kupiga kura
Ni kweli mkuu lakini itasaidia kukata kilimilimi cha wafuasi wa Magamba hapa jamvini.Na ndiyo maana vibaraka nguli wa Magamba hapa JF wanachungulia tu hii thread na kukimbia.
Kumbe kelele nyingi sana za vyura ni 15.78% tu?. Hizi kweli hazitamzuia tembo(84.22%) kunywa maji. Pro ccms wanajilaumu sana kwenye kura hii ya maoni.